Nicholaus Kilunga
JF-Expert Member
- Feb 15, 2014
- 1,188
- 570
Je Ugaidi anaotuhumiwa nao mh Mbowe ni ugaidi wa serikali?
Najaribu kutafakari kimyakimya kwa maandishi kuhusu mashataka aliyofunguliwa mwenyekiti wa CHADEMA mh Freeman Mbowe.
Nimejaribu kupitia rekodi mbalimbali za Mbowe tokea akiwa mwenyekiti wa vijana (BAVICHA) taifa, mpaka anakuwa mwenyekiti wa CHADEMA taifa, mbunge, mgombea urais na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Kwa takribani miaka 15 mh Mbowe amefanya siasa za upinzani kwa mafanikio makubwa,mafanikio hayo ni ya jasho na damu,amepoteza mengi kuliko amevyopata kama angeamua kujitazama yeye binafsi na famila yake kuliko sisi watanzania, na kwa kupitia yeye wapo wanasiasa walioibuka na kukulia mikononi mwake na kupata mafanikio makubwa kisiasa hapa nchini ,hapa nawazungumzia wale wanasiasa ambao kwa namna moja ama nyingine walipitia mikononi mwake,wengine wakiwa wapo vyama vya upinzani mpaka sasa, na wengine walioamua kwenda CCM na wengine wapo serikalini mpaka napoandika tafakuri hii.
Kwa muda wote huo mh Mbowe amekuwa akifanya kazi na serikali kama mwanasiasa wa upinzani na mbunge,amekuwa pia akifanya kazi na taasisi za serikali,mashirika ya umma na ya le binafsi,makampuni ya serikali na binafsi pia,amekuwa akishirikiana na taasisi za ndani na nje ya nchi,dini na vyombo mbalimbali vya habari.
Ila kwa wakati wote huo serikali na vyombo vyake havikuwa na mtazamo wa kumwona Mbowe kama gaidi ila mwanasiasa wa upinzani na mfanyabiashara, na baba wa familia,mwenyekiti wa CHADEMA na kama ilikuwa inamtazama kama gaidi kwa kipindi chote hicho, je ilikuwa inamlea gaidi?
Ama ilikuwa inamchunguza na kumwacha azunguke nchi nzima akifanya shughuli zake, akijenga chama chake na kuwafunda viongozi na wananchama wake? Tutafakari tena, kama Mbowe anatuhumiwa kwa ugaidi vipi viongozi wa serikali waliopitia mikononi mwake?je na wao tunze kuwatazama kwa jicho la ugaidi?vipi wao hawakuwa magaidi wala kufundishwa ugaidi?
Je, kwa miaka yote serikali ilikuwa inamfumbia macho gaidi mpaka alipoanza kuongoza harakati za kudai katiba mpya na masuala mengine ya kidemokrasia?
Je, serikali inataka tuamini kwamba ilikuwa inamlinda gaidi?mpaka akawa kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani? Kwa maslahi gani?
Je, serikali inafahamu athari za kutangaza kwamba imemshikilia Mbowe kwa tuhuma za ugaidi? Athari za kiuchumi, kidiplomasia na athari za kijamii?
Je, Serikali inajaribu kutuma ujumbe gani ndani na nje ya nchi?kwamba kwa sasa Tanzania tupo vitani tukiwindwa na magaidi na serikali ikipambana na magaidi?vp hao walipokuwa wanaandaa mpango huu wa kumshtaki mh Mbowe kwa tuhuma hizi,walitazama suala la utalii?walipima madhara ya shitaka hilo kimataifa na wageni wanataka kuja Tz kama watalii ama wawekezaji?
Maana kwa wenzetu huko ughaibuni neno ugaidi linamaana kubwa sana na ni neno lenye kuogofya sana ,tofauti na tawala nyingi za kiafrika zinazotumia neno hilo ama shitaka hilo kuwashinda wapinzani wao kisiasa na kuwajengea picha mbaya,jamii inaamini kesi hyo imechochewa zaidi kisiasa,hasa ikichochewa na siasa za maji taka alizokuwa ameziasisi mwendazake na ccm yake mpya,wakilenga kutaka kukifta chama kikuu cha upinzani CDM,ni bahati tu binadamu wanapanga na Mungu anaamua,.
siku hizi madai ya katiba mpya na demokrasia yamekuwa sehemu ya ugaidi? Je, tuziiteje serikali zilipita ambazo hazikuwahi kumwona Mbowe kama gaidi?je serikali imesahau maonyo waliyopewa na jaji kuhusu kesi za ugaidi wakati ule Wilfred Rwakatale kiongozi na mwanachama wa CDM wakati alipofunguliwa mashtaka ya ugaidi?kama wamesahau walejee kumbukumbu ya hukumu ile.
Huku Kwetu Kibondo Kigoma tunamsemo wetu unaosema(wuhagalikiwe ni ngona alavoma amazi, yaani aliesimamiwa na mamba mtoni ndo anaechota maji).
By Nick Kilunga