Je ulitokaje kwenye kifungo cha kichawi/kishirikina?

Huyu nimemsikia sana sifa zake....nitafuatilia
 
Mshana Jr naomba msaa`da wako wa ushauri
 
Nipo katika same situation naww,nimelogwa mm mpaka familia yangu yaani wazazi. Nimefungwa nisipate kazi, nisipate mtoto(nishawapa ujauzito wanawake wawili mimba 4 zimetoka),biashara 2 za familia zimekufa kimazingaombwe sana. Tumehangaika sana kujitoa kifungoni ila wapi. Nimetumia sana chumvi ya mawe,ombewa sana ila hakuna mabadiko,kilichobakia sasa ni kumjua mchawi wetu na kwenda kumkata tu mapanga.
 
Mtafute Yesu kwa bidii zote utakuwa salama mkuu,kuombewa unaweza kuombewa sana tu lakini kama hujasimama vizuri kiroho huwezi kuchomoka...
 
WACHAWI NYOKOW
 
MKUU HII HALI INAKERA SANA
 
Mungu akuongoze kwa kweli.
Nikisema sijui ushirikina kuwa upo itakuwa ni swaga Tu mkuu, ushirikina upo na unafanya kazi
 
Mchawi ni dhaifu dhaifu dhaifu na mwoga kuliko makundi yote ya waovu Duniani. Si lolote si chochote. Anategemea weakness na woga wako tuu ili kufanikisha mission zake. Nasema Mchawi ni mpuuzi wa mwisho asiye na power yeyote.. Zaidi tuu ni kuwaendekeza. Ni kama tuu nyoka asiye na sumu au meno alivyo na mabaka mabaka na mbwembwe za kumtishia adui kwa lengo la kujihami tuu laki is ukimsogelea zaidi anakimbia. Ushirikina ni upuuzi fulani tuu unaoendekezwa na jamii za waoga.
 
Hapa unazungumzia ulokole...ambao asilimia kubwa ni unafiki..na mimi sitaki kumkwaza Mungu kwa huo unafiki
Kwahiyo ukitafuta uchawi ndio utampendeza Mungu? Hapa nahisi unasumbuliwa pia na fikra zako mwenyewe zinakupoteza,.. Kama hautabadili attitude yako ni ngumu sana kufanikiwa kutoka kwenye hicho kifungo..
 
Vingi tu wanashindwa, wangekuwa wanaweza KILA kitu wangefanya uharibifu mkubwa Sana
 
Ulimwengu wa roho ni mpana sana, yaani Mungu atusaidie maana lengo la wachawi na waganga lengo lao ni kuharibu future ya kizazi hata Ukoo wote. Fanya maombi bila kuchoka, pia uache dhambi za kisiri Siri, zile ambazo unafikiri hakuna mtu anaekuona mfano wivu,kibri,tamaa, hasira,kusengenya nk.....
 
Kumvisha tairi ndiyo nzuri,piga moto
 
Nasikia Kuhani Musa wa pale Temboni anaweza kukuondolea hayo mabalaa na kisha akayaboresha akayarudisha kwa aliyekuloga yakiwa na nguvu mara dufu.

Ni wewe tu unaamua adui afe ama ateseke tu.
Mpo wengi mnaompigia debe!
 
Dawa yake na wewe anza kufanya ushirikina wa kujilinda. Mnuwie maneno tumia mawe ya chumvi. Mchape bakora kwa maneno. Maneno yana nguvu sana. Toa chuki yako kwake ingia nae mapambano ya kiroho huku ukiwa na amani.
 
Wanatesa sana hawa washenzi . Kwa mtu ambaye hayajamkuta hawezi kuelewa tunaongelea nini. Tunashukuru sisi tumeshamjua mtesi wetu sasa tunajipanga kufanya kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…