Je, ulishawahi kukutana na kitu cha kutisha usiku? Pita hapa tupeane uzoefu

1997 Vi-form 1 wenzangu wananitambia kuiona movie ya PREDATOR (Anorld ya jini) kwenye kibanda umiza,nikailaani sana mifugo (mbuzi)waliosababisha niwe malishoni wakati wenzangu wako wanafaidi mikwara ya akina BILLY DUKE...ikapita kama wiki hivi hiyo muvi ikawa inaoneshwa tena ila bahati mbaya inawekwa usiku kuanzia saa 4 mara tu baada ya trela la Alain Kounkou....
Home- ruhusa kama hiyo sahau kupewa (kutembea usiku?!)....nikajiapiza kutoikosa siku ya leo hata iweje,....Ili nifanikiwe lengo mzee nikalihujumu dirisha la chumbani kwangu kwa kung'oa nondo moja ili nipate pa kutokea pale familia nzima ikiwa imelala...
Saa 3 tayari raia wote wanakoroma,starling nikalinyatia dirisha nikajikuta niko nje,...ndani ya dk 5 nikawa nimejumuika na watu wazima holini tunamalizia album ya R.A.S (Alain) ili muvi lianze...muvi likaanza, muvi likaisha,nikaridhika...
Kutoka nje giza totoro....njia ya kwenda home mwendaji ni mimi tu,sina kampan coz tulikuwa tunakaa kwenye kota za shule alafu zimejengwa mbali na kijiji (Kunaitwanga Mahuta-Mtwara)...
Kijiji usiku huu kiko kimyaa,nyayo zangu tu ndo zinatoa sauti...kuna kipande cha msitu kinachotenganisha eneo la shule na hiki kijiji (hilo ndo eneo pekee nililolihofia kabla hata sijalifikia)....sasa wakati nazimalizia hizi nyumba za mwisho-mwisho ili niukabili huu msitu,mita kama 7 hivi kulia kwangu,kati ya nyumba moja na nyingine (zote zimeezekwa kwa nyasi) nikaona kundi la watu wako uchi,wako wima, wametengeneza kamduara hivi,wako kimya...BWANA BWANA wee...
Kuna kitu kama shoti ya umeme hivi iliyonifanya mwili,nywele visisimke kwa pamoja na nikauona mwili kama hauko na mimi vile...huku nikiwa nimesimama,moyo unataka utoke nje kwa mapigo ya KUDU-KUDU,nikiwa sijui la kufanya maana lile kundi nahisi lilikuwa bado halijaniona 'mwana mzurura usiku'... (vyote hivyo ni ndani ya kama sekunde 5 hivi)...
Mara kwa pamoja (utadhani waliambiana) kundi lote lile wakageuza vichwa vyao na kunitazama fwaaa......
Nakumbuka nikasema "Mawee" bila kutoa sauti (nikijua saasaa nyama ya mtoroka kwao inaenda liwa punde) na kufuatia na mbio za kukimbilia vidole/kama sio kucha pasipo kugeuka nyuma...nyumbani nikapitiliza,mbwa wa home akaanza kubweka na yeye akaniungia tela kimyakimya akijua tunacheza,nikajua hapa naenda chaka,nikageuza...mbio hadi dirishani...sikujali nani atasikia ninavyoingia au lah,...narukia dirishani,mbwa naye anavuta suruali kwa chini(huyu dog alikua best angu sana)baada ya zile kukuru-kakara za kuingia ndani...nikajikuta niko kitandani nahema kwelikweli, tena kwa nguvu,koo limekauka, huku mguu mmoja unaning'inia dirishani suruali inaendelea kuvutwa na mbwa nje......
Oya ngaillo malizia hii

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Mwaka 1998 nilikuwa Mpanda mjini maeneo ya City nasubiri barmed afunge nitoke nae, makazi Kawajense,baada ya kusubiri kwa muda majira ya 5 demu akaniambia nisubiri kidogo.
Ili kupata uhakika nikamwambia anipe kitu chake nikaenacho, akanipa jacket lake.
Nikakaa mpaka saa 6 nasubiri kwa nje, nilipoingia ndani nikamuulizia nikaambiwa ametoka kama dk20 hivi nikazunguka kila kona sikukuona.

Nikaona hii noma nikaondoka zangu na jacket lake,kufika maeneo ya soko kuu nikaona polisi kwa mbali,nikaona hapa nimeisha nikala kona kumbe walikuwa wameniona.

Wakaanza kunifuata nikapiga kona za kutosha nikajikuta niko maeneo ya tajiri mmoja alikuwa anaitwa Tarimo, nikakutana na kundi la mbwa ikawa nafukuzwa na mbwa napolisi kwa pamoja, polisi walivyoona mbwa wakarudi nikapita barabara inayoelekea hosptali ya wilaya.
Nilichoka kupita maelezo, nafika shule ya Msakila nakutana na watu wako doria wakaniambia nisimame nikaona sasa hapa kama kufa nife siyo kwenda polisi nikaanza mbio tena,nilipofika nyumbani nilivyoingia ndani sikuamini,nikakoma kutembea usiku.
Na sintasahau kabisa ile siku, kwanza barmed alivyo niachia jacket lake na nilivyokoswa koswa kunyea debe kwa ajili yake.
.
Mkuu Kama hilo koti unalo naomba uniuzie nimpe Shemeji yako

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
1997 Vi-form 1 wenzangu wananitambia kuiona movie ya PREDATOR (Anorld ya jini) kwenye kibanda umiza,nikailaani sana mifugo (mbuzi)waliosababisha niwe malishoni wakati wenzangu wako wanafaidi mikwara ya akina BILLY DUKE...ikapita kama wiki hivi hiyo muvi ikawa inaoneshwa tena ila bahati mbaya inawekwa usiku kuanzia saa 4 mara tu baada ya trela la Alain Kounkou....
Home- ruhusa kama hiyo sahau kupewa (kutembea usiku?!)....nikajiapiza kutoikosa siku ya leo hata iweje,....Ili nifanikiwe lengo mzee nikalihujumu dirisha la chumbani kwangu kwa kung'oa nondo moja ili nipate pa kutokea pale familia nzima ikiwa imelala...
Saa 3 tayari raia wote wanakoroma,starling nikalinyatia dirisha nikajikuta niko nje,...ndani ya dk 5 nikawa nimejumuika na watu wazima holini tunamalizia album ya R.A.S (Alain) ili muvi lianze...muvi likaanza, muvi likaisha,nikaridhika...
Kutoka nje giza totoro....njia ya kwenda home mwendaji ni mimi tu,sina kampan coz tulikuwa tunakaa kwenye kota za shule alafu zimejengwa mbali na kijiji (Kunaitwanga Mahuta-Mtwara)...
Kijiji usiku huu kiko kimyaa,nyayo zangu tu ndo zinatoa sauti...kuna kipande cha msitu kinachotenganisha eneo la shule na hiki kijiji (hilo ndo eneo pekee nililolihofia kabla hata sijalifikia)....sasa wakati nazimalizia hizi nyumba za mwisho-mwisho ili niukabili huu msitu,mita kama 7 hivi kulia kwangu,kati ya nyumba moja na nyingine (zote zimeezekwa kwa nyasi) nikaona kundi la watu wako uchi,wako wima, wametengeneza kamduara hivi,wako kimya...BWANA BWANA wee...
Kuna kitu kama shoti ya umeme hivi iliyonifanya mwili,nywele visisimke kwa pamoja na nikauona mwili kama hauko na mimi vile...huku nikiwa nimesimama,moyo unataka utoke nje kwa mapigo ya KUDU-KUDU,nikiwa sijui la kufanya maana lile kundi nahisi lilikuwa bado halijaniona 'mwana mzurura usiku'... (vyote hivyo ni ndani ya kama sekunde 5 hivi)...
Mara kwa pamoja (utadhani waliambiana) kundi lote lile wakageuza vichwa vyao na kunitazama fwaaa......
Nakumbuka nikasema "Mawee" bila kutoa sauti (nikijua saasaa nyama ya mtoroka kwao inaenda liwa punde) na kufuatia na mbio za kukimbilia vidole/kama sio kucha pasipo kugeuka nyuma...nyumbani nikapitiliza,mbwa wa home akaanza kubweka na yeye akaniungia tela kimyakimya akijua tunacheza,nikajua hapa naenda chaka,nikageuza...mbio hadi dirishani...sikujali nani atasikia ninavyoingia au lah,...narukia dirishani,mbwa naye anavuta suruali kwa chini(huyu dog alikua best angu sana)baada ya zile kukuru-kakara za kuingia ndani...nikajikuta niko kitandani nahema kwelikweli, tena kwa nguvu,koo limekauka, huku mguu mmoja unaning'inia dirishani suruali inaendelea kuvutwa na mbwa nje......
Dah we jamaa ni shidaaa kwenye kusimulia...maana ulichonifanya
Nimeshacheka hapa mpaka basi...eti wakaniangalia fwaaa[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Ebu nisaidie hapa kujua...
Hili kundi la watu waliokuwa uchi lilikuwa mbele yako uelekeo wa nyumbani how come ukaelekea walipo badala ya kurudi ulipotoka

All in all umenichekesha sanaaaa

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Miaka ya 2006 nikiwa secondary school boarding tulitoroka maeneo ya shule na kwenda kwenye shamba la machungwa ya shule tukiwa na viroba tuliiba machungwa kwa kuvuna Hatari tukijaza kwenye viroba tukiwa Kama mtu sita Hivi sasa baada ya kuvuna Kama dakika kumi Hivi tunaona kikundi cha watu wananyatia nao kwenye shamba lahaula tulitimua mbio za Hatari kwenye makorongo kuna jamaa yangu mmoja aliyaangusha machungwa yote korongoni sisi mbio mpaka bwenini kumbe baadae kuja kushtuka wale pia walikuwa wezi wenzetu wa machungwa ingawa walikuja kivyaovyao kesho yake asubuhi ulikuwa bonge moja la msala kwa headmaster kuhusu Yale machungwa yaliyotapakaa korongoni ilipita inspection ya Hatari. ingawa machungwa mengine tuliyaficha kwenye Dari na kingine cha ajabu asubuhi pale walikuta bonge la chatu maeneo ya shamba la machungwa wakaliua Daaah ilikuwa Kama Mungu tu Usiku ule hizi njaa nyingine.... I miss those days at school...

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Hatari hizi siyo mada za kusoma usiku .[emoji32][emoji32][emoji32][emoji32][emoji32]
 
Niliota ccm imechagua kiongozi mwenye sifa kama za Mugabe. Sitasahau siku hio

cephalocaudo the greatest
 
Dah we jamaa ni shidaaa kwenye kusimulia...maana ulichonifanya
Nimeshacheka hapa mpaka basi...eti wakaniangalia fwaaa[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Ebu nisaidie hapa kujua...
Hili kundi la watu waliokuwa uchi lilikuwa mbele yako uelekeo wa nyumbani how come ukaelekea walipo badala ya kurudi ulipotoka

All in all umenichekesha sanaaaa

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
Tuchukulie upo
barabarani,upande wa
kulia na kushoto kuna
nyumba zilizojipanga
kwa uelekeo wa
barabara...sasa mimi
bedui ndo nanyooka
kuifata bara iendako,si
ndo nikaangalia
upande wa kulia sasa!!
(note:hizi nyumba
zimejengwa karibu
kabisa na hiki kinjia)
laiti ingekuwa
barabara kuu,alama ya
X ingewahusu!
U got me nawoo?
 
1997 Vi-form 1 wenzangu wananitambia kuiona movie ya PREDATOR (Anorld ya jini) kwenye kibanda umiza,nikailaani sana mifugo (mbuzi)waliosababisha niwe malishoni wakati wenzangu wako wanafaidi mikwara ya akina BILLY DUKE...ikapita kama wiki hivi hiyo muvi ikawa inaoneshwa tena ila bahati mbaya inawekwa usiku kuanzia saa 4 mara tu baada ya trela la Alain Kounkou....
Home- ruhusa kama hiyo sahau kupewa (kutembea usiku?!)....nikajiapiza kutoikosa siku ya leo hata iweje,....Ili nifanikiwe lengo mzee nikalihujumu dirisha la chumbani kwangu kwa kung'oa nondo moja ili nipate pa kutokea pale familia nzima ikiwa imelala...
Saa 3 tayari raia wote wanakoroma,starling nikalinyatia dirisha nikajikuta niko nje,...ndani ya dk 5 nikawa nimejumuika na watu wazima holini tunamalizia album ya R.A.S (Alain) ili muvi lianze...muvi likaanza, muvi likaisha,nikaridhika...
Kutoka nje giza totoro....njia ya kwenda home mwendaji ni mimi tu,sina kampan coz tulikuwa tunakaa kwenye kota za shule alafu zimejengwa mbali na kijiji (Kunaitwanga Mahuta-Mtwara)...
Kijiji usiku huu kiko kimyaa,nyayo zangu tu ndo zinatoa sauti...kuna kipande cha msitu kinachotenganisha eneo la shule na hiki kijiji (hilo ndo eneo pekee nililolihofia kabla hata sijalifikia)....sasa wakati nazimalizia hizi nyumba za mwisho-mwisho ili niukabili huu msitu,mita kama 7 hivi kulia kwangu,kati ya nyumba moja na nyingine (zote zimeezekwa kwa nyasi) nikaona kundi la watu wako uchi,wako wima, wametengeneza kamduara hivi,wako kimya...BWANA BWANA wee...
Kuna kitu kama shoti ya umeme hivi iliyonifanya mwili,nywele visisimke kwa pamoja na nikauona mwili kama hauko na mimi vile...huku nikiwa nimesimama,moyo unataka utoke nje kwa mapigo ya KUDU-KUDU,nikiwa sijui la kufanya maana lile kundi nahisi lilikuwa bado halijaniona 'mwana mzurura usiku'... (vyote hivyo ni ndani ya kama sekunde 5 hivi)...
Mara kwa pamoja (utadhani waliambiana) kundi lote lile wakageuza vichwa vyao na kunitazama fwaaa......
Nakumbuka nikasema "Mawee" bila kutoa sauti (nikijua saasaa nyama ya mtoroka kwao inaenda liwa punde) na kufuatia na mbio za kukimbilia vidole/kama sio kucha pasipo kugeuka nyuma...nyumbani nikapitiliza,mbwa wa home akaanza kubweka na yeye akaniungia tela kimyakimya akijua tunacheza,nikajua hapa naenda chaka,nikageuza...mbio hadi dirishani...sikujali nani atasikia ninavyoingia au lah,...narukia dirishani,mbwa naye anavuta suruali kwa chini(huyu dog alikua best angu sana)baada ya zile kukuru-kakara za kuingia ndani...nikajikuta niko kitandani nahema kwelikweli, tena kwa nguvu,koo limekauka, huku mguu mmoja unaning'inia dirishani suruali inaendelea kuvutwa na mbwa nje......
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] huyo mbwa bado yupo?
 
Mie bhana nliendaga kwa ndugu zangu uko kijijini sasa tulikua ndugu wengi kidogo, hapakua na option zaidi ya wao ndugu zangu kunipa chumba cha ajabu kidogo, yaan nje ya nyumba yao kulikua na chumba ambacho kilikua hakitumiwi na watu, kilijengwaga kwa ajili ya wafanyakazi wa ng'ombe nk. Sasa hao wafanyakazi walikua ni wakabila flani iv tata kidogo kwa maswala ya ushirikina, walivyoondoka na kurudi kwao watu wakawa wanalalamika kila wakilala icho chumba, sasa mie sikuwai kujua habari hizi na kwa siku ile hapakua na option yoyote zaidi ya mie kupewa icho chumba, sasa sijui ndugu zangu waliniona mie kijana wa mjini mauza uza yatakwama au vp, ila ni vile ndugu wengine walikua watu wazima.

Kimbembe kikaanza usiku wa siku hio, sasa nimelala nahisi mmmmhh humu mbona kama kuna watu wengine tena waziada,basi napuuza mawazo haya tu ila sense zinaniambia kabisa we are more than 3 humu, aargggh nkafungulia RFA sikujali, sasa kimbembe kikaja usiku sanaa nikaanza kuskia watu wanatembea humo ndani, wengine wanapanda hdi juu ya kitanda nlicholala yaan nimelala naskia kabisa kuna mtu imesimama hapa kitandani, asee nliatuka vibaya sanaa, moyo unadunda, presha juu najiuliza naota au live, kumbe live, mara nikaskia mtu anavuta shuka, asee nliongea kwa nguvu "k**mamaaaaaeeeee" nani uyo, nkaskia sauti ya kicheko, nkajiuliza ndan au nje, asee nlisali sala zote, hali ikatulia kidogo, nikalala ila usingizi hauji, yaani nimetetemeka mpaka nimechoka, nimesali sanaa, sasa ukaja kama usingizi iv nikaanza kuota mambo ya ajabu et mule kuna watu watatu wananihoji wew umetoka wap, mbona mkorofi? Nani kakutuma uje chumbani kwetu khaaa nkastuka sasa nimestuka ila ile ndoto naiona kabisa inaendelea nikiwa macho, asee usiku ule ulikua vita vikali sanaa, nikawa macho tu nimefungulia radio kwa saut kubwa tu ila natetemeka haswa,,, kilichofuata kesho yake nikawaeleza ndugu zangu yote ndo wakanipa huu mkanda wa icho chumba na wengine hawakuamin kwamba nimewezaje kulala humo? Nikawamind kimoyo moyo wale ndugu kesho yake mchana tena uyoo nkarudi kwetu mjini,na nikasema niko radhi niue mchawi ila sio mwizi.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] bila Shaka walikuwa wafanyakazi kutoka kigoma
 
Huko kigoma ni balaa, siku moja tulikuwa huko ikafika mida ya usiku tukatoka kuingia mitaani kuwasaka ma chick. tukiwa ktkt ya road tukamwona demu mmoja mfupi kwa mbali tukampigia mluzi gafla akaingia kwenye kona kuangalia nyuma demu si huyu hapa acha ma raia wajikojolee dah....

Siku nyingine tukiwa shinyanga mida ya saa moja usiku tukakimbizwa na mfuko empty wa sementi du balaa.... Kuna maeneo yanatisha

Siku moja tukiwa moshi town usiku kama saa 3 tunarudi hotelin tukapitia njia flani tukakutana na bonge la nyumba lina uzio halijakamilika tukachungulia ndani kuna nini kulikuwa na mipaka imefika kama ndama ikaruka ukuta ikasepa na sis kujihami tukaingia ndani kwa mtu wote sijui yalikuwa majini ...
[emoji23]mfuko wa cement polen aisee
 
Tena wakijua kuwa huna madhara kwao wala hawaangaiki na wewe.
Anko wangu aliwah kunihadithia kwamba wakat anasoma huko Tunduru kuna siku waliwasindikiza wenzao stendi wakapande mabasi ya alfajir (miaka hiyo safar huanza saa 10 alfajiri)Basi baada ya kuhakikisha wenzao wamepanda basi wao wakaona haina haja ya kubaki pale wakaona warud shule.Ni mwendo kidogo na ni porini.Walipokuwa katikati ya safar Porini wakakutana na msafara.
Msafara ulikuwa unaongozwa na vikongwe wawili (Babu mbele na bibi nyuma)katikati wapo watu kama kumi wamebebeshwa mizigo ya kuni.
Anko alipowaona wale jamaa na mwenzie wao wakawapisha wale watu (Babu na bibi walijifunga nguo nyeus like kaniki)hawakusemeshana,so hawa wazee wa feva za usiku kama hawana na shida na wewe wanakuacha ila wale vibwengo watakua wanakuchezeachezea tu kwa bitimbwi

May Allah bless Me and You
 
Tuchukulie upo
barabarani,upande wa
kulia na kushoto kuna
nyumba zilizojipanga
kwa uelekeo wa
barabara...sasa mimi
bedui ndo nanyooka
kuifata bara iendako,si
ndo nikaangalia
upande wa kulia sasa!!
(note:hizi nyumba
zimejengwa karibu
kabisa na hiki kinjia)
laiti ingekuwa
barabara kuu,alama ya
X ingewahusu!
U got me nawoo?
Nimeelewa mwl...
Naona nilicheka sana mpaka nikawa sikuiona hii maana umeielezea hata kwenye story maana imebidi niirudie (wakanitizama fwaa)
Mi nilidhani walikuwa katikati ya barabara

Nazan kwa huu mwaka huu uzi wa tatu kunichechekesha sana...

Back
Top Bottom