Je ulitokaje kwenye kifungo cha kichawi/kishirikina?

Je ulitokaje kwenye kifungo cha kichawi/kishirikina?

ngongoti2000

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2017
Posts
2,236
Reaction score
2,142
Wadau
Moja kwa moja kwenye mada.
Ni ukweli kwamba uchawi upo hata kwenye Biblia imeandikwa. Familia yangu iko kwenye kifungo kibaya cha kichawi na tumemjua huyo aliyetufanyia hivyo baada ya miaka mingi. Evidences ni nyingi toka kwenye vyanzo mbalimbali tofauti , ambavyo vingine havina uhusiano na ndugu yeyote lakini vimemfichua ndugu nyetu huyo huyo... HII HAINA UBISHI WOWOTE .Hii ni baada ya kuhangaika kwa watumishi ,manabii , waganga mbalimbali ambao hawajawahi kuniambia ninakwama wapi...lakini hatimaye nimepata mwanga...Sasa nahitaji msaada jinsi ya kutoka/kujikwamua kwenye kifungo hiki maana najua humu lazima kuna watu waliopitia masahibu kama haya .Jambo hili huwezi kulielewa mpaka likukute.Naomba msaada wenu wakuu
 
Hupo

Unahitaji kuombewa na Shehk au nikuunganishe na mtaalam ??
 
Huwezi toka Ndugu yangu! Nakuhakikishia,Kama Hujaarhirika moja kwa moja Achana nao tu( Ishi nao tu).
.Wachawi hawajawahi kishindwa vita sababu kuu wana Ushirikiano kuliko Waganga na kama Mara nyingi wanasumbua watu wenye mafanikio ili wawafilisi( Roho mbaya).
.Mwisho nikwambie Hakuna mganga Ambae sio Mchawi,Utanikumbuka Ukishafilisika!!
 
Nifilisike mara ngapi mkuu?....hapa nilipo nipo hoi kabisa....siwezi endelea kuishi nao
 
mchaw utumia mazngira yanayokuzunguka kukuloga na kukuarbia future yako kama n mnywaj wa pombe lazma atatumia bar au vlabu vya karbu kukulogea mpka wakuokote mtaron vivyo hivyo kielim hata kiuchumi njia moja yapo ya kwanza ya kumwekwepa mchaw n kukaa nae mbal mana mchaw n mtu mwenye wivu sana utampa elfu 10 hiyo hiyo ataitumia kwenda kukuangamiza nayo kiuchumi kwa kuifanyia makafara yao kwa kile wanachoita unajifanya una hela sana ngoja tukuonyeshe kama unaweza ukaondoka mazngira hayo potea kabisa hata kwa miaka 5 kaanze maisha yako mapya usfanye show off ya mitandaon wala nn hakiksha hawajui lolote kuhus ww zaid ya kujua flan n mzima tu usishirik sherehe wala misba isio ya lazma kijijin kwenu kwan hapo ndio ua lango kuu la kukukandamizia Nna meng ya kukuelezea kwasababu mm pia n mhanga wa hilo na nmelmudu kwa garama kubwa sana japo bado sijion katika ile hali yangu ya kwanza lakn n bora sasa kulko apo katikati nlvyokua sema mm sio mwandsh mzur nngekupa hints kbao za kukuvusha

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kaombewe kanisani...kwa jina la YESU KRISTO aliye hai utapona...

Ila uwe na Imani...

Kama huna Imani na YESU unaweza ukawa umeenda kutembea...

Nakumbuka nililogwa nikawa naumwa na kitu hicho ktk kifua...

Kunawakati vitu vilikuwa vinatembea tumboni vinakuja shingoni...

Nipona kwa kuombewa NGOMENI kwa Kuhani Musa...nilipona kwa jina la YESU.

Sikulazimishi ila nenda au sikiliza ibada za Kuhani Musa
 
Ukiwa ndani ya Kristo Yesu unakuwa kiumbe kipya. Ya kale yanapita tazama yanakuwa mapya.
Sibishani na wewe. Ila kuna muda uelewa na shida huwa vinagombani. Inahitaji level kubwa ya imani mpaka aelewe hili neno.

Kuna namna unaweza kaenda kuombewa akajikuta Ana maratizo zaidi, ushauri ujitolee kumwombea na kumuelewesha juu ya ukiwa ndani ya Kristo Yesu umekuwa kiumbe kipya
 
Atafute kanisa ambalo limejikita kumfundisha mtu neno la Mungu ili akue kiroho. Kuombewa ni suala la emergency lakini ushindi wa kudumu ni suala la kukua kiroho.
 
1. Kwa imani yako wewe( kwa mimi ni mkristo namwamini Yesu Kristo) anza kumtafuta kweli kweli. Soma neno la Mungu na uliweke kwenye matendo haswa, naamanisha haswa ukimtafuta Mungu kweli kweli anaonekana ila upambane
2. Kuna masomo huwa anatoaga hapa ndugu @mshanajr haswa somo la chumvi litafute lisome na ulifanyie kazi utafanikiwa kwa asilimia kubwa.
3. Embu mtafute @mshanajr na kina.mdada mmoja anajua sana mambo ya dini sijui heaven sent au yule bibi wa kiislamu watakushauri vyema
 
Back
Top Bottom