kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Nchi ndogo kama Rwanda mikakati yake kutafuta maendeleo inaweza hata kumstaajabisha mtu. Unakuta wako kila umoja wa ushirikiano lakini ni kwa ajili ya vigogo wao kupata ulaji. Wasipopata mambo yanakua sio mazuri. Hebu fikiri, wapo commonwealth, na ufaransa ilipowafuatilia ili warudi umoja wa francophone wakatoa sharti mtu wao kama hivyo apewe ukatibu mkuu. Na kweli wakafanikiwa kupewa kula waziri wao wa nje zamani kua katibu mkuu.
Sisi Tanzania nchi yetu ni kubwa ina fursa chungu nzima kwa nguvu kazi ya kila aina ya taaluma kutumika kutoa mchango kuendeleza taifa.
Haya mambo ya kuchukulia kama sera kuwinda nafasi za kimataifa za ulaji kupitia uongozi kwenye mashirika hadi serikali kutumia gharama kubwa kwa kupitiliza kwa kampeni sio sahihi. Hivi sasa Tulia Ackson kama rais wa mabunge duniani kwa hakika faida kubwa ni kwa mwenyewe kuliko taifa. Kama kuna ubishi waweke hesabu tuone. Binafsi naona bunge letu lenyewe haendeshi kwa maslahi mapana ya umma kwa hivyo huko nje anatafuta maslahi binafsi tu.
Mfano ni jinsi alizima hoja nzito ya Mpina ndani ya bunge. Nachosema hakuna haja kupania eti mtu wetu alipata nafasi kubwa nje bahati mbaya katutoka kabla ya kushika ofisi basi rais eti kaahidi kutoa kila msaada tuweze kupata mbadala agombee tena nafasi hiyo. Kama sio riziki sio tu. Vyeo kama hivyo itokee kama juhudi binafsi na pale ikibidi serikali kusaidia kiasi sio kupambania kufa na kupona kuzitafuta kama serikali. Ikibidi hivyo basi tujue tuna serikali imeweka mbele maslahi ya kibinafsi kama sera yake.