Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Kama kawa, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa. Leo niko Mbeya, hiki kibaridi cha Mbeya, kwa sisi tulio zoea mablangeti yale, hata ujifunike vipi, na blangeti zito kiasi gani, kibaridi bado kiko pale pale, kinapenya, unakisikia!, mpaka saa hizi uzingizi umegoma!, hivyo the best company na companion ni kushuka jf.

Huu mjadala wa IGA ya DPW na Bandari zetu, unatusaidia kwa mengi, sasa kuna watu wanaanza kuhoji serikali ya Tanganyika, wanataka serikali 3.
Hoja nyingine mjadala huu wa IGA ulizotusaidia ni hizi
Sasa Watanzania wanahoji muungano na kuitaka serikali ya Tanganyika!, at this point, naomba ku declares interest kuwa mimi ni pro Nyerere ambao tunaamuaminia Wazo kama hili nililileta humu kitambo, Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"

Huku kuhoji hoji muungano kunakoibuliwa sasa na baadhi ya watu, nako sasa kunageuka ni kero ya muungano!, kwa maoni yangu, dawa ya pekee na tiba ya kweli ya kiuhakika na ya kudumu kutibu kero zote za Muungano, ni kwenda kwenye serikali moja!. Swali ni Je Tanzania sasa umefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye serikali moja?

Mimi ni mtu wa mastori mastori, kama wewe ni mtu wa short and clear, ishia hapa na ku jump kule kwenye conclusion, wale wa mastori tuendelee
Mastori ya Pasco
Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana ili iweje!
Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.

Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa

Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.

Conclusion
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, hili pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa mmefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye serikali moja?

Wasalaam,
Paskali.

PIA SOMA
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?
 
Masikini.

NCHI zetu karibu zote Africa ziliwahi mno sana kupata uhuru wake Mapema.

NASIKITIKA KOSA kubwa waliloolifanya wakoloni ni kuziacha NCHI hizi zijitawale mapema.

AFRIKA TULIPASWA kupata uhuru kuanzia Mwaka 2000.

AFRIKA Kuna LAANA.
AFRIKA Kuna VIONGOZI WAPUMBAVU
AFRIKA KUNA MAJUHA.
AFRIKA KUNA MIUAJI.
MIFISADI.
MAJIZI

WAZUNGU hamkupaswa kutupa uhuru Mapema mngetusaidia kama south Africa
 
Vipi mkuu, kwema? Pole kwa baridi mkuu. Kwani haupo nyumbani?

Turudi kwenye hoja, hii bandiko lako ndo linazidi kuchanganya zaidi ya kuelewesha kuhusu mkanganyiko wa huu muungano wa kitapeli.

Unasema eti nchi ya Zanzibar ilikufa lakini bado ina serikali yake na katiba yake.

Unasema Tanganyika nayo kama Zanzibar imekufa, wakati siyo kweli kwamba Zanzibar imekufa kama ilivyokufa Tanganyika.

Sikuelewi unaposema “Nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili. Sasa mkuu, hizo sehemu mbili ambazo moja ina katiba yake na serikali yake, na nyingine haina, unaona ni muungano wa kuweka tu Serikali moja na itakuwa sawa?

Zanzibar ina serikali yake ambayo wewe unaiita “ya ndani”, na siyo nchi, hiyo nchi imetowekaje? Na wakati bado unasema hiyo “sehemu” imemezwa kama Tanganyika lakini kwa ndani muungano ina serikali yake. Sasa hiyo serikali siyo ya nchi ni kitu gani? Au kwasababu unaita eti “sehemu” moja ya muungano. Ni wapi kwenye katiba hiyo sehemu imemezwa kama Tanganyika ambayo kiukweli inatawiwa na Zanzibar kwa kupitia kivuli cha muungano?

Halafu eti muungano ni wa kimataifa tu. Mkuu Ebu tuanze na kitu kimoja kabla ya kuendelea sana na mjadala.

Maana Ikiwa mungano ni kwa kimataifa yani serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania peke yake, ndo inatambulika kimataifa peke yake na Zanzibar haitambuliki, ila kwa ndani peke yake ndo utambuwe kwamba muungano huu upo hivyo ulivyo kwasababu maalum. Na hizo sababu, ndizo zilizofanya kusiwepo na serikali moja. Sababu hizo zilizokuwepo, sidhani kama zimejiishia zenyewe tu.

Ebu tuwekee hapa mfumo wa hiyo serikali moja utakavyokuwa ili Zanzibar nayo ipotee kiukweli kama Tanganyika ilivyopotea. Na yenyewe imezwe na hiyo katiba ya serikali moja ya jamuhuri kama Tanganyika ilivyo mezwa.
 
Ok

Lakini ili kuridhia lazima zipigwe kura

Kwenye kupiga kura sasa ndio wapinzani na watu wengine wanapopoteza haki yao ya msingi

Unajua Pasca karatasi za kupiga kura zina vyumba vidogo sana mara nyingi wafuasi wa serikali tatu watakosea tu kwa kupitiliza na kelele zao zote huharibikia kwenye zoezi la kupiga kura ya kuridhia

Ni mara ngapi Pascal wafuasi wa vyama hivi pendwa wanakosea kupiga kura kwa kumfuta futa mgombea wa ccm kumbe ndio wanaharibu kura zao

Halafu Serikali moja itatoka wapi na ni nani atatangaza hayo matokeo

Tatizo ni nani anayeridhia hayo,Na ni nani atasimamia kuhesabu kura na ni nani atatangaza hiyo Serikali unayosema?

Halafu kwenye issue ya IGA ,Tatizo ni lugha tu
Nimeshangaa eti mkataba haujataja ukomo kwa tafsiri ya waswahili,Hivi usipoambiwa utaishi miaka mingapi ndio umeambiwa utaishi milele?

Kuna muda huwa naona ukiwa mbunge wa ccm ni wewe tu uamue kustaafu kugombea au jina lako likatwe kinguvu ,Lakini hii nchi ina wapumbavu na wajinga wengi sana wasioelewa uhalisia wa siasa za Afrika

Afrika wananchi wana njaa,Wewe ongea lakini mwisho wa siku wanahitaji ile kitu ya kubrashia viatu,Kama unayo ya kubrashia viatu wajumbe na wananchi hata serikali kumi wataunga mkono
 
Kwa sasa nadhani Serikali moja haiwezekani! Waasisi wa Taifa letu walichelewa au walikosea kutolishughulikia tangu mapema!
Mimi nadhani suruhisho ni Serikali tatu! Kila nchi iwe na serikali yake harafu iwepo Serikali ya Muungano!
 
Tatizo ni hawa matapeli "wanasiasa" kitu kikubwa wanachowaza ni jinsi gani muundo wa muungano utawanufaisha. Amini nakwambia kwa roho zao mbaya, zisizo jali utu, roho yakujali matumbo yao, jibu watakalo kuja nalo ni serikali tatu, ili bendera ziongezeke ving'ora viongezeke. Huku wakijua fika kama zile hela za kuhudumia serikali ya tatu zingesaidia kwenye elimu na afya ila kwakuwa afya mbovu na elimu mbovu ni mtaji wa wanasiasa wanafumba macho na kupita kama gari lililokatila breki. Kama kweli viongozi wanania ya dhati kuwaletea wananchi maendeleo pasipo kujali matumbo yao. Serikali moja ndiyo mwarubaini wa na sisi wananchi hatuna shida na hilo ndiyo maana ndugu zetu wa Pemba wapo kuanzia mtwara mpaka tanga,wapo kuanzia ruvuma mpaka mara,Dar wa salaam ndiyo ndiyo makao makuu na inapoanzia safari ya kuitafuta mikoa tabora kigoma na kanda ya ziwa yote. Na siwezi kusahau ndugu zake watanganyika wanaofanya shughuli za upagazi Zanzibar wako poa na hawana shida. Ila shida ipo kwa viongozi ambao kitu cha kwanza wanufaike vipi na muungano sio wananchi muungano uwanufaishe vipi
 
Naunga mkono hoja,ila Kwa kutunza utamaduni wa Wazanzibar kama wanavyotaka basi sheria ya restriction ya Ardhi nk iwepo kama kawaida maana hata Baada ya Ujerukani kuwa Moja Bado Kuna sheria za kuibeba East Germany
 
Pascal Mayalla serikali moja ndiyo suluhisho, hasa kiroho maana in years to come Zanzibar yote haitokuwepo kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi, maana yake itafunikwa na maji, kwa hiyo wananchi wa Zanzibar wakiwa watanganyika itabidi wahamie huku Tanganyika. Na chanzo chetu cha mafuta ambacho ayatollah na wengine waarabu wanakitegemea basi tutaanza kuchimba na kuitajirisha Tanzania yetu. Ila hivyo vyote ni nadharia kwa sababu mwarabu anataka Zanzibar iendelee kubaki kama Zanzibar ili isije tokea watanganyika wakaingia mkataba na Israel wakaanza kuchimba mafuta ayatola atakufa njaa, hivyo serikali moja haiwezekani kabisa tena hicho kitu mataifa ya kiarabu yata hakikisha nchi haitawaliki
 
Zanzibar sio nchi!.
Mimi naelewa Zanzibar ni moja ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muunano wa Tanzania.
dawa ya pekee na tiba ya kweli na ya kiuhakika ya kutibu kero zote za Muungano, ni kuwa na serikali moja!.
Hili haltotokea, hasa kwa msimamo ya Watanganyika kwamba Zanzibar lazima dhibitiwe. Tumejifunza kwamba kwa Watanganyika kwao muungano ni kwa ajili ya kuidhibiti Zanzibar na Wazanzibari kwa kisingizio cha siasa kali na Uarabu.

Nitashangaa sana kwa Mzanzibari, baada kujua msimamo wa Watanganika, kukubali muungano wa serikali moja. Nawakumbusha Wazazibari halahala ujiti na jicho ncha una hoho.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.
Inapotokea mkanganyiko au utata wa kisheria kati ya zile nchi mbili zilizoungana, huwa hatuangalii katiba kwasababu katiba ni zao la yale makubalano. Makubaliano yanatambua kuweko kwa Zanzibar, hivyo kusema katiba ndo ya mwisho kwa hili hauko sawa.

Zaidi hiyo katiba yenyewe tunaiita siyo, kwani haikufuata melekezo ya makubaliano. Nayaita mkubaliano kwa kuangalia msimamo wako, kama tunavyoambiwa eti "when you are Rome do as Romans do.

Naandika haya nikiwa kama munavyotuita 'lay' kwani kwenu msomi ni mwanasheria tu hata kama ana shahada ya kwanza, na wengine ni wajinga ( lay) hata kama ana shahada ya uzamivu au profesa. Mambo ya ajabu!!
 
Hapa nakuunga mkono; serikali moja ndio suluhisho ili kuondosha upande wa pili kudai hawaruhusu Mtanganyika kumiliki ardhi Zanzibar eti itapoteza utamaduni wake!!!!
Maamuzi yanayotolewa yanatakiwa yaathiri pande zote mbili sio wa upande wa pili kunufaika na jasho la upande mwingine.

Ni kosa mkoa kuwa na katiba na sheria zake zinazokinzana na katiba ya Jamhuri wa Muungano
 
Swala la JMT na serikali ya Zanzibar, hata majiarani wanatushangaa, wanashindwa tu kutuambia. Tanganyika iko wapi? Tangu enzi ya ukoloni ni Tanganyika. Nani kamuuwa mama Tanganyika? Haya sasa, kwa kuwa Gwajima ni mzee wa ufufuko, fufua Tanganyika, paza sauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…