JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
'Washtue' ndugu, jamaa au marafiki ili wawe sehemu ya Mjadala huu muhimu kwa 'kesho' ya Nchi yetu.
Washiriki watapata fursa ya kutoa maoni au mapendekezo na kuuliza maswali Wazungumzaji wetu
Kushiriki bofya https://jamii.app/KujipendekezaSpace
Khalifa Said (Mwandishi wa habari The Chanzo)
"Uchawa sidhani kama unazorotesha uwajibikaji, ninavyodhani mimi kitu kikubwa kinachodhorotesha uwajibikaji ni uimla, ukatili wa kidola, matumizi ya nguvu kwa polisi na mbinu nyingine za kihuni na za kishenzi zinazotumiwa na waliopa madarakani kuwanyamazisha watu ikiwemo kuwateka"
"Vijana wengi wanajikaribisha kwenye nafasi za Viongozi kwa kuwa wanaona hiyo ndio njia salama ya wao kufanikisha mambo yao mbalimbaliKama tunataka kuondoa hali hiyo tunatakiwa kuweka msingi ambao kila mchango wa Mtu unaweza kuheshimiwa tofauti na ilivyo sasa, mfano Msanii ukiimba nyimbo tofauti na wale waliopo Madarakani inakuwa ngumu kufanikiwa"
"Hautakiwi kushangaa kuona siku moja hata usiyemtegemea akajiunga kwenye timu ya hao wanaoitwa 'Machawa' kwa kuwa atakuwa anafanya hivyo ili kuweza kuishiKila Mtu anataka kuishi Maisha mazuri hivyo Uchawa sio sababu ya kukosekana kwa Uwajibikaji, matumizi mabaya ya Madaraka ndio chanzo"
"Vijana wengi wanajikaribisha kwenye nafasi za Viongozi kwa kuwa wanaona hiyo ndio njia salama ya wao kufanikisha mambo yao mbalimbaliKama tunataka kuondoa hali hiyo tunatakiwa kuweka msingi ambao kila mchango wa Mtu unaweza kuheshimiwa tofauti na ilivyo sasa, mfano Msanii ukiimba nyimbo tofauti na wale waliopo Madarakani inakuwa ngumu kufanikiwa"
"Tukiendelea kuwakandamiza Machawa tutakuwa hatusemi ukweli na hatuzungumzii tatizo la msingi ambalo ni la Dola kukandamiza Jamii"
Carlos Buto (Mkuu wa idara ya programu TCD)
Carlos amezungumzia kuhusu historia ya Uchawa, ameeleza uchawa haujanza leo katika nchi yetu, uchawa umekuwepo kuanzia kipidni cha mfumo wa chama kimoja lakini kwa hivi sasa unaonekana sana kutokana na uwepo wa mitandao ya kijamii. Ameeleza kuwa mifumo bora ya uchaguzi ndiyo inayoweza kuondoa kadhia hii ya uchawa.
"Ipo mifano ya Nchi kadhaa, mfano Nchi za Magharibi kama Norway, Ujerumani, Canada ukiangalia siasa zao sio za kubebana kwa mambo ya kusifiana, yanazingatia hoja na Utendaji wa TaasisiBoksi la Kura linaamua namna gani unamwajibisha Kiongozi, hivyo kama Kiongozi hana mwenendo mzuri wa utendaji, Kura yako ndio itakayomuwajibisha"
"Uchawa unaanzia katika ngazi ya Familia zetu, mfano ni kawaida kupokea simu na kuitwa majina kama “Mkuu” n.k. Ukishaujenga kuanzia ngazi hiyo ni ngumu kuuondoa katika Ngazi ya Taifa"
Amependekeza mabadiliko ya mifumo ya kimaisha, mfumo wa kishera na mifumo ya kitaasisi ili vitu viongozwe kwa mifumo na siyo kwa matwaka ya mtu ili kuondokana na tatizo la uchawa
Annastazia Rugambwa (Mkurugenzi wa Uchechemuzi Twaweza)
Annastazia ameeleza na kukubali kuwa uchawa ni tatizo kubwa sana na ili kuweza kutatua uongozi wa kiimla inabidi uchawa ukomeshwe. Ameleza pia kutokana na utafiti walioufanya watanzania zaidi ya 53% wanazungumzia kuhusu hali ngumu ya maisha, wengine wameelezea kuhusu ukosefu wa ajira. Ameeleza kuwa Chanzo cha uchawa ni hali ngumu ya maisha, kama wangekuwa na hali nzuri za maisha isingekuwa rahisi kwa wao kufanya uchawa kwani uchawa ni aibu.
"Wakati mwingine Uchawa unaharibu Viongozi, wapo wanaoingia wakiwa na nia ya kufanya mabadiliko kweli lakini kwa kuwa tunakuwa na tamaduni ya kuwasifia sana, wanazoea na inapotokea wanahojiwa wanakuwa wakali"
Ameeleza pia kuwa umasikini ndiyo mtaji wa viongozi na hiyo ndiyo sababu ya wao kutokupambana na umasikini kwa sababu ndiyo mtaji wao. Ameuliza kama umasikini ukiondoka machawa watatoka wapi?
"Uchawa una viwango, kuna viwango vya juu, kati na chini, hata Wanawake wapo Machawa, wanatumiwa kama ngazi ili wanaowatumia wafike wanapopataka"
Rubara (Mdau)
"Tunahitaji kupata Mifumo ya Elimu ya Uraia kama ambayo tulikuwa tunaipata Miaka ya 80Kuna uhitaji mkubwa wa kutoa Elimu ya Haki ya Mwananchi, hiyo inaanzia kwa Elimu ya Uraia"
Mwaura Robert (Mdau)
"Uchawa haupo tu kwenye Siasa kuna wakati ulifika hadi katika Mamlaka za Kisheria, uamuzi ulifanyika huku mhusika anayefanya maamuzi akilenga kupandishwa cheo"
"Kuwa na Watu ambao wanatokana na upendeleo, wanapofanya kazi duni hawawezi kuwajibishwaKwa ufupi Uchawa unaletwa na Umasikini"
Francis Nyonzo (Mdau)
"Uchawa ni kusifia tu hata kama jambo sio la kusifia, mfano tabia ya Watoto kuwa na utii bila kutoa hoja imekuwa ikitengenezwa na Wazazi na Walezi, kadiri inavyokuwa inamtengeneza Mtoto ambaye hawezi kubishana kwa hoja"
"Inatakiwa Watu wafundishwe kuwa na msimamo wa kusimamia kile wanachokiamini, hilo linatakiwa kwenda pamoja na Utawala wa Sheria"
Nkindikwa (Mdau)
"Wakati tunapata Uhuru tulikuwa na Vijana wanaoweza kuhoji Viongozi, lakini leo hawapo Vijana wa aina hiyo, sababu ni kwa kuwa wengi wao wanazingatia maslahi binafsi"
Singularity (Mdau)
"Ikitokea kikundi ambacho kinataka kuishi chenyewe bila kujali maslahi ya Watu wengine, hicho kikundi hakifai kwenye Jamii"
"Inapotokea katika Kundi la Watu Milioni moja, kati yao Watu Laki tisa wakiwa wanatoa kilio cha uhitaji Maji, wakati huohuo kundi la Watu 100 wao wanasema kila kitu kipo sawa, huo ndio Uchawa ambao hauna faida, hiyo ni kama Saratani na inatakiwa kuondolewa"
