Pre GE2025 Je, Ugumu wa Maisha na Ukosefu wa ajira kwa vijana inawezekana kikawa Chanzo cha CCM kushindwa Uchaguzi ujao?

Pre GE2025 Je, Ugumu wa Maisha na Ukosefu wa ajira kwa vijana inawezekana kikawa Chanzo cha CCM kushindwa Uchaguzi ujao?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Asilimia kubwa sana ya Watu wana MAISHA MAGUMU

Asilimia kubwa ya vijana hawana AJIRA

Lazima CCM watashindwa au kuwa wa mwisho au kushika Mkia

Je, CCM watapata kura wapi wakati asilimia kubwa ya watu wana hali ngumu?
hao wenye maisha magumu ndio kutwa wanaimba mama mama unafikri wanajitambua basi
 
Asilimia kubwa sana ya Watu wana MAISHA MAGUMU

Asilimia kubwa ya vijana hawana AJIRA

Lazima CCM watashindwa au kuwa wa mwisho au kushika Mkia

Je, CCM watapata kura wapi wakati asilimia kubwa ya watu wana hali ngumu?
Vijana wakiisimamia vizuri shughuli ya uchaguzi hakika CCM watakuwa chama Cha upinzani by october 2025. Vijana wanapitishwa katika tanuru la moto mkali mno. Mfano wanasafirishwa km kibao kufuata usaili muda huo Wana CCM wanao watu wao tayari. Kama kutakuwa na namna ya kuwaunganisha vijana nchi nzima kupambania na ma CCM naunga mkono hoja hiyo.
 
Asilimia kubwa sana ya Watu wana MAISHA MAGUMU

Asilimia kubwa ya vijana hawana AJIRA

Lazima CCM watashindwa au kuwa wa mwisho au kushika Mkia

Je, CCM watapata kura wapi wakati asilimia kubwa ya watu wana hali ngumu?
Tanzania Kuna maisha magumu na ukosefu wa Ajira kweli? Au unatania?
 
Jibu litaanzia hapa.
 

Attachments

  • IMG-20250131-WA0005.jpg
    IMG-20250131-WA0005.jpg
    124.4 KB · Views: 4
Tanzania Kuna maisha magumu na ukosefu wa Ajira kweli? Au unatania?
Acha unafiki na usaniiiii 🤣 Kama ajira zingekuwepo, usingekuwa Chawa. Wewe ni chawa tu 🤣 🤣 Ndio maana unajitoa akili kusifia kila kitu ili mkono uende kinywani 🤣🤣
 
Wanaoipigia kura na kuibeba ccm hata JF hawaijui
 
Asilimia kubwa sana ya Watu wana MAISHA MAGUMU

Asilimia kubwa ya vijana hawana AJIRA

Lazima CCM watashindwa au kuwa wa mwisho au kushika Mkia

Je, CCM watapata kura wapi wakati asilimia kubwa ya watu wana hali ngumu?
Hao ni mtaji wa CCM...

Ikishafika uchaguzi wanapewa Tshirt ,wanapikiwa Ubwabwa ,wanapewa elfu 10 za kwenda mikutanoni.
 
Kwa vyovyote vile kete ni 2 kuu.

1.Tume ya Uchaguzi iko chini ya CCM
2.Jeshi la polisi liko chini ya CCM

Mkiweza kubadili hayo ndio mfikirie vinginevyo. Otherwise CCM iko pale pale
 
Kwa vyovyote vile kete ni 2 kuu.

1.Tume ya Uchaguzi iko chini ya CCM
2.Jeshi la polisi liko chini ya CCM

Mkiweza kubadili hayo ndio mfikirie vinginevyo. Otherwise CCM iko pale pale
 
Shida ni kwamba wengi wao wameamua kuwa chawa kwahiyo wameona bora wajisalimishe kwenye makwapa ya ccm wakiamini watapata chochote kitu.
 
Ukosefu wa ajira na ugumu wa maisha kuwabebesha viongozi kuwa ni chanzo ni dalili ya IQ ndogo.Ajira ni aina ya kazi ihusishayo kutumikishwa na kulipwa ujira.Ili ajira ziwepo sharti mabwanyenye(bourgeosis) waongezeke ili wagombanie makabwela(proletariat) wahitajike.Bila ya kufanya kazi inawezekana?Ugumu wa maisha utatatuliwa pasipo kufanya kazi?Hao viongozi mwataka wawafanye muwe 'doley'(kuishi kama wazee wa TASAF)?
 
Acha unafiki na usaniiiii 🤣 Kama ajira zingekuwepo, usingekuwa Chawa. Wewe ni chawa tu 🤣 🤣 Ndio maana unajitoa akili kusifia kila kitu ili mkono uende kinywani 🤣🤣
Nchi hii usipopata hela au kazi imeamua mwenyewe mama alishagungua Nchi kitambo 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DFauhm5NN_2/?igsh=d2U5ZzNhNG1lZWZk

Watu wanatengeneza Ndege hapa hapa Bongo wewe unasema hakuna Ajira na maisha magumu? Uko serious kweli? 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DFaHJJ2t7Bl/?igsh=NDM3cnJtMnhmdWg=
 
Tatizo ni kwamba Chama Cha Mashetani ushindi wao hautegemei uchaguzi.Uchaguzi ni 'hadaa' tu.
 
Asilimia kubwa sana ya Watu wana MAISHA MAGUMU

Asilimia kubwa ya vijana hawana AJIRA

Lazima CCM watashindwa au kuwa wa mwisho au kushika Mkia

Je, CCM watapata kura wapi wakati asilimia kubwa ya watu wana hali ngumu?
Kwani siku zote wanapata kura wapi watashinda tu kwa kishindo CCM ni ileile wezi wa kura, Jasiri haachi asili. Wagombea wote wa upinzani watakatwa watawabakisha wachache kisha hao wachache wataenda kudhurumiwa kwenye sanduku la kura. hakuna uchaguzi Bongo tena kama Zanzibar ambako kuna uchaguzi wa mapema ile uchaguzi wa Mapema tu CCM wanakuwa tayari wameshinda ACT wanapewa viti vyao viwili vya kupozwa, kazi imeisha. Mimi sijisumbui kwenda kupiga kura mwaka huu hata kwa mizinga kwa mazingira haya, nitajipikia ugali wangu tu najilia nasikiliza matokeo, wala hainiumi kwasababu utawafanya nini wababe. Tena safari hii mapema kuna mijigari ya ajabu ajabu ya Mapolisi fanya fyoko kama hajakutoa utumbo. Wanao jidai kupiga piga vikelele ni CHADEMA wala hata nao hawana kitu, Lisu na heche wake watashikwa kama kuku wenye mdondo kwio, kwio, kwio, kwio hao wanaenda kufanywa Mboga, hii mikiki ya safari hii si kitoto.
 
Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025, moja ya masuala makubwa yanayoibuka ni ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira, hasa miongoni mwa vijana. Hali hii inatoa taswira wazi ya changamoto zinazowakabili wananchi, na inaweza kuwa sababu kubwa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushindwa katika uchaguzi ujao. Katika makala hii, tutachambua jinsi masuala haya yanavyoweza kuathiri matokeo ya uchaguzi.

Ugumu wa Maisha

Maisha ya kila siku yanaonekana kuwa magumu zaidi kwa wananchi wengi, hasa vijana. Bei za bidhaa za vyakula, mafuta, na huduma mbalimbali zinaendelea kupanda, huku mishahara ikibaki palepale. Hali hii inawafanya vijana wengi kujihisi wameachwa nyuma, na hivyo kuathiri morali yao katika kushiriki katika shughuli za kisiasa na kiuchumi.

Wakati vijana wanahangaika kutafuta njia za kujikimu, ni vigumu kwao kuungana na harakati za kisiasa zinazohusisha CCM. Wanapojaribu kuangalia mustakabali wao, wanakutana na ukosefu wa ajira, ambao ni tatizo kubwa nchini. Hii inawafanya wengi kuamini kuwa chama hiki hakiwezi kutatua matatizo yao, na hivyo wanajikuta wakitafuta mbadala katika vyama vingine vya siasa.

Ukosefu wa Ajira

Ukosefu wa ajira ni moja ya changamoto kubwa zinazowakabili vijana nchini Tanzania. Kwa mujibu wa takwimu, idadi kubwa ya vijana wanahitimu vyuo na shule za sekondari, lakini nafasi za ajira hazitoshi. Hali hii inawafanya vijana wengi kukosa matumaini na kuwa na ghadhabu dhidi ya serikali na viongozi wao.

Mwanasiasa anayeshindwa kutoa suluhu kwa tatizo hili anaweza kukabiliwa na hasara kubwa katika uchaguzi. Wakati vijana wanapokosa ajira, wanajikuta wakishindwa kuboresha maisha yao na familia zao. Hali hii inaweza kupelekea vijana kuwa na mitazamo hasi kuhusu CCM, na hivyo kuamua kutoshiriki katika uchaguzi au kuhamasishwa kuunga mkono vyama vingine.

Matokeo ya Kisiasa

Ukosefu wa ajira na ugumu wa maisha yanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika upeo wa kisiasa nchini. Wakati vijana wanapojisikia kukataliwa na mfumo wa kisiasa, wanakuwa na uwezekano mkubwa wa kuhamasika na vyama vya upinzani. Hali hii inaweza kupelekea CCM kupoteza kura nyingi katika uchaguzi ujao.

Vijana wanaweza kuhamasishwa na viongozi wa upinzani ambao wanaonekana kuwa na sera zinazowagusa moja kwa moja. Wakati viongozi wa CCM wanaposhindwa kutatua matatizo ya msingi, kama vile ajira na ugumu wa maisha, wanaweza kupoteza uaminifu wa vijana, ambao ni kundi muhimu katika uchaguzi.

Hitimisho

Katika muktadha huu, ni wazi kuwa CCM inakabiliwa na changamoto kubwa kuelekea uchaguzi wa 2025. Ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira ni masuala yanayohitaji umakini wa hali ya juu. Kama chama hakiwezi kutoa suluhu kwa matatizo haya, kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza kura nyingi, hasa kutoka kwa vijana.

Kama CCM itataka kubaki katika uongozi, itahitaji kuja na mipango madhubuti ya kuboresha maisha ya wananchi, hususan vijana. Sera zinazolenga kutoa ajira na kutatua matatizo ya kiuchumi zitakuwa muhimu. Viongozi wa CCM wanapaswa kujifunza kutoka kwa maoni ya vijana na kufanya kazi kwa karibu nao ili kujenga imani na ushirikiano.

Katika ulimwengu wa kisasa, vijana wanahitaji kuona matokeo ya haraka na ya dhahiri katika maisha yao. Wanahitaji viongozi wanaowajali na wanaoweza kuleta mabadiliko chanya. Ikiwa CCM itashindwa kuonekana kama chama kinachoweza kutatua matatizo haya, kushindwa katika uchaguzi ujao kutakuwa ni jambo la kutokea.

Kwa hivyo, ni jukumu la CCM kuchukua hatua sasa ili kuhakikisha kuwa inabaki kuwa chaguo la kwanza kwa vijana. Hii itahitaji siasa za uwazi, ushirikiano na jamii, pamoja na mipango ya maendeleo inayowalenga vijana.

Hili litakuwa ni jambo la msingi katika kuhakikisha kuwa chama kinapata uungwaji mkono wa kutosha katika uchaguzi ujao.
Mkuu hongera, maliwazo jipe mwenyewe. Ila vijana tuko bize na kutafuta mkate wa familia. Maisha yanasonga mbele na CCM ni hii hii.
 
Back
Top Bottom