Wakati nipo mdogo nilipenda Sana kuja kuwa mwanajeshi Yaani nilikua napenda hatari nahisi movie ndio zilinifanya nipende jeshi, Basi nikawa najifaninisha na arnold Schwarzenegger. Badae nilipofika darass la sita nkachange gia angani nikawa nataka nije kuwa daktari, hapa sasa nikawa namzuka wa udaktari Hatari Ila nilipofika secondari mambo yakaanza kubadilika taratibu. Nakumbuka sikumoja Teacher wa bios akasema kama mtu unapenda uje kuwa daktari Basi hujachelewa msingi ndio unaanzia hapa akasema nilazima ufanye vizuri masomo ya sayansi. Nikasema Hamna shida mbona ntakomaa tu, nilianza vizuri tu wakati nipo form one hapo ila nilipo fika form two Mwishoni mambo yakaanza kubadilika nikaanza kuona mahesabu Mara eti H+O=H2O Sasa hapo ndio wakawa wananipoteza unauliza hii mbili imetoka wapi unaambiwa wewe elewa tu kua Hydrogen akiungana na Oxygen unapata water. Unakutana na vifupisho eti uvikariri vyote Na for "sodium", H " for Hydrogen" achana na Ile ya sijui Halo Elena beberu amechinjwa na mgogo wa Canada sijui wa Serengeti, Sasa hapo ndio nikaanza kuona Moto unaanza kuwaka Physics ndio ikaja kunitoa kwenye reli kabisaa yani hasa kwenye prac ya mirror na pendulum bolb nikaona hapa SITOBOI, labda biology na yenyewe topic ambayo siisahau na nilikua naipenda Ni reproduction hasahasa in Mamalia pale, Yaani nilikua naipenda saanaaaa, Mathew ndo eeehh mama weee [emoji1751][emoji1751] cycle, na maLog yalinishinda nikahama science kabisa. Ila siku ambayo sitaisahau Ni ile siku niliyo mtania mwalimu wa civics nikamwambia mwalimu SoMo lako tuna soma Basi tu kwani SoMo lenyewe halina hata Combi yoyote ile, nikikumbuka kilichonipata siku Ile daah [emoji2305][emoji2305] wakati Teacher mwenyewe ndio alianza kunitania. Teacher Sam nakukumbuka bado