Je, ulisajili kampuni na hujafungua e-filing ya TRA?

Je, ulisajili kampuni na hujafungua e-filing ya TRA?

Bexb

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2016
Posts
715
Reaction score
1,619
Habari ya jioni wakuu.

Kuna baadhi ya watu walifungua/kusajili kampuni lakini wakawa kama wameitelekeza iwe ni kwa kufanyia kazi kwa muda mfupi na kuiacha ama kutoifanyia kazi kabisa baada ya kuisajili.

Mjue kuwa taarifa zenu zipo TRA tena nyie mliofungua kampuni kuanzia mwaka 2018 ndio hadi TIN zenu zinasoma madeni na fines tu huko.

Hakikisha kama ulifanya huo usajili wa kampuni na hukufungua ama kujisajili katika mfumo wa TRA unafanya hivyo haraka dana kabla deni halijazidi kuwa kibwa zaidi.

Kama utakia na swali uliza hapa hapa
 
Hii kitu imenifanya ninadaiwa hela ya Kiwanja na TRA bila kupenda.
 
Pia wale waliofungua kampuni BRELA na huwa hawalipii ada za mwaka ama annual returns za BRELA na nyie mkumbuke kufanya hivyo.
Kwa upande wa BRELA ritani hufanyika kila mwaka kwa ile tarehe ya kuanzishwa kwa kampuni yaani birthdate ya kampuni. Hii itakuepushia kulimbikiza deni na fine pia kutokana na kutolipa kwa wakati
 
Hii kitu imenifanya ninadaiwa hela ya Kiwanja na TRA bila kupenda.
Kweli kabisa mkuu, wengi huwa hawajui hili suala na mamlaka husika huwa hawawakumbushi wahusika ama wateja wao juu ya huu wajibu.
Imewaumiza wengi sana. Mimi nimeleta thread hii kwa sababu huwa nina kawaida ya kuwatumia emails wateja wangu kiwakumbusha huu wajibu kumbe mmoja wao alikua akipuuza, kimeumana huoo ndio ananipigia.
 
Hii ngoma hatari, mimi yalinikuta nikaenda kufile siku ya mwisho na mtandao wao kama unavyoujua ukanigomea yani nililipa 450,000/ machozi yananitoka
 
Hii ngoma hatari, mimi yalinikuta nikaenda kufile siku ya mwisho na mtandao wao kama unavyoujua ukanigomea yani nililipa 450,000/ machozi yananitoka
Hii inaumiza sana na wengi hawajui. Juzikati hapo kunamteja alinifuata na case kama hii, yeye alikuta deni ni 10+M alifungua kampuni mwaka 2017 huko na hakuwahi kufanya lolote, sasa mwaka huu anataka kuishughulikia ndio anakutana na madeni
 
Back
Top Bottom