Je, tume ya Uchaguzi inaona aibu kusema samahani kwa hatua walizokosea?

Je, tume ya Uchaguzi inaona aibu kusema samahani kwa hatua walizokosea?

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Mgombea Urais kupitia chadema amesema kuna hatua za kuchukua kabla ya kufikia hatua za kumuadhibu au kamati kufikia maamuzi, maswali yafuatayo ni ya kujiuliza ili tupate majibu:

1. Mgombea Urais anapo saini Fomu ya maadili, je ni chama, katibu wa chama au ni Mwenyekiti wa chama ndiye anakuwa amesaini pia?
2. Je, Mgombea urais anapo kiuka maadili ya uchaguzi, je, hawezi kuwa contacted moja kwa moja? maana yupo. mdhamini anakuwaje contacted kabla ya kijiridhisha kuwa mtuhumiwa hapatikani. Mfano kesi za mahakamani au Polisi mtuhumiwa au mshtakiwa akitafutwa anapo kosekana ndipo mdhamini huwa anahusishwa kumtafuta au kupatikana kwa mtuhumiwa au mshtakiwa, hivi tume hawalijui hili au wana watu ambao sheria kwao ni ngumu kuelewa.

3. Maadili yakielekeza kuwa mgombea anaye kiuka maadili anatakiwa kupewa nakala ya malalamiko ayajibu ndani ya masaa 48 ili baadae kamati iyapitie na imuite ajitete endapo kuna swali, je ni mujibu wa tume au kamati kuchukua hatua au kupuuzia na kufanya inavyo fikiria yenyewe. au kuna mtu anawalazimisha na kuwaelekeza la kufanya huku yeye hajui nini kinachotakiwa kufanyika, je kuna mapungufu kwa watumishi au kamati husika ya tume ya maadili au kuna makusudi.

4. Je, Kama tume na Kamati walishindwa kumpa masaa 48 ya kujieleza, na walishindwa kumfikia kumkabidhi barua kwa dispatch ili awasilishe utetezi wake mbele ya kamati, kuna haja ya kukiamini chombo hiki na watu wake?

5. Katibu wa chama kupewa barua ya kumpa mgombea urais kwa niaba ya Tume ni ku ashiria kuwa yeye amekuwa wakala wa tume ili kufikisha kile kinacho takiwa kwa mgombea? Chama kumdhamini mgombea urais na tume kujiridhisha kuwa chama kina wajibu huo wa kumpa mgombea urais ni cha kingwana?

Je, tume ya uchaguzi na kamati ya maadili wako sahihi kwa walicho kifanya (baada ya kujibu maswali yote hapo juu).
 
Chadema acheni kuweweseka, mtapigwa October hamtapata mbunge hata mmoja
 
Jibu hayo maswali hakuna anaye weweseka, subiri october 29 ndio uongee hivyo, kama huweweseki wewe kwanini unachonga sana, umelipwa kufanya kazi hii umesikia mi nalipwa.
Chadema acheni kuweweseka, mtapigwa October hamtapata mbunge hata mmoja
 
Wasaliti wa Nchi mtajuta kumsimamisha lissu hamtapata hata mbunge mmoja
Jibu hayo maswali hakuna anaye weweseka, subiri october 29 ndio uongee hivyo, kama huweweseki wewe kwanini unachonga sana, umelipwa kufanya kazi hii umesikia mi nalipwa.
 
Wasaliti wa Nchi mtajuta kumsimamisha lissu hamtapata hata mbunge mmoja
Unahangaika nini, mbona mmepata wabunge 20 waliopita bila kupingwa kwa kazi nzuri mliyoifanya, jibu maswali hapo juu kama huwezi ishia, ukirudi hapa na utopolo naku block.
 
Rais Magufuli hata asipofanya kampeni kuanzia leo ushindi ni 89% na akiendelea na kampeni hadi October 27 ushindi ni 98%
Kwann usimpelekee maoni yako aache kufanya kampeni ili apite kwa 89% mbona rabish sana, nilijua utasema utapeleka maoni sifanye kampeni kumbe.
 
Wameingia kwenye mtego mkuu mwaka huu!! Eti kumfungia Lissu lampeni siku 7 wakati CCM wanavunja sheria na taratibu wamekaa kimya

Wanasahau kuwa Kuna matokeo kutoka kwa marekani kwa wote watakaominya demokrasia kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Hawajui kumfungia Lissu kufanya kampeni kwa siku 7 ni moja ya kuminya demokrasia kwenye uchaguzi huu
 
Anafanya kampeni ili kujua changamoto chache za Watanzania zilizobaki

Na kitu kizuri mgombea wetu Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania hatetei ushoga
Kwann usimpelekee maoni yako aache kufanya kampeni ili apite kwa 89% mbona rabish sana, nilijua utasema utapeleka maoni sifanye kampeni kumbe.
 
Back
Top Bottom