Je ulipenda kuwa nani ulipokuwa mdogo?

Papaa007

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2016
Posts
1,103
Reaction score
1,737
Wasalaam.... Naona makarani wanapiga chenga za kututembelea wakat tumewapikia na diko kabsa wasije kusingizia njaa, Binafsi kama mimi mzaliwa wa tanzania mwenyeji na mkazi wa R-chuga nlipenda niwe rubani wa ndege za kivita kwasababu ya mazoea ya kuangalia movie za kivita/kijeshi zaman.....lakin leo hii mambo imekuwa tofaut kabsa na nadharia yangu kwan niko field tofaut kabsa na nliyokusudia, anyway life linasonga.

Mwenzangu na mimi ww ulipendelea kitu gan?
 
Nilipenda kuwa international spy(007 sababu ya movies kama wewe), nilivyokuwa nkagundua Tz kuwa hamna hata hicko kitu... utoto raha πŸ˜…
 
Nilipenda kuwa international spy(007 sababu ya movies kama wewe), nilivyokuwa nkagundua Tz kuwa hamna hata hicko kitu... utoto raha [emoji28]
Mambo ya james bond
 
Nilipenda kuwa dereva wa mabasi au malori kilichonifanya nipende mlio wa engine hasa mabasi Aina ya scania na fuso kile kimruzi na sauti inayotoka wakati inapanguliwa gia ili isimame
 
Nilipenda kuwa dereva wa mabasi au malori kilichonifanya nipende mlio wa engine hasa mabasi Aina ya scania na fuso kile kimruzi na sauti inayotoka wakati inapanguliwa gia ili isimame
Je kwa sasa ushakuwa davoo mkuu?
 
Nilipenda kuwa mfanya biashara kama Elon Musk[emoji56]
 
Nilipenda kuja kuwa mjeda wakati nimemaliza kidato cha nne miaka hiyo nasubiria matokeo nipo mtaani, jirani yetu alikuwa mwanajeshi na siku hyo wenzake walikuja na wakanitaka kabsa niende kwa kigezo urefu na umbo ila cha ajabu nilikataa na mpaka sas nina ishu nyngne kabsa maisha yanaenda.
 
Wakati nipo mdogo nilipenda Sana kuja kuwa mwanajeshi Yaani nilikua napenda hatari nahisi movie ndio zilinifanya nipende jeshi, Basi nikawa najifaninisha na arnold Schwarzenegger. Badae nilipofika darass la sita nkachange gia angani nikawa nataka nije kuwa daktari, hapa sasa nikawa namzuka wa udaktari Hatari Ila nilipofika secondari mambo yakaanza kubadilika taratibu. Nakumbuka sikumoja Teacher wa bios akasema kama mtu unapenda uje kuwa daktari Basi hujachelewa msingi ndio unaanzia hapa akasema nilazima ufanye vizuri masomo ya sayansi. Nikasema Hamna shida mbona ntakomaa tu, nilianza vizuri tu wakati nipo form one hapo ila nilipo fika form two Mwishoni mambo yakaanza kubadilika nikaanza kuona mahesabu Mara eti H+O=H2O Sasa hapo ndio wakawa wananipoteza unauliza hii mbili imetoka wapi unaambiwa wewe elewa tu kua Hydrogen akiungana na Oxygen unapata water. Unakutana na vifupisho eti uvikariri vyote Na for "sodium", H " for Hydrogen" achana na Ile ya sijui Halo Elena beberu amechinjwa na mgogo wa Canada sijui wa Serengeti, Sasa hapo ndio nikaanza kuona Moto unaanza kuwaka Physics ndio ikaja kunitoa kwenye reli kabisaa yani hasa kwenye prac ya mirror na pendulum bolb nikaona hapa SITOBOI, labda biology na yenyewe topic ambayo siisahau na nilikua naipenda Ni reproduction hasahasa in Mamalia pale, Yaani nilikua naipenda saanaaaa, Mathew ndo eeehh mama weee 🀦🀦 cycle, na maLog yalinishinda nikahama science kabisa. Ila siku ambayo sitaisahau Ni ile siku niliyo mtania mwalimu wa civics nikamwambia mwalimu SoMo lako tuna soma Basi tu kwani SoMo lenyewe halina hata Combi yoyote ile, nikikumbuka kilichonipata siku Ile daah πŸ™†πŸΎβ€β™‚οΈπŸ™†πŸΎβ€β™‚οΈ wakati Teacher mwenyewe ndio alianza kunitania. Teacher Sam nakukumbuka bado
 
Inaonekana wewe haukuipenda kutokea rohoni
 
Aisee mkuu sasa ukaishia wap udakar au usoja? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…