Je tuna wacheza mpira kama hawa?

Je tuna wacheza mpira kama hawa?

There are many like Nurdin Bakari, Salum Swedi, Nizar Khalfani, Shedrack Nsanjigwa...wanahitaji support tu. wapo wengi tu. Tatizo sasa hivi hakuna Timu, viongozi, chama cha soka, washabiki......wote mmehamia Vilabu vya ulaya....sasa sijui nani atengeneze kwenu?
 
Shukran mzee,

Hizi umeweka appearance kwenye African Cup of Champions Club (??)kama ni kitu cha kujivunia au mafanikio..na semi -final na final appearence kimsingi hizi hazihesabiki.

Shida ni vikombe tu

...kaka nadhani wewe utakuwa unashabikia "kandambili!" 🙂
 
Naombeni mnitajie japo mchezaji mpira leo hii ana kiwango cha wachezaji hawa

YANGA AFRICAN
(1)HAMISI KINYE/JOSEPH FUNGO
(2)AHMED AMASHA
(3)ATHUMAN JUMA(CHAMA)
(4)ALLAN SHOMARI
(5)CHARLES BONIFACE(MKWASA)
(6)HUSSEIN IDDI
(7)ABEID MZIBA
(8)MAKUMBI JUMA
(9)OMARI HUSSEIN
(10)FRED FELIX MINZIRO
(11)JUMA KAMPALA
KAINGILILA MAUFI, MOHAMEDI KIZERUZE NA ABDALLA KABURU
PAMBA FC
(1)PAUL RWECHUNGURA
(2)GEORGE MASATU
(3)MADATA LUBIGISA
(4)HUSSEIN MASHA
(5)MAO MKAMI
(6)DAVID MWAKALEBELE
(7)ABDALLA BORI
(8)HAMZA MPONDA
(9)KITWANA SULEIMAN
(10)FUMO FELICIAN
(11)DEO MKUKI
(12)RASHIDI MSONGA
(13)JUMA AMIRI

MBONA TUMEPOTEZA DIRI KATIKA MICHEZO TATIZO NINI?
Tatizo ni hao uliowaorodhesha maana hakuna hata mmoja aliyekwenda kucheza mpira wa kweli nje ya nchi sana sana uarabuni na indonesia. Unajua kwenye familia mtoto wa kwanza akiendelea na masomo vizuri basi wale wadogo zake watafuata kwa wivu wa maendeleo ili nao wawe kama kaka/dada yao. Hii ni sheria ya maendeleo. Siku moja nilikuwa Mkuranga (Pwani) kuna mtoto alikuwa anamsumbua mzazi wake kwa kutohudhuria shuleni ipasavyo, nilipomuuliza ni kwanini alinijibu eti wao (ukoo wao) hauna asili ya elimu. Kwa undani kuwa haoni mtu aliye mbele yake wa kumuiga. Akaendelea kusema kuwa "...hata ukienda shule kila siku utaishia kuokota kurosho kama fulani na fulani na fulani. Vivyo hivyo kwa wachezaji wetu. Swala la elimu kwa wachezaji sio ishu maana enzi hizi akina Tenga na wengine waliweka kitabu hasa.

Pia hatuna utashi (ama-uthubutu) wa kusema nataka kuwa hivi baada ya muda fulani. Tunamuachia shetani atuamulie tuwe akina nani.
 
Matangazo ya mechi kupitia kwenye radio yalichangia sana kuhisi boli lipo juu kipindi kile! Kwa ufupi mpira wa miguu Tz ulikuwa juu kati ya miaka ya sabini hadi themanini.

Baada ya miaka hiyo sauti za watangazaji wa RTD ziliweza kuwafanya wachezaji wengi kuonekana ni nyota!
 
Bila kuwasahau:
Ezekiel Greyson (jujuman)
Kesi manangu
Jumanne masimenti
Nicodemus Njohole na Elisha John
 
Matangazo ya mechi kupitia kwenye radio yalichangia sana kuhisi boli lipo juu kipindi kile! Kwa ufupi mpira wa miguu Tz ulikuwa juu kati ya miaka ya sabini hadi themanini.

Baada ya miaka hiyo sauti za watangazaji wa RTD ziliweza kuwafanya wachezaji wengi kuonekana ni nyota!

...upo sahihi kabisa!

utasikia kampira na mpira, kampira na mpira,... kumbe jamaa ndio kwanzaaaaa...yupo kwenye duru la uwanja!

Miaka hiyo unaingia mpirani na kiredio cha national, au phillips unakitega sikioni kumsikiliza mikidadi mahmoud na kina kipozi 'wakiwaongopea' wasikilizaji majumbani!
 
Back
Top Bottom