Mafundisho ya dini hutueleza kuwa tumeumbwa kwa mfano wa mungu. Swali langu ni kama sisi sote ni mfano wa mungu inakuaje kuna mwanamke na mwanaume? Inakuaje mwanaume anakuwa mfano wa mungu hapo hapo mwanamke pia na yeye ni mfano wa mungu?
Nimetolea mfano wa jinsia pekee lakini bado ipo mingi maana binadamu hatufanani kwa umbo wala Rang
Labda ungeuliza hivi: Ni mfano upi huo unaozungumziwa? Wanaofahamu wangejitahidi kukupa majibu!.Mimi kwa ufahamu wangu mdogo nadhani mfano na sura hapa ni zaidi ya ule unaotufanya sisi tuwe wanadamu na tusiwe malaika, bali ni hali ile inayotuweka karibu sana na Mungu kuliko wanyama. Mfano mmoja ni roho ya mwanadamu. Mungu ni roho lakini pia ametuumba sisi na kutupa inayoitwa "pumzi yake". Hatufanani na Mungu kwa jinsi ya mwili bali kwa jinsi ya roho. Mtu akifa ni roho ndiyo inayobaki hapo, mwili unarudi mavumbini.Roho inarudi kwa aliyeitoa (Mhu 12). Huko inahukumiwa kihalali kuishi na Mungu milele ama kutengwa mbali na Mungu milele. Mfano upo kwenye tabia hasa zile ambao ni asili ya mwanadamu. Matendo mema ya Mungu tuliumbwa nayo, tuliharibiwa baadaye na kuumbatia uovu, lakini huo haukua asili yetu.Mungu ni wa milele na mwanadamu aliumbwa aishi milele ila akaharibika. Hapa ndipo neno wokovu linapopata maana kubwa. Hapa ndipo Fundisho la Ufufuo sio ufufuko, bali ufufuo linapata maana. Mwanadamu anaweza kuishi maisha matakatifu akitaka kwa msaada wa Mungu mwenyewe. Nitaendelea na kuwasilisha vifungu vinavyohusika vya Biblia kwani swali ni la KiBiblia.