Je,ulimwengu hauna namna yoyote ya utunzaji kumbukumbu?

Je,ulimwengu hauna namna yoyote ya utunzaji kumbukumbu?

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Habarini waungwana,Leo tena mbele yenu huku nikiwa na swali nyeti kidogo ambalo limejikuta tu likilanda kwenye fikra zangu!..

Je, ulimwengu hauna namna yoyote ya utunzaji kumbukumbu..?

Nikiandika ulimwengu naomba ichukuliwe vitu vyote kwa maana ya nyota, sayari zote,Galaxy n.k kiujumla vyote vinavyounda ulimwengu..
Zalisho la swali langu limetokana na hoja hii let's say ktk sayari nyengine ambayo hatujawahi kuifikia kuwe na viumbe hai wawe na mambo yao,utamaduni wao,teknolojia zao n.k lkn kwa bahati mbaya kukatokea angamizo ambalo hakutafanya chochote kibaki! I mean chochote kile hata hiyo sayari isibaki yote iteketee au hata Kama ikibaki basi kumbukumbu zote za juu ya uhai kuhusu hiyo sayari vyote vikafutika na kuteketea!.. then baada ya muda mrefu au mfupi binadamu aweze kufika kwenye sayari hiyo au eneo hilo ilipokuwepo sayari husika na atakapofanya tafiti asipate taarifa yoyote ya kwamba sayari husika iliwahi kuwa na uhai!,japo kabla ya angamizo ilikuwa na uhai!.. hapo ndipo swali langu linapokuja je, ulimwengu hauna namna yoyote ya utunzaji wa kumbukumbu(taarifa) juu ya kitu fulani kuwa kiliwahi kuwepo hata kama kilishapotea kitambo..???

Au hili swali litahitaji kujua laws zote za ulimwengu zinavyofanya kazi..? Kama ulimwengu haubakizi(hautunzi taarifa) kwanini iwe hivyo..?
Au bado hatujapata ujuzi wa kudetect ishara zote zinazozalishwa ktk ulimwengu ndio maana tunakosa majibu baadhi ya maswali..? Namaanisha taarifa huenda zipo lkn hatujajua namna ya kuzidetect hii inakuwa na mfano wa kiziwi anaweza kuona mwanga wa radi ila hasikii muungurumo!.. 😅

Naishia hapo kwa walionielewa karibuni tujadili.
 
Ngoja tufikirie swali lako kupitia mfano huu kwanza

Ukiwa na flash drive ambayo ime contain documents muhimu sana ambazo hujazi share sehemu nyingine halafu ikatokea mtu kai-format au kaitumbukiza flash drive kwenye acid ikayeyuka yote, je katika ulimwengu huu wa teknohama kuna IT mwenye uwezo wa ku backup hizo data?

Tuje kwenye swali lako mkuu

Vipi kama tuki advance miaka hiyo tukaweza kurudi nyuma ya wakati (time travel) tukarudi miaka ya nyuma enzi za uhai wa hiyo sayari tukashuhudia kilichotokea tukawa na historia ya hiyo sayari?
 
Is time travel possible au ni theory tu..? Tuanzie hapa kwanza.
 
Is time travel possible au ni theory tu..? Tuanzie hapa kwanza.
Ni theory ambayo imepewa probability kubwa katika uwezekano wake kufanyika huku asilimia ndogo ikionesha kutowezekanika

Binafsi naamini kwa miaka ijayo inawezekana watu wakasafiri katika muda ila hizi propaganda sijui pastor gani alirudi nyuma ya wakati kipindi cha yesu na kumpiga picha ni uwongo
 
Time travel kwenda future theoretically ukisafir near light speed au ukienda karibu Na black holes inawezekana....Lakini time travel kurudi past ndiyo haiwezekani...

Ingekuwa inawezekana watu wa future ambao wangeigundua, wangekuwa wamesharudi past miaka yetu Na wangekuwa wameshaithibitisha (tungepata evidence).
Na ingetengenez paradox nyingi Sana, mfano mtu arudi past kumuua Hitler, Je vita vya pili havitokei? Na Sisi Je sasaivi itakuwaje??tutaamka asubuhi Na kusahau Kila kitu kuhusu vita vya pili??vipi kuhusu impact yake? Uadui wa ujerumani Na urusi utapotea ghafla? Au mtu arudi past akawaue homo erectus wote, Je binadamu wote wangepotea? Na Sisi tutapotea wote?
Au mtu akirudi past akamuua mama Ake, Je Huyo mtu atazaliwa?? Na kama hatazaliwa, Je aliwezaje kukua Na Kuwa mtu mzima aliyeweza kutengeneza mashine ya kurudi past??
 
Bonge la nondo
 
Kunao wanaodai kwamba maji yanatunzaga kumbukumbu....... bado tunafuatilia ukweli wake

Kuhusu time travel sishabikii uwezekano wake katika hii physical world it is impossible.

Muda ni mabadiliko, unaweza kuyachelewesha au kuyaharakisha ila kuyahamuna hilo hapana. Maana hata ukianza mchakato wa kuyahamna[kuyanegative] utajikuta unaendelea kufanya mbadiliko mapya kutokea kwenye hali iliyopo hivyo kiufupi utaendelea kuupeleka muda mbele tu.

Mh! aliyeelewa zaidi nilichokiandika anieleweshe na mimi mazee 🤦‍♂️😂😂😂😂🤣🤣
 
Back
Top Bottom