Spika wa Bunge Marekani, Nancy Pelosi amechana hotuba ya Rais Donald Trump muda mfupi baada ya kumaliza kuisoma wakati akihutubia Bunge kwa kile kilichoelezwa kuwa kiongozi huyo wa Marekani hakumpa mkono wakati anamkabidhi nakala.
Chanzo Habari: Mwananchi Online
Hivi Yule Spika Mmoja hivi wa Afrika Mashariki ‘ Pua Kitenesi ‘ ana hata ‘ Ubavu ‘ kwa Kumuiga Mwanamama ‘ Shujaa ‘ Spika Pelosi pale na Yeye Siku moja ikitokea akaonyeshwa ‘ dharau ‘ kama aliyofanyiwa Spika Mwenzake kwa Rais Mwalimu Mkemia?
Naamini huenda hapa kukawa na Somo zuri, jema na kubwa sana tu Kwake Spika ‘ Pua Kitenesi ‘ wa Afrika Mashariki na Kati.
Nawasilisha.
Tanzania hatuna Bunge ila tuna watu wanaokaa kwenye jumba la Bunge pale Dodoma karibu na CBE.
Hii kitu inatia uchungu. Mabingwa wa separation of powers John Locke, katika
Maandiko Mawili kuhusu Serikali, na
Baron de Montesquieu katika
Roho ya Sheria, walitetea
mgawanyo wa madaraka (Separation of Powers) kati ya mihimili ya kisiasa ya mahakama, bunge na Serikali.. Kanuni yao ilikuwa kuwa hakuna mtu anayestahili kuwa na uwezo wa kuchukua mamlaka yote yaT
aifa. Lengo lao ni kuleta dhana ya check and balnces, yaani vyombo hivi kila kimoja kimkague mwingine ili kuleta mizania ya utawala.Mashirika ya kisasa ya kimataifa huzingatia umuhimu wa utawala wa sheria na
utawala bora, huku waandishi wengine hutafiti uhsusiano kati ya utawala wa sheria na utawala wa ufanisi katika nchi za kisasa.
Nadharia hii ya Locke na
Montesquieu imepuuzwa kabisa na JPM. JPM amefanya wabunge watekeleze yale anayotaka yeye kwa mfano amepeleka sheria mbali mbali kwa mtindo wa miscellaneous amendments ili ziweze kumsaidia yeye au matakwa yake. Ananunua wabunge wa upinzani kwa kuwapa hela au kuwarudishia majimbo lengo likiwa ni kuwa na majority ndani ya Bunge. Spika huwa anasikia maagizo yake ndiyo maana kwenye kila shughuli ya Serikali lazima aalikwe. Jaji Mkuu amebakia kuwa mlalamikaji kama mwanchi tu. Kuna kesi nyingi zina miaka 4 sasa ambazo Mahakama inaweza kuzifuta lakini Jaji Mkuu anamsikiliza JPM anasema nini. Hata kuteuliwa kwa Jaji Mkuu kulikuwa kinyume cha Katiba. Alikaimu zaidi ya miezi 6 kitu ambacho hakipo kwenye katiba.
CAG Professor Assad aliondolewa kwa vile alikuwa anafanya kazi vile inavyotakiwa mpaka aliweza kutambua ufisadi wa Tsh 2.4 Trillion ambazo Serikali ilikuwa haijatoa maelezo zimetumikaje. Mwanasheria Mkuu wa Serikali AG Killangi ameteuliwa bila kuwa na vigezo vinavyotajwa kwenye Katiba ya JMT.
Kwa hiyo Tanzania haina Bunge kwa tafsiri halisi na wakla haina Mahakama kwa vile Rais ana uwezo wa kuwafutia kesi watuhumiwa kama alivyofuta ya wale wa Butimba. Au akawaweka ndani asiowapenda kama alivyowaweka akina Rugemalira na Kitilya n