Je, ugoni ni kosa la jinai ?

Je, ugoni ni kosa la jinai ?

Mjuni Lwambo

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2012
Posts
11,133
Reaction score
12,361
Wakuu habari za leo?!

Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ugoni, wanaume kufanya mapenzi na wake za watu na wanawake kufanya mapenzi na waume za watu, hali hii sasa imechukua sura mpya baada ya kuibuka kwa mtindo wa watu waliokamatwa ugoni kulawitiwa, kuuawa na waliolawitiwa hatimae kuamua kujiua.

Mimi binafsi sielewi kwa usahihi sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu ugoni, je ni kosa la jinai, la madai au ni kosa la namna gani?
Kwa watu huambiwa kulipa fedha kiwango tofautitofauti kulingana na matakwa ya mtendewa.

Je mtu aliyekamatwa ugoni anaweza kupelekwa mahakamani?

Kuna vifungu vipi vya sheria kusupport hili?

Wakuu naomba tusaidiane kufafanua vifungu vya sheria vinavyoweza kuwa vinahusiana na suala la ugoni.

Kwa heshima naomba niwaite EMT, PETRO E Mselewa, Ruttashobolwa na mwanaJF yeyote mwenye uelewa juu ya jambo hili au yeyote atakayejisikia kuchangia, sitaki kuwasahau maswahibu NyaniNgabu na Kiranga.
 
Kwa tanganyika adultery is not a criminal offence, lakin kwa sheria za zanzibar ni kosa la jinai. Samahani vifungu sinavyo karibu ila ndivyo ilivyo. Hao wenaowatendea vitendo ulivyotaja wanafanya kosa kisheria. Adhabu inapaswa itolewe na competent court tu.
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi, na inakuwaje sasa kama sio kosa la jinai, inakuwaje aliyeshikwa ugoni anawekwa lockup, au ni kwa ajili tu ya usalama wake?, na kulipa fidia ni halali lisheria?
 
kuna kambo yanayoweza kuambatana na hilo kama usalama wake,uchunguzi wa nini kilichotokea hasa; kuna makosa yanayoweza kumtia mtu hatiani yanayoweza kuambatana na tendo la ugoni, kama: indecent assault, tresspassing etc kutegemeana na mazingira ya tukio. fidia ya polisi sio halali kisheria mana hiyo siyo kazi polisi bali ya mahakama.
 
Sawasawa mkuu, ila trespassing nadhani inaweza kuhusu tu kama huo ugoni umefanyika nyumbani kwa mtu, ila kama ni guest house naona labda ni ile indecent assault, lakini ii nayo kama mtu hakubakwa, ina imply kweli?

Kwenye suala la kulipa fidia mkuu nilikuwa namaanisha mume kwa mfano, anamtaka huyo mtu aliyemfumania na mke wake, atoe labda kiwango fulani cha fedha.
 
sawasawa mkuu, ila trespassing nadhani inaweza kuhusu tu kama huo ugoni umefanyika nyumbani kwa mtu, ila kama ni guest house naona labda ni ile indecent assault, lakini ii nayo kama mtu hakubakwa, ina imply kweli?

Kwenye suala la kulipa fidia mkuu nilikuwa namaanisha mume kwa mfano, anamtaka huyo mtu aliyemfumania na mke wake, atoe labda kiwango fulani cha fedha.

kwenye trespassing huko sahihi kabisa. Hilo swala la fidia ni kupenda kuyamaliza kimyakimya si unajua kuna vitu morally wrong but legally right . (kuondoa hiyo aibu ya kijamii ndo wanamalizana, lakini kisheria sio sahihi wenyewe wanasema mutual settlement out of court)
 
Kama ndivyo basi wake za watu wataendelea kunyemelewa
Hata kama sio criminal offence ila ni morally wrong, na ukikutwa mkuu unaweza hata kuuawa!
Kwa hiyo wake za watu sio vizuri kunyemelewa hata kama sheria iko silent!!
 
kwenye trespassing huko sahihi kabisa. Hilo swala la fidia ni kupenda kuyamaliza kimyakimya si unajua kuna vitu morally wrong but legally right . (kuondoa hiyo aibu ya kijamii ndo wanamalizana, lakini kisheria sio sahihi wenyewe wanasema mutual settlement out of court)
Mkuu kwa mfano adultery imefanyika katika mazingira ambayo hakuna trespassing wala ile assault uliyoizungumzia, wamekutwa na mwenye mke let say, halafu aliyefumaniwa kalazimishwa kutoa kiasi fulani cha fedha, je, baada ya hapo aliyetozwa fedha anaweza kwenda kushtaki mahakamani?, maana yake mkuu umesema kuwa ni moraly wrong but legally right. (​it should be noted that i am not encouraging adultery, ninajaribu tu kuliangalia hili suala kisheria.)
 
anaweza kwenda mahakamani kudai hela.yake na extra damages on the grounds of cohesion.
 
sioi mpaka vifungu vya sharia vibadilishwe tena ingekuw vzur ukimfumania mwenzi wako unaweza kuomba talaka ya bila kugawana vitu mlivy vichuma kungekwa na uoga flan hv wa kuanza moja
 
Nashangaa hawa jamaa wa Global publisher(OFM),wanao vamia watu guest kuwavamia,hawa jamaa wapuuzi sana,nawasubili siku moja waje kwangu niwaoneshe mziki wake wapuuzi sana,hata kama ni mke wa mtu mi nitajuaje kama huyu ni mke wa mtu,kwanza sifungui mlango hata kidogo,mfano katiba inasema 16.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi
kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na
unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na
mawasiliano yake ya binafsi-Katiba ya jamhuri ya muungano mwaka 1977
 
Unaweza kufungua kesi ya madai ya fidia (Soma sheria ya Ndoa No. 29 ya 1971 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kifungu cha 72 )
 
Hii OFM ni kitu gani mkuu?, na wanavamia watu katika mazingira gani?
 
Unaweza kufungua kesi ya madai ya fidia (Soma sheria ya Ndoa No. 29 ya 1971 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kifungu cha 72 )
Kama hautojali mkuu ungetuwekea hiyo sheria ya ndoa ili tuijadili kwa faida ya wote!!
 
sioi mpaka vifungu vya sharia vibadilishwe tena ingekuw vzur ukimfumania mwenzi wako unaweza kuomba talaka ya bila kugawana vitu mlivy vichuma kungekwa na uoga flan hv wa kuanza moja
Kwa hiyo mkuu wasipoweka hiyo sheria ndio huoi kabisa?
 
Back
Top Bottom