Je,tuuiteje?! Udini shuleni?

Je,tuuiteje?! Udini shuleni?

Wanafunzi wa shule ya sekondari Ndanda,iliyoko wilaya ya Masasi, wamefukuzwa shuleni jana. Hii ni pamoja na wanafunzi wa kidato cha sita! Sababu kubwa ni baadhi ya wanafunzi wa imani ya dini ya Kiislamu kutotimiziwa ahadi ya kujengewa nyumba yao ya ibada kwa muda mrefu sasa. Chanzo kinasema ilifikia hata 'parade' za 'assembly' asubuhi,wanafunzi wa imani hiyo,kuanza kujitenga na wenzao! Habari zaidi tutaendelea kujuzana..

Nadhani walipaswa kuhama shule tu sasa, wakasome kule wanakojua watakuwa pekeyao. Na uzuri kuna chuo pia so wataendelea na mambo hizo! watafute na kazi watakazokuwa pekeyao na maduka watakayoenda wao tu and the list continues...
ukiangalia hili pia unagundua ni mawazo finyu tu hayana uhalisia! hakuna maisha ya aina hiyo.

 
Labda huo ukumbi haujaelekea misri.
Kama mabenki wanawafeva kwa account maalumu,,mwisho watadai wawe na masoko yao,daladala na hata barabara zao.
 
kwanini wachanganyike na makafiri chumba kimoja. Wanaingia na viatu sehemu takatifu. Wasiochagua kuwa za kuingia nazo sehemu takatifu.

Nasema NO!. Hongera vijana kwa kusimamia msimamo wenu.

Mara nyingi wewe hupinga migomo yoyote dhidi ya "serikali" (mfano ule mgomo uliomalizika majuzi tu pale udsm wanafunzi wakidai wenzao waliokosa mikopo wapewe mikopo ili waendelee na masomo). Lakini hapa unaunga mkono mgomo huo kwa kujustify sababu za mgomo huu. Sasa najua kinachokumotivate. Good well done mkuu
 
Kuna mambo najaribu kujiuliza, kwa mwenyeji wa ndanda anaweza kunisaidia, kuna misikiti karibu na shule hiyo labda? wanafunzi (wanaopenda) wanaruhusiwa kwenda kuswali? Na wanaruhusiwa mda gani? kwa sababu tunajua muda wa vipindi mashuleni. na lini?
Ni kweli iko haja ya kuwa na msikiti hapo shuleni? au labda pana kanisa? je kuweka msikiti kwa sababu pana kanisa ndio njia pekee ya kutatengeneza usawa?
Hii ndiyo bottom line kwangu.
Bahati mabaya tabia za binadamu ni ngumu kuzitabiri, unaweza kukuta kwamba kuna katika hao waliogoma kuna ambao hata pangekuwa na msikiti huwa hawaendi na wala wasingekwenda kuswali.
Ukiniuliza mimi shuleni ni mahali mtu amekwenda kusoma, naelewa kila mtu ana dini yake ambayo inapaswa kuheshimiwa na ndiyo maana tukapewa siku ya ijumaa kuwa nusu siku kwa ajili ya hilo, na pia jumapili!
Huwa nakereka sana pale watu wanapoamua kufanya suala la dini kama ni la vikundi! Mmoja mmoja tunafanya mambo ya aibu halafu katika vikundi tunajifanya wamoja na kudai haki bila kujua kuwa hakuna haki iliyo bila wajibu!
Imani yangu ni kwamba, moja, hakuna dini nzuri au mbaya, kwa sababu wengi wa waumini (ukiacha wale ambao labda kwa sababu moja ama nyingine waliamua kubadili) walijikuta kwenye dini kutokana na malezi waliozaliwa wakayakuta. Mbili, dini inapaswa kutufanya tuwe wema zaidi, tupendane zaidi, kwa ujumla tutende matendo mema coz Mungu ni mmoja.

Nimeona nikujibu, neno mungu lipo katika umoja, wanaolitumia neno mungu ni wengi, na tafsiri ya mungu kwa hawa watu inaonyesha mungu si mmoja, kwa mfano, kuna mungu anasema mtu akikukosea umsamehe, mungu mwingine anasema kama mtu akikukosea tafuta bomu ukajilipue pamoja nae ujilipizie kisasi! naamini umeelewa mungu si mmoja isipokuwa neno mungu ni umoja!
 
Hata kama usipoingia na viatu lakini kama moyo ni mchafu (yaani kama umdhambi), wala haikusaidii chochote!!! Udhu wa moyoni ni bora kuliko udhu wa mwili! Jitakase moyo wako ndipo uingie nyumba ya ibada....hilo ni la muhimu zaidi!!!
kwanini wachanganyike na makafiri chumba kimoja. Wanaingia na viatu sehemu takatifu. Wasiochagua kuwa za kuingia nazo sehemu takatifu.

Nasema NO!. Hongera vijana kwa kusimamia msimamo wenu.
 
  • Thanks
Reactions: TNA
Wanafunzi wa shule ya sekondari Ndanda,iliyoko wilaya ya Masasi, wamefukuzwa shuleni jana. Hii ni pamoja na wanafunzi wa kidato cha sita! Sababu kubwa ni baadhi ya wanafunzi wa imani ya dini ya Kiislamu kutotimiziwa ahadi ya kujengewa nyumba yao ya ibada kwa muda mrefu sasa. Chanzo kinasema ilifikia hata 'parade' za 'assembly' asubuhi,wanafunzi wa imani hiyo,kuanza kujitenga na wenzao! Habari zaidi tutaendelea kujuzana..

siyo wewe ni ugonjwa wa macho unakusumbua=trachoma
 
Suluhisho ni kurudisha hiyo shule kwa wakatoliki kisha kuwafukuzia mbali hao magaidi wa alshaabab
 
serikali ina dini. Unadhani hao wanaoomba msikiti shuleni ujasiri huo wameupata wapi? Kumbuka waziri wa elimu Dr...., prsdent, vice presdnt, waziri wa mambo ya ndani na IGP wake, ma RPC, wakuu wa mikoa wao ndo wengi. Serikali kutikuwa na dini ilikuwa wakati wa nyerere na mkapa si hii. Hili liko wazi unaficha nini?
 
kuna kitu inaitwa mobile masjjid kwa ajili ya wanafunzi wanaokosa hizo huduma.
baadae nitawatumia link muwe mnapata huduma hapo hamna haja ya kugombana wakati rais aliahidi comp kwa kila mwanafunzi.
tumkumbushe hiyo ahadi alishasema ni msikivu.
 
Nadhani walipaswa kuhama shule tu sasa, wakasome kule wanakojua watakuwa pekeyao. Na uzuri kuna chuo pia so wataendelea na mambo hizo! watafute na kazi watakazokuwa pekeyao na maduka watakayoenda wao tu and the list continues...
ukiangalia hili pia unagundua ni mawazo finyu tu hayana uhalisia! hakuna maisha ya aina hiyo.


Form V na VI za kizamani ni tofauti na sasa.. Kwanza wanakuwa na umri mdogo,na nature ya kizazi cha sasa si ya kujitafutia muda na kujisomea. Wao wanalishwa vitu na magazeti pendwa,vitabu pendwa,TV,Internet ambako nako wanachagua yanayowapendeza. Tuende nan taratibu.
 
Kuna jamaa ana ushauri mbaya kule jirani. Eti, waliotaifishiwa skuli zao warejeshewe! Kila kila mwenye dini yake akasome shule inayomhusu! I really doubt some people's minds! Mi ningelikuwa rais,ningelikuwa dikteta wa kuhakikisha nchi yangu haina ubaguzi wa aina yoyote.Rangi,kabila,dini,ukanda,n.k. zinazofananazo!
 
Walioleta hayo madini yenu wanapeta tu na maisha, wanafanya maendeleo ya kueleweka na wananchi wao at least wanapata huduma muhimu, nyie mtakalia na madini yao na kuendelea kupigwa na jua tu hapa nchini, bure kabisa, imani ndio zilizotufikishahapa tulipo, rushwa imekithiri, mfumuko wa bei unatisha, nyie labda mtadai MUNGU AKIPENDA mambo yatakuwa poa, bila hata ya kuchukua hatua zozote, wapuuzi wakubwa hao wanafunzi, wache wakakeshe na misahafu, tuone kama maendeleo yao yatakuja na koran!
 
"kimuingiacho mtu ndio kimtokacho" Ikiingia hekima utatenda kwa hekima, ikiingia chuki inakutoka roho ya kujilipua.
 
... Utanzania sio udini ni UTU!!
... Utu hauna udini! Utu hauna matabaka, Utu hauna ukanda, utu hauna ukanda ...Utu ni Utanzania
 
nazan wanafunzi wamesahau kilichowapelea huko,pili tufaham km sehemu ya ibada wakitaka wajengewe inabidi waombe taasisi zao ziwajengee,wapewe kibali na serikali kujenga ndani ya eneo la shure au waamue kujenga nje,pia ifahamike kwa shule nyingi zilizokuwa za dini waliokua wanamiliki walijenga majengo ya ibada,mfano pugu minaki nk,na baada ya serikali kutaifisha majengo yakabaki km kawaida mwisho shule zetu za serikali zina changamto nyingi za msingi hasa upungufu wa vifaa,madarasa,walimu nk,hata nyumba za walimu,nazani busara itumike hasa kwenye maamuzi,ni vema wakaswali ila si lazima wajengewe na serikali maana serikali haina dini
 
Jamani jamani wandugu swala la Udini linazidi kujipenyeza taratibu da naumia sana kuhusu swala hili,any way yote haya ameyaleta Jk lakn Mungu atuepushe mbali na hili balaa
 
Jamani jamani wandugu swala la Udini linazidi kujipenyeza taratibu da naumia sana kuhusu swala hili,any way yote haya ameyaleta Jk lakn Mungu atuepushe mbali na hili balaa

Hongera mkuu! wewe ndiye mkristo ! Hawa wapumbavu wanaokashifu ni freemason! wanajenga chuki baina ya waislam na wakristo ili watimize matakwa yao! Walaaniwe wote wanao kashifu dini za watu
 
Back
Top Bottom