Je ukiachishwa kazi,unalipwa kwa muda gan uliotumikia?

Je ukiachishwa kazi,unalipwa kwa muda gan uliotumikia?

jashmoe32

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Posts
1,089
Reaction score
424
nlikua nnaulizia kuhusu sheria ya kazi ya Tanzania kua Kampuni ikiwa inavunja mkataba kwa mfanyakazi inamlipa mshahara wa wiki Moja tu kwa mwaka yani unalipwa mshahara wa siku 7 tu katika mwaka ambao mtu amefanya Kazi au mana sioni kama haki inatendeka kwa hiyo hela mana haimfikishi popote mfanyakazi na ndo kitu kinachoendelea katika Migodi ya Barrick,ni kweli hii sheria ipo?
 
siyo hivyo mkuu, ni hivi:-
Hicho unachokizungumzia wewe kinaitwa 'severance pay', ni malipo anayolipwa mfanyakazi endapo mwajiri wake ndo amesitisha ajira yake. Mfanyakazi anayestahili malipo haya ni yule ambaye ajira yake imesitishwa na mwajiri wake na sio kwa makosa ya mwajiriwa mwenyewe na pia mfanyakazi anatakiwa awe amefanya kaz kwa mwajiri wake kwa muda usiopungua miez 12 mfululizo.
Hivyo basi jinsi ya kulipwa hiyo 'severance pay' ni unachukuliwa mshahara wa siku 7 wa mwajiriwa unazidishwa mara 12 (miez 12 au mwaka mmoja) alaf unazidishwa mara 10. Hii kumi ni miaka ambayo inachukuliwa kwamba huyu mwajiriwa angeweza kufanya kaz kwa mda huo. Ila hii miaka 10 mwajiri anaweza anaweza kuamua kuiongeza kama hana kinyongo na wewe na wala hamna bifu na hivyo mshiko nao utaongezeka. Unaweza ukasoma kifungu 42 cha sheria ya kazi ya mwaka 2004
 
Mkuu je mimi niliefanya kaz kwa miez 7 na siku 10,na hatukuwa na mkataba wowote!,nimeachishwa kaz bla maelezo yoyote
 
Back
Top Bottom