Je, Tumejiandaa na 'Uvamizi wa WaChina?'

Je, Tumejiandaa na 'Uvamizi wa WaChina?'

Ndugu zangu,

Jeshi la Wachina linakuja, wako wengi. Kwenye moja ya picha za magazetini hii leo, inamwonyesha Rais wetu akiwa amezungukwa na Wachina.

Rais amevalia ' Kijamaa', lakini Wachina wamevalia ' Kibepari'.

Naam, China ni taifa kubwa kiuchumi. Uchumi wake unakua kwa kasi kubwa, ni uchumi wa Kibepari.

Na idadi ya Wachina nayo ni kubwa.
Ili kuweza kushindana kibiashara, China kwa sasa inahitaji mali ghafi nyingi kwa viwanda vyake. China inahitaji nishati pia; mafuta na gesi.

Wachina wameigeukia Afrika. Wachina leo, kwa kutumia mahusiano mazuri na ya kirafiki ya kihistoria, ya tangu ya enzi za Vita Baridi vya Dunia, wanajipenyeza kila kwenye uwezekano wa kuvuna mali ghafi ikiwamo mafuta na gesi.

Nao wanakuja na ahadi za misaada ikiwamo kutujengea WaAfrika barabara, viwanja vya michezo vya kisasa na hata kumbi za Kimataifa za mikutano.

Duniani hakuna cha bure. WaChina wanavuna zaidi ya wanachotupa.

Tujiulize; tunataka nini? Tuangalie pia, masharti ya misaada ya Wachina. Tuangalie vile vile mazingira ya ajira wanazokuja nazo Wachina katika kuwekeza kwao hapa kwetu.

Ilivyo sasa, inatokea wawekezaji wa Kichina wanakuja nchini wakiwa na wafanyakazi wao, na wakati mwingine, hata vibarua wa kubeba zege wanatoka UChina. Hali hii haisaidii kutatua tatizo la ajira kwa vijana wetu.

Na hata inapotokea Wachina wakatoa ajira, basi, mazingira ya ajira huwa magumu kwa vijana wetu. Ujira ni mdogo na masharti ya kazi kwa vijana wetu huwa magumu sana.

Tujiulize pia, uwekezaji wa Wachina unatoa fursa kwa Watanzania kupata maarifa ya kiufundi na kiutawala kwenye sekta ambazo Wachina hao wanawekeza hapa nchini?

Hofu yetu, kama nchi, ni kuendelea kuwa tegemezi, hivyo masikini, huku nchi yetu ikiwa na rasilimali nyingi.

Na tujiahadhari, na ‘Uvamizi wa Wachina.’ Yumkinini umetukuta tukiwa hatujajiandaa, kama taifa.



kaka Maggid,kwa taarifa yako rais mpya wa china Xi Jinping atatembelea Tanzania hivi karibuni,jiandae kuandika habari zake.Ni ngumu sana Africa ya leo kutofanya biashara na Africa.
 
Wachina ni hatari sana nchi za Malasiya wanajua matatizo yao pia wachina hawa sio wale wa enzi hizo za utawala wa Mao ambao walikuwa wakija nchini mwetu kwa nia njema wachina wa sasa hivi ndio kwa kiasi kikubwa wanaiba magogo yetu,madini,meno ya tembo ndio maana ukisikia mzigo wa meno ya tembo ama umekamatwa China,Hongkong au vietnam ndio maana hata walipopewa urafiki hakuna cha maana kilichofanyika na ndio wanaongoza kwa vikampuni vya kitapeli kama ile iliyopewa mkataba wa kutengeneza mfumo wa maji sisemi kwa sababu nawachukia lakini wamechangia vijana wetu wasiosoma kupata ridhiki kwa sababu wanafanya hata kazi ambazo walistahili kufanya watu ambao ama hawajaenda shule au elimu yao ni ndogo nafahamu china wana makampuni makubwa ambayo yanaweza kushindana na nchi kubwa duniani lakini tujiulize kwanini kwetu zinakuja bidhaa feki wakati watu hao hao wanapeleka bidhaa bora ulaya jibu ni rahisi wanajua udhaifu wa viongozi wetu ndio maana wameamua kuja kutuua
 
Back
Top Bottom