Je, tunashuhudia heshima kwa Rais, au utamaduni wa political sycophancy unaojificha nyuma ya mila na desturi?

Je, tunashuhudia heshima kwa Rais, au utamaduni wa political sycophancy unaojificha nyuma ya mila na desturi?

Mla Bata

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2013
Posts
8,461
Reaction score
19,779
Wasalaam

Kuna jambo limenifanya nitafakari sana baada ya kuwaona baadhi ya viongozi wakifika kumpa pole Rais Samia kufuatia msiba wa mume wake.

Kutoa pole ni jambo la kibinadamu. Hapo hakuna ubishi. Rais naye ni binadamu, ana majonzi, na ni jambo jema viongozi wenzake kwenda kumfariji.

Lakini sasa tujiulize swali ambalo wengi wanaogopa kuliuliza:

Kiongozi wa kiume kupiga magoti mbele ya Rais ni heshima kweli, au ni dalili nyingine ya ile siasa yetu ya “mkuu hakosei”?


Maana kuna tofauti kati ya heshima na kujishusha.


Unapokuwa kiongozi wa umma, una heshima ya ofisi yako. Unaweza kutoa pole kwa unyenyekevu, kwa utu na kwa staha bila kuonekana kama mtu anayekwenda mbele ya mamlaka kusujudia cheo.


Kinachotia mashaka zaidi ni kwamba matukio kama haya yanaweza kuendeleza utamaduni wa viongozi kuonyesha utii wa kupindukia kwa aliye madarakani. Leo ni kupiga goti, kesho ni nini? Kesho kutwa tutaanza kuona nani anaweza kujipendekeza zaidi kuliko mwenzake?


Wanasiasa wanajua kabisa thamani ya kuonekana mwaminifu mbele ya mwenye mamlaka.Ndiyo maana swali si kama kupiga magoti ni desturi katika baadhi ya jamii. Swali ni,

katika mazingira ya uongozi wa taifa, tunataka kuona heshima ya taasisi au mashindano ya kuonyesha nani ni mtiifu zaidi kwa Rais?

Kwa maoni yangu, kiongozi anaweza kuwa mnyenyekevu bila kujidhalilisha. Anaweza kumfariji Rais kama binadamu mwenzake bila kuacha hadhi ya nafasi anayoiwakilisha.


Na kama kweli tunataka kujenga taasisi imara, basi viongozi wanapaswa kujifunza tofauti kati ya loyalty kwa nchi, heshima kwa Rais na loyalty binafsi kwa mtu aliyeko madarakani.


Hii nchi ina tatizo la viongozi kuogopa kusema ukweli mbele ya wenye mamlaka. Tusije tukaanza pia kuwa na tatizo la viongozi kuogopa hata kusimama mbele ya Rais.
Karibuni tujadili bila unafiki hii ni heshima ya kitamaduni, au tunashuhudia political sycophancy ikivaa sura ya mila na desturi?

Wasalaam,

Mla bata

München, Deutschland 🇩🇪.
 
katika mazingira ya uongozi wa taifa, tunataka kuona heshima ya taasisi au mashindano ya kuonyesha nani ni mtiifu zaidi kwa Rais?
Wanachofanya hawa ni maonyesho ya nani kaguswa zaidi na msiba huo na katika kufanikisha hilo miongoni mwa mbinu zinazotumika ni huo unyenyekevu uchwara wa kinafiki.
 
Wanachofanya hawa ni maonyesho ya nani kaguswa zaidi na msiba huo na katika kufanikisha hilo miongoni mwa mbinu zinazotumika ni huo unyenyekevu uchwara wa kinafiki.
UKiangalia mibaba mijitu mizima inavyojipinda migongo mbele ya yule mama unabakia kucheka tu, comedy at its finest.
 
Africa hususannhuko kwetu sifa kubwa ya kupata cheo ni unyenyekevu, unategemea nini?
 
11284.jpg
 
Back
Top Bottom