Je, tuna Watu Jeuri (Kauzu) kama akina Nancy Pelosi katika Serikali (Tawala) zetu za Afrika hii ya sasa?

Tatizo huku kwetu Afrika wanafikiria kupitia matumbo yao na si akili zao. Ogopa kuona kiongozi anakata viuno kwenye halaiki ya watu ili tu amfurahishe aliye kwenye hatamu.
Ukijumlisha na viongozi wetu kuwa vimeo wa afya, nini kuchana hotuba, watu wanatukaniwa shangazi zao na bado wanacheka. Kulazwa India raha ndugu ukilinganisha na Mloganzila.
 
Akili yako ndogo sana wewe, kwako wewe demokrasia ni Trump kuondolewa madarakani, kwa hoja za kipuuzi za huyo mwanamke asie na mume?
Marekani wanajua, kama Clinton hakuondolewa kwa kufanya mapenzi ofisini, basi ujue Trump hawezi kuondolewa hata siku mmoja.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahaha imebidi ni like tu maana pua kitenesi kamwe hatoweza kwake hili ni jambo gumu ni kama movie ya kutisha hata kusikia tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja ya matukio ya kijinga na kitoto kabisa tunayoanza nayo mwaka huu hili ni moja wapo! Kwahiyo kwenu wazee wa kulinganisha kila kitu hili nalo ni la kuiga?
 
Maspika wengine wananguvu za kuwaonea wabunge wa upinzani tu. Hawashuhuliki na uhuru wa bunge wanashuhulika na kuua demokrasia
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenzetu wanafanyiana dharau za waziwazi na yanaisha hapohapo, atakayeshinda kwa sheria ama kwa hoja ndiye mshindi and its over. Lakini sisi waafrika mkitoka hapo haijalishi sheria imefuatwa ama lah kitakachofuata ni kuanza kuwindana kama wanyama wa mwitu.

Kwa mfano kesho kama Trump atapeleka hoja iliiyo na maslahi ya nchi, yule mama atamsifu bila hofu yoyote ile.

Hii ndiyo tofauti kubwa iliyopo kati ya Mzungu na Mwafrika.
 
Mimi simsaport yoyote pale ila hana adabu kuchana hotuba kivile hata kama mnatofautiana na raisi wa nchi.Ndio wale akina mama ndani ya ndoa wakiudhiwa tu wanasikia kichefuchefu na kuanza kufanya mambo ya ajabu.Khaaa sio poa kabisa
Kule duniani hakuna kuabudiana we ukifanya ujinga watu wanakufanyia upuuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

We dogo umenichekesha sana siku ya leo, yani unamuita ndugai ni pua kitenesi?? Lol nadhani dispilini yako ni zerooo kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…