siyo hivyo mkuu, ni hivi:-
Hicho unachokizungumzia wewe kinaitwa 'severance pay', ni malipo anayolipwa mfanyakazi endapo mwajiri wake ndo amesitisha ajira yake. Mfanyakazi anayestahili malipo haya ni yule ambaye ajira yake imesitishwa na mwajiri wake na sio kwa makosa ya mwajiriwa mwenyewe na pia mfanyakazi anatakiwa awe amefanya kaz kwa mwajiri wake kwa muda usiopungua miez 12 mfululizo.
Hivyo basi jinsi ya kulipwa hiyo 'severance pay' ni unachukuliwa mshahara wa siku 7 wa mwajiriwa unazidishwa mara 12 (miez 12 au mwaka mmoja) alaf unazidishwa mara 10. Hii kumi ni miaka ambayo inachukuliwa kwamba huyu mwajiriwa angeweza kufanya kaz kwa mda huo. Ila hii miaka 10 mwajiri anaweza anaweza kuamua kuiongeza kama hana kinyongo na wewe na wala hamna bifu na hivyo mshiko nao utaongezeka. Unaweza ukasoma kifungu 42 cha sheria ya kazi ya mwaka 2004