Je Uchawi upo?

pet geo pet

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2018
Posts
508
Reaction score
788
Wakuu habari! Mimi ni mtu wa dini sana na ninaamini katika MUNGU,

Nipo maeneo ya ukanda wa pwani ninafanya kazi.

Kuna mambo yananitokea usiku nikiwa nimelala yanaendana na imani za kishirikina kabisa mpaka natamani kuacha kazi ingawa bado wiki mbili tu niondoke huku ila naziona nyingi sana.

Usiku kuna mambo yananitokea siyaelewi kabisa, yameanza hivi karibuni tu wala sio muda mrefu.

Usiku hasa mida ya saa 5 na kuendelea usingizi huwa unakata ghafla halafu moyo unaanza kuwa kama unafanya spark pia na mwili unasisimka sana. Hali hii inachukua muda mrefu ambayo unisababisha nikae macho mpaka asubuhi.

Wakuu mliokaa sana maeneo ya pwani hasa Tanga na Zanzibar, hawa watu wapoje kuhusu mambo ya kishirikina?

Mimi ni Msukuma kutoka kanda ya ziwa lakini mambo yanayonitokea sielewi kabisa. Halafu huwa ninaamini katika MUNGU. Sipendi mambo ya kishirikina.

Naombeni kujuzwa zaidi kuhusu hawa watu hasa mambo ya uchawi kwani kwa jinsi ninavyoona nafanyiwa uchawi kabisa ila hawaniwezi kwa njisi nilivyolelewa katika maisha ya Kisukuma.
 
Wakati hali hiyo inakutokea mpaka mwili unasisimka unauhakika kua ulishiba vizuri?

Mi naona hizo ni dalili za njaa mkuu na wala sio uchawi maana hata mimi nina experience katika hilo
 
Subiri waje w
Kukupurura hizo nyeti.. Ni hatare hao mku
 
Wakati hali hiyo inakutokea mpaka mwili unasisimka unauhakika kua ulishiba vizuri??

Mi naona hizo ni dalili za njaa mkuu na wala sio uchawi maana hata mimi nina experience katika hilo
Nashiba vizuri sana.
 
Kwetu tulikua tunawangiwa hadi mama akakimbia nyumba na sisi. Ikifika saa 6 usiku unasikia vishindo barazani akiwasha taa/kibatari anaona kiganja kinazima taa.
Waliniiba siku moja mama akanikuta chini ya mtungi..😂😂😂😂 Kigoma wasikie tu
 
Hivi wanapataga faida gani

Cc mshana jr
 
Au ndio moyo ushaanza kutoa spark nn maana ndio mida yenyewe hii!!!

Pole sana mkuu, omba Mungu akupe nguvu hafu jifunike shuka lala
 
Mi nashangaa ila wasukuma wengi huwaga hawaamin ktk mungu wanapenda uganga sana
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Pole sana mkuu maana mama yako alikuwa hodari wa kuona maficho ya wachawi[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nashiba vizuri sana.

Basi utakua na tatizo la hallucinations jaribu kumtafuta mbobezi wa maswala ya fiziolojia atakusaidia na tatizo lako litakwisha niamini mimi

Ila usiende kwa waganga wala kwa mchungaji eti ukaombewe hapo utabugi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Pole sana mkuu maana mama yako alikuwa hodari wa kuona maficho ya wachawi[emoji23][emoji23][emoji23]
Ahsante sana after hayo matukio nilikuja kua mtu nayefahamu sana mambo yahusio vitu hivu kwa upande kinzani (Anti witch crafts) Siwez wangiwa tena au kusumbuliwa na wachawi
 
Ungelikuwa Jews kama mimi ningelikupa maombi maalum ya kiebrania ulale unono..!
 
Kitu nilicho note kutokana na matukio ya kuwangiwa sana..
Kama una vitu mwilini vinataka uwe mganga hua vinavuta wachawi waje kukupa challenge..
 
Ndio matokeo ya "Anti witch crafts" imani ndio mwisho wa kila kitu.... imani ya kiganga itakuwa kwao na ile safi ya Mungu huwa huru ki Mungu Mungu
Kitu nilicho note kutokana na matukio ya kuwangiwa sana..
Kama una vitu mwilini vinataka uwe mganga hua vinavuta wachawi waje kukupa challenge..
 
Kitu nilicho note kutokana na matukio ya kuwangiwa sana..
Kama una vitu mwilini vinataka uwe mganga hua vinavuta wachawi waje kukupa challenge..

Nyumban kwetu walikuaga na desturi ya kufanya mazindiko na kuwachanja chale watoot wote. Mie nikawa nakwepa sana. Siku ya tukio napotea narudi usiku.

Wakawa wanani maind kuwa nitakua sina kinga. Dunia ina watu wabaya. Wataniloga.

Lakin mpaka leo nadunda. Sijawahi kulogwa wala nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…