Je, umbea ni kosa kisheria?

Je, umbea ni kosa kisheria?

Luigi Alfred

Member
Joined
Mar 17, 2016
Posts
66
Reaction score
45
Umbea umekuwa tatizo sugu miongoni mwa wanajamii waishio mitaani kiasi cha kusababisha ndoa za watu kuvunjika na mifarakano kuongezeka.

Kwa wana JF wenye uelewa kisheria hili ni kosa ambalo mtu anayesababisha haya anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwafarakanisha wanandoa?
 
Umbeya ni tatizo kubwa. Wengi wanasema mambo wasiyokuwa na uhakika nayo bila kujali athari itakayotokea
 
Inategemea na kilichotokea baada ya umbea kufanyika, kama matokeo ya umbea huo. Fikiria scenerio ambayo mtu kafanya umbea ukapeeleka watu kupigana na kuumizana au kuuana!
 
Hapa mtaani kwetu jamaa amempiga mke wake nusura amtoe roho baada ya kupata taarifa za umbeya .Baadae imefahamika kuwa mke wake alisingiziwa na shoga yake sasa anataka akamwone mwanasheria ili kesi iende Mahakamani!
 
Umbeya siyo tu kwamba ni kosa kisheria, bali kosa la JINAI
Kwa hiyo waathirika wa umbeya wanaweza kuripoti matukio kama hayo polisi endapo tuna uhakika kuwa hili ni kosa la jinai. Hapa mtaani kwetu jamaa kampiga mke wake hadharani na kumdhalilisha wakati kisa kilikuwa cha kusingiziwa. Mme wake kamwomba samahani baada ya kubaini kuwa ilikuwa ni taarifa za ksingiziwa sasa huyu mama akienda polisi itakuwaje?
 
Back
Top Bottom