Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,662
- 6,888
Leo asubuhi nemesikia kwenye redio ya East Africa, kwenye kipindi cha Supa Breakfast mambo ya tume ya uchaguzi ya kustaajabisha. Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi akiwa Mara na kusema wagombea wanaotumia lugha ya matusi na uchochezi kwenye kampeni wataondolewa kwenye karatasi ya kupigia kura. Yaani hakutakuwa na picha na majina yao.
Maswali:
1. Je, yale maandalizi ya asilimia 80% kufikia mwezi jana hayahusishi karatasi za kupigia kura?
2. Je, kama karatasi za kupigia kura zipo tayari, je wametoa aina tofauti tofauti kwa kulenga baada ya kutabiri kuwa baadhi ya wagombea watatumia lugha chafu?
3. Hizi karatasi zina ubora gani kutofautisha na fake? Hizi karatasi zinaandaliwa/ ziliandaliwa wapi?
4. Je, hii sio mbinu nyingine ya 'enguaengua'?
5. Je, haya ndio matumizi ya dola kubaki madarakani?