Mpe pole kwa Niaba na pole na wewe pia
Asilimia hamsini ya wagonjwa wa Asthma(Pumu) ni kutokana na kurithi , ni hali ya kiafya ambayo huamshwa na allergy(sometimes non allergic) isio na matibabu ya moja kwa moja lakini hali hio inaweza kudhibitiwa na madawa pamoja na mgonjwa kupewa elimu mahsusi namna ya kuepuka visababishi kama vile kubadili mtindo wa kimaisha.
Good news ni kwamba ukishafahamu namna ya kuishi nao hautokusumbua mara kwa mara na kuingilia shughuli zako za kila siku...
Ni vyema mgonjwa kufuata maelekezo na kujua visababishi vya tatizo lake na hii itamrahisishia sana hali hio isimtokee mara kwa mara.
Nakazia hakuna tiba mbadala ambayo itauondoa huu ugonjwa zaidi ya kuzuia dalili zake tu , hivyo mshauri mgonjwa kuzingatia elimu na maelekezo anayopewa na watu wa maswala ya afya.