pet geo pet
JF-Expert Member
- Jun 30, 2018
- 508
- 788
Wakuu habari! Mimi ni mtu wa dini sana na ninaamini katika MUNGU,
Nipo maeneo ya ukanda wa pwani ninafanya kazi.
Kuna mambo yananitokea usiku nikiwa nimelala yanaendana na imani za kishirikina kabisa mpaka natamani kuacha kazi ingawa bado wiki mbili tu niondoke huku ila naziona nyingi sana.
Usiku kuna mambo yananitokea siyaelewi kabisa, yameanza hivi karibuni tu wala sio muda mrefu.
Usiku hasa mida ya saa 5 na kuendelea usingizi huwa unakata ghafla halafu moyo unaanza kuwa kama unafanya spark pia na mwili unasisimka sana. Hali hii inachukua muda mrefu ambayo unisababisha nikae macho mpaka asubuhi.
Wakuu mliokaa sana maeneo ya pwani hasa Tanga na Zanzibar, hawa watu wapoje kuhusu mambo ya kishirikina?
Mimi ni Msukuma kutoka kanda ya ziwa lakini mambo yanayonitokea sielewi kabisa. Halafu huwa ninaamini katika MUNGU. Sipendi mambo ya kishirikina.
Naombeni kujuzwa zaidi kuhusu hawa watu hasa mambo ya uchawi kwani kwa jinsi ninavyoona nafanyiwa uchawi kabisa ila hawaniwezi kwa njisi nilivyolelewa katika maisha ya Kisukuma.