Je, tumejipanga na ujio wa pikipiki za umeme?

Samwel Ngulinzira

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2017
Posts
1,829
Reaction score
1,972
Habari za wakati huu!

Siku ya jana nmeona tangazo la pikipiki za umeme (electric bike) zinazouzwa jijini Dar es salaam.

Nimefurahishwa kwa sababu inaonesha tunaenda na kasi ya mabadiliko kiteknolojia, lakini kuna kitu najiuliza kama tumeandaa miundombinu ya kuchaji vifaa hivi.

Tukichukulia mfano Marekani kila gas station kuna sehemu special kwa ajili ya kuchaji electric cars na serikali inafinance program hiyo.

Ukitaka kuchaji pikipiki au gari marekani ni bure kabisa na dira yao ni kwamba kufikia 2030 watatumia electric cars pekee.

Tukija kwa majirani zetu Rwanda wamemuunga mkono ndugu yetu R. Mengi kwenye uwekezaji wa matumizi ya gesi asilia (compressed natural gas) kwenye magari kupitia kampuni yake ya IPP energy. Kwa hiyo Rwanda wataanza kutumia teknolojia ya gesi kwenye magari yao.

Ningependa kujua watanzania dira yetu ni nini? Kama nchi ndogo kama Rwanda wanafanikiwa kwa nini sie tunaokusanya trillion 1.3 tushindwe?

Nawasilisha
 
swala la kutumia umeme tu haliwezekani kwanza vitu vya umeme vina range ndogo per charge unakuta kakijaa unaenda km 150 mfno sasa kama unaenda mwanza unaanzia arusha ukifika babat usimame uchaji haya kijae ufike singida uchaji tena??? siutatumia siku tatu
 
Labda ni fast charging [emoji16]
 
Habari za wakati huu!

Siku ya jana nmeona tangazo la pikipiki za umeme (electric bike) zinazouzwa jijini Dar es salaam.

Nimefurahishwa kwa sababu inaonesha tunaenda na kasi ya mabadiliko kiteknolojia, lakini kuna kitu najiuliza kama tumeandaa miundombinu ya kuchaji vifaa hivi.

Tukichukulia mfano Marekani kila gas station kuna sehemu special kwa ajili ya kuchaji electric cars na serikali inafinance program hiyo.

Ukitaka kuchaji pikipiki au gari marekani ni bure kabisa na dira yao ni kwamba kufikia 2030 watatumia electric cars pekee.

Tukija kwa majirani zetu Rwanda wamemuunga mkono ndugu yetu R. Mengi kwenye uwekezaji wa matumizi ya gesi asilia (compressed natural gas) kwenye magari kupitia kampuni yake ya IPP energy. Kwa hiyo Rwanda wataanza kutumia teknolojia ya gesi kwenye magari yao.

Ningependa kujua watanzania dira yetu ni nini? Kama nchi ndogo kama Rwanda wanafanikiwa kwa nini sie tunaokusanya trillion 1.3 tushindwe?

Nawasilisha
Hatushindwi mkuu ni swala la vipaumbele, kila mtu ana cha kwake,ni kama vile wewe unapata pesa unaamua kununua gari na mwingine ya kwake anajengea nyumba n.k...
 
Maamuzi mengi hapa nchini ya kibiashara huwa yanaathiriwa na ukitimba uliopo kwenye mifumo yetu.....kwa kuwa hao hao wanasiasa ndio wafanyabiashara
 
hizi hazitakuwa kama zile gari costar za HINO maana nazo sahivi zipo gerege tu
 
Back
Top Bottom