JE! TUTARAJIE RAIS WA MAHAKAMAa?

Karikari

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
250
Reaction score
41
Wanajf

Kwa hali halisi inayoendelea ktk Taifa letu hatuelekei kuwa na Rais wa mahakama?

Japo mimi sio mwanasheria lkn naamini mahakama zina mipaka yake.

Chombo pekee ninachoamini kinaweza kumrudishia mtumishi kazini ni Idara ya kazi ila sina uhakika kama Idara ya kazi ina uwezo wa kumrudishia mpaka cheo alichokuwa anatumikia.

Sasa kuhusu taasisi kama ya siasa au dini mahakama ina uwezo wa kuzishurutisha eti huyu jamaa lazima awe mwanachama wenu au awe Shehk au Mchungaji wenu kama amefukuzwa kundini?

Kwanza nionavyo mimi kwenye katiba yetu ya nchi hakuna cheo cha Diwani,Mbunge,Meya au Rais wa mahakama na hata cheo cha Naibu IGP.

Kwakuwa hatuna mfumo unaoeleweka wa utawala basi kutokana na udhaifu wa Mr.Dhaifu tutarajie pindi wananchi watakapomtoa mkuku atakimbilia mahakamani na ndipo tutakapokuwa na Rais wa mahakama
 
idara ya kazi pia inatumia mahakama, mahakama ni mahali haki inapatikana kwa kila mtu ikiwemo taasisi na co., mtu au taasisi inaweza kushtakiwa pale inapovunja haki, au mtu au taasisi inaweza kwenda mahakama pale inapoona haijatendewa haki,
 

hebu organise tumtoe mkuku tuone itakuaje
 
...

....nawasiwasi siku ni kimwacha mkewangu atakwenda mahakamani!!!!
 
Kila mtu ana haki ya kukimbilia mahakamani hata kama anafungua kesi ya uwongo kwa mtu, taasisi, kampuni, shirika n.k. Mfumo wa mahakama ni kusikiliza pande mbili na kutoa haki kwa upande unaostahili kupata haki hiyo. Wapo wanaokimbilia mahakamani ku-buy time na kunufaika na na hali hiyo ijapokuwa wanajua hawana hoja wala kesi ya maaana ya kwenda huko, tunayo mifano ya hao.Mlolongo wa raisi kukimbilia mahakamani labda awe amepinduliwa kama alivyo raisi Mursi wa Misri na inategemea na katiba yao. Kwa Bongo raisi kukimbilia mahakamani kwa sababu yoyote ile kwa katiba ya sasa nadhani labda labda ashinde uchaguzi na ionekane ameibiwa kura na wananchi wawe bado wanampenda, vinginevyo kwa raisi kuwa katika Ikulu ya bongo sasa hivi kama ni wewe ungeomba lolote litokee uondoke kwa amani ukapumzike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…