Je, ufanye nini kwa waliokuwa wakikudharau, wakikucheka, wakikusanifu na kufurahia mapito yako maishani pale mwenyezi mungu akikubariki kuwazidi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Je,

1. Uwalipizie Kisasi?
2. Uwasamehe na ikibidi Uwasaidie baadhi yao?
3. Uwafanyie Kufuru ya Kimatumizi?
4. Kama ni Wanaume basi kwa Makusudi utembee / ulale na Wake zao?
5. Kama ni Wanawake basi Ulale nao ( Uwakaze ) bila Huruma?
6. Uwatambie kwa Kuwakera
7. Unyamaze, utumie muda wako mwingi Kufanya Jukumu lako huku sasa Ukijijenga upya Kimaisha na ukiendelea Kumuomba na Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa BARAKA zake KUBWA na KUKUFUNGULIA MLANGO wa MAFANIKIO ya KIHESHIMA tena katika Taifa lingine?

Nasubiria tu Kusoma Maoni yenu Ok?
 
Ulipe kodi vyema na kupigania nchi bora zaidi kwa wote
 
8. Ujitenge na maisha ya uswahili. Maisha ya Kiswahili ndio kuna kufuatiliana, kuchekana, kuzodoana, kudharauliana na kuringiana.
 
Umeshasema aliyekubariki ni Mwenyezi Mungu. Yeye Mwenyezi Mungu anahitaji uwasamehe waliokukosea, imeandikwa , "Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani" Warumi 12:14
 
Umeshasema aliyekubariki ni Mwenyezi Mungu. Yeye Mwenyezi Mungu anahitaji uwasamehe waliokukosea, imeandikwa , "Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani" Warumi 12:14
Amina Mtumishi.
 
Achana nao mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…