Je tuwakumbuke kwa yapi wazee waliozaliwa 1940-1960

Je tuwakumbuke kwa yapi wazee waliozaliwa 1940-1960

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Viongozi wetu wengi ukiacha wale wazee waanzilishi ni hawa wa 1940-1960.

Hichi ndiyo kizazi cha wasomi, mafisadi, waheshimiwa , watunga sheria karibu wote wa Tanzania ya sasa

Swali tuwakumbukaje? Kwa mazuri au hawa ndiyo sababu ya Tanzania kuwa masikini mpaka leo
 
Baba yangu amekula chumvi nyingi huo mwaka 1940 alikuwa na miaka saba. Bado akili zinafanya kazi japokuwa hasikii vizuri ukiongea haraka haraka. Ni wale wazee waliofanya kazi Tanzania ya awamu ya kwanza, waaminifu na shuleni walikuwa na akili inayofanya kazi vizuri.

Amepitia pilika pilika nyingi miaka ya shule ya msingi na sekondari bahati yake alikutana na wazee waliojua maana ya elimu tangu miaka hiyo kabla ya uhuru.

Mungu ni mwema siku zote na siku zote Mungu ni mwema.
 
Tuwapotezee tu,wengi wao walizaliwa 70s, 80s, 90s wala hawana tofauti nao sana.
 
Baba yangu amekula chumvi nyingi huo mwaka 1940 alikuwa na miaka saba. Bado akili zinafanya kazi japokuwa hasikii vizuri ukiongea haraka haraka.
Hata Ngara atakuwa haikumbuki tena. Nilimuona bushubhi mara ya mwisho 1985.
 
Baba yangu amekula chumvi nyingi huo mwaka 1940 alikuwa na miaka saba. Bado akili zinafanya kazi japokuwa hasikii vizuri ukiongea haraka haraka. Ni wale wazee waliofanya kazi Tanzania ya awamu ya kwanza, waaminifu na shuleni walikuwa na akili inayofanya kazi vizuri.

Amepitia pilika pilika nyingi miaka ya shule ya msingi na sekondari bahati yake alikutana na wazee waliojua maana ya elimu tangu miaka hiyo kabla ya uhuru.

Mungu ni mwema siku zote na siku zote Mungu ni mwema.
Sawa Ila usitufokee basi hujui Kuna Vita mjomba?
 
Nyie
Tuwapotezee tu,wengi wao walizaliwa 70s, 80s, 90s wala hawana tofauti nao sana.
Wa 2000's ndio mnapigwa na wake zenu mnavaa kata K mnalewa na wanawake bar na bado baba zenu tunawasaidia kuwatunza mademu zenu maana hamna hata hela ya kutunza wanawake kazi kunyoa viduku na kucheza betting hakuna mnachozalisha.

Wenzenu tulikuwa tunazalisha haswa chakula hakikosekani, wanawake unaoa hata sita. Tumewazaa nyie mkiwa mtu mwenye watoto wachache anao Saba au nane huko Ila unakuta jembe ana watoto 30.

Nyie katoto kamoja unakimbia mwanamke anaanza kuhangaika peke yake ndio maana wanawadharau wanarudi kwetu wahenga.

Hebu nanyi jiongezeni pale tulipoishia mtatuaibisha sana baba zenu.
 
Viongozi wetu wengi ukiacha wale wazee waanzilishi ni hawa wa 1940-1960.

Hichi ndiyo kizazi cha wasomi, mafisadi, waheshimiwa , watunga sheria karibu wote wa Tanzania ya sasa

Swali tuwakumbukaje? Kwa mazuri au hawa ndiyo sababu ya Tanzania kuwa masikini mpaka leo
Ungesema baadhi ya wazee hao ambao ni wale waliobahatika kupata nyadhifa katika nchi, lakini wewe umejumlisha wazee wote waliozaliwa kipindi hicho, umewakosea sana wazee waadilifu ambao ni wengi zaidi kuliko Hao mafisadi nk.
 
Wapewe kadi za senior citizens wa nchi hii na wapate huduma zote bila kulipia; huduma za matibabu first class, huduma za usafiri bure mara mbili kwa mwaka popote Tanzania, wapewe posho ya kujikimu walao shs. laki tano kwa mwezi wasio na makao wajengewe hosteli ya kuishi inayohudumiwa na serikali, wapewe mkutano na rais kila mwaka mara moja. Wapelekwe kwenye mbuga zetu kutalii japo mara moja kwa mwaka. Huduma zote za macho, meno sikio, moyo na maradhi yote makubwa yawe bure kwa kiwango cha first class.
 
Viongozi wetu wengi ukiacha wale wazee waanzilishi ni hawa wa 1940-1960.

Hichi ndiyo kizazi cha wasomi, mafisadi, waheshimiwa , watunga sheria karibu wote wa Tanzania ya sasa

Swali tuwakumbukaje? Kwa mazuri au hawa ndiyo sababu ya Tanzania kuwa masikini mpaka leo
Hakuna hata mmoja wa kukumbuka maana ni wapiga dili tupu na matapeli
 
Hiki kiza kikifutika Tz ndio itakua kama ulaya aaah sema kuna mitoto itaendeleza tena yale yale madudu.
 
Back
Top Bottom