Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kuwa na serikali moja, itapelekea Zanzibar kuwa mkoa; ingawa si rahisi kwa wanufaika kukubali.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakika kama tunataka muungano kudumu suluhisho ni serikali moja ya muungano. Zanziba inaweza kua na madaraka ya ndani kiasi lakini sio kwa level hii ya sasa. Serikali ya zanzibar inaweza kuongozwa na waziri mkuu toka chama chenye wabunge wengi badala ya rais lakini madaraka ya rais wa jamhuri ya muungano kuonekana zanzibar. Uwepo wa serikali tatu hakika ni sahihi ya kuvunjika muungano kwani wasioutaka wataweza kuleta chokochoko na fitna na hatimae muungano kuvinjika kwa urahisi kutokana na kila upande kua na serikali yakeWanabodi,
Kama kawa, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa. Leo niko Mbeya, hiki kibaridi cha Mbeya, kwa sisi tulio zoea mablangeti yale, hata ujifunike na blangeti zito kiasi gani, kabaridi bado unakasikia!, mpaka saa hizi uzingizi umegoma!, hivyo the best company na companion ni kushuka jf.
Huu mjadala wa IGA ya DPW na Bandari zetu, unatusaidia kwa mengi, sasa kuna watu wanaanza kuhoji serikali ya Tanganyika, wanataka serikali 3.
Hoja nyingine mjadala huu wa IGA ulizotusaidia ni hizi
- IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria vilaza wa Ajabu. Je, Bunge letu na Serikali navyo ni vya Ajabu?
- IGA ya DPW imetusaidia mambo mengi. Kwanza kuonyeshea tuna wanasheria wa aina gani, pili kuidogosha fani ya sheria na sasa kila mtu ni Mwanasheria?
- Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
Sasa Watanzania wanahoji muungano na kuitaka serikali ya Tanganyika.
Huku kuhoji hoji muungano kunakoibuliwa sasa nako zinageuka ni kero ya muungano, kwa maoni yangu, dawa ya pekee na tiba ya kweli na ya kiuhakika ya kutibu kero zote za Muungano, ni kuwa na serikali moja!. Swali ni Je Tanzania sasa mmefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye serikali moja?
Mimi ni mtu wa mastori mastori, kama wewe ni mtu wa short and clear, ishia hapa na ku jump kule kwenye conclusion, wale wa mastori tuendelee
Mastori ya Pasco
Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu...
Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.
Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa
Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, ni kwaajili ya Zanzibar tuu, lakini mabadiliko hayo hayatambuliwi na katiba ya JMT.
Conclusion
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, hili pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa mmefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye serikali moja?
Wasalaam,
Paskali.
Endelea kuotaHapa nakuunga mkono; serikali moja ndio suluhisho ili kuondosha upande wa pili kudai hawaruhusu Mtanganyika kumiliki ardhi Zanzibar eti itapoteza utamaduni wake!!!!
Maamuzi yanayotolewa yanatakiwa yaathiri pande zote mbili sio wa upande wa pili kunufaika na jasho la upande mwingine.
Ni kosa mkoa kuwa na katiba na sheria zake zinazokinzana na katiba ya Jamhuri wa Muungano
Endelea kuotaSerikali 1 ndio
Naunga mkono hoja ✔️ ingawa kuna wazalendo uchwara humu walituita tuna akili za ukoloni!! Africa nzima ilipaswa tawaliwa kwa miaka zaid mbele ndipo kungekua na maendeleo ✔️Masikini.
NCHI zetu karibu zote Africa ziliwahi mno sana kupata uhuru wake Mapema.
NASIKITIKA KOSA kubwa waliloolifanya wakoloni ni kuziacha NCHI hizi zijitawale mapema.
AFRIKA TULIPASWA kupata uhuru kuanzia Mwaka 2000.
AFRIKA Kuna LAANA.
AFRIKA Kuna VIONGOZI WAPUMBAVU
AFRIKA KUNA MAJUHA.
AFRIKA KUNA MIUAJI.
MIFISADI.
MAJIZI
WAZUNGU hamkupaswa kutupa uhuru Mapema mngetusaidia kama south Africa
Viongozi wengi waliotawala baada ya mkoloni wengi walikuwa wabinfsi,walikuwa wanajiona wana akili kuliko wanaowatawalaMasikini.
NCHI zetu karibu zote Africa ziliwahi mno sana kupata uhuru wake Mapema.
NASIKITIKA KOSA kubwa waliloolifanya wakoloni ni kuziacha NCHI hizi zijitawale mapema.
AFRIKA TULIPASWA kupata uhuru kuanzia Mwaka 2000.
AFRIKA Kuna LAANA.
AFRIKA Kuna VIONGOZI WAPUMBAVU
AFRIKA KUNA MAJUHA.
AFRIKA KUNA MIUAJI.
MIFISADI.
MAJIZI
WAZUNGU hamkupaswa kutupa uhuru Mapema mngetusaidia kama south Africa
Sii kweli!.Masikini.
NCHI zetu karibu zote Africa ziliwahi mno sana kupata uhuru wake Mapema.
NASIKITIKA KOSA kubwa waliloolifanya wakoloni ni kuziacha NCHI hizi zijitawale mapema.
Sii kweli!. Naomba nikuulize swali dogo, nchi za Liberia na Sierra Leone zilipa uhuru lini?AFRIKA TULIPASWA kupata uhuru kuanzia Mwaka 2000.
Sii kweliAFRIKA Kuna LAANA.
Kweli but sio Africa pekeeAFRIKA Kuna VIONGOZI WAPUMBAVU
Kweli but sio Africa pekeeAFRIKA KUNA MAJUHA.
Kweli but sio Africa pekeeAFRIKA KUNA MIUAJI.
Kweli but sio Africa pekeeMIFISADI.
Kweli but sio Africa pekeeMAJIZI
Fafanua kivipi?.WAZUNGU hamkupaswa kutupa uhuru Mapema mngetusaidia kama south Africa
Asante, niko MbeyaVipi mkuu, kwema? Pole kwa baridi mkuu. Kwani haupo nyumbani?
Muungano wetu ni muungano adhimu, tumheshimu, usiuite muungano wa kitapeliTurudi kwenye hoja, hii bandiko lako ndo linazidi kuchanganya zaidi ya kuelewesha kuhusu mkanganyiko wa huu muungano wa kitapeli.
Yes nchi iliyokuwa ikiitwa Zanzibar, ilikufa sambamba na Tanganyika, kilichopo ni sehemu inayoitwa Zanzibar ambayo ni sehemu ya JMT.Unasema eti nchi ya Zanzibar ilikufa lakini bado ina serikali yake na katiba yake.
Nchi ya Tanganyika nayo sio tuu ilikufa bali, ilikufa na jina la Tanganyika pia likafa, ila kuna la Zanzibar likabaki. Nchi mpya ya Tanzania, ikazaliwa, sehemu iliyokuwa Tanganyika ikawa Tanzania Bara, sehemu ilikuwa Zanzibar ni Tanzania Visiwani.Unasema Tanganyika nayo kama Zanzibar imekufa, wakati siyo kweli kwamba Zanzibar imekufa kama ilivyokufa Tanganyika.
Kwenye hizo sehemu mbili, sehemu ya iliyokuwa Tanganyika iko ndani ya Tanzania ila sehemu ya Zanzibar ilipewa mamlaka yake ya ndani kwa mambo yasiyo ya muungano, ndio maana ina katiba yake, wimbo wake wa taifa, na serikali yake, rais wake, eneo lake etc.Sikuelewi unaposema “Nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili. Sasa mkuu, hizo sehemu mbili ambazo moja ina katiba yake na serikali yake, na nyingine haina, unaona ni muungano wa kuweka tu Serikali moja na itakuwa sawa?
Hili ni eneo ambalo Watanzania wanapaswa kuelimishwa, watu wanachanganya nchi na eneo, kwenye Bible neno Mungu na nchi, neno nchi ni eneo. Hivyo neno nchi kwenye katiba ya Zanzibar inamaanisha eneo, lakini nchi kwa maana ya nchi, Zanzibar sio nchi bali ni eneo la Zanzibar ambalo ni sehemu ya JMT. Nchi ni moja tuu, Tanzania.Zanzibar ina serikali yake ambayo wewe unaiita “ya ndani”, na siyo nchi, hiyo nchi imetowekaje?
Nimeelimisha sana humu kuhusu aina kuu mbili za miungano ya nchi, ni miungano ya union na federation. Muungano wetu ni unique, kimataifa ni muungano wa union, ambapo Tanzania ni nchi moja yenye serikali moja ya JMT na rais mmoja wa JMT ambaye ni Mkuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali, na Amiri Jeshi Mkuu. Lakini Kitaifa muungano wetu ni federation ya nchi mbili, Tanzania bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, zina katiba mbili, serikali mbili, marais wawili. Kwenye federation hii Serikali ya JMT ndio hiyo hiyo serikali ya Tanganyika. Kwenye mambo ya muungano, serikali ya JMT ni serikali ya muungano, kwenye mambo yasiyo ya muungano, serikali ya JMT ni serikali ya Tanganyika.Na wakati bado unasema hiyo “sehemu” imemezwa kama Tanganyika lakini kwa ndani muungano ina serikali yake. Sasa hiyo serikali siyo ya nchi ni kitu gani?
Kila kitu kimesemwa kwenye katiba ya JMTAu kwasababu unaita eti “sehemu” moja ya muungano. Ni wapi kwenye katiba hiyo sehemu imemezwa kama Tanganyika ambayo kiukweli inatawiwa na Zanzibar kwa kupitia kivuli cha muungano?
Maswali mengine...Halafu eti muungano ni wa kimataifa tu. Mkuu Ebu tuanze na kitu kimoja kabla ya kuendelea sana na mjadala.
Maana Ikiwa mungano ni kwa kimataifa yani serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania peke yake, ndo inatambulika kimataifa peke yake na Zanzibar haitambuliki, ila kwa ndani peke yake ndo utambuwe kwamba muungano huu upo hivyo ulivyo kwasababu maalum. Na hizo sababu, ndizo zilizofanya kusiwepo na serikali moja. Sababu hizo zilizokuwepo, sidhani kama zimejiishia zenyewe tu.
itakuwa ni serikali moja ya JMT yenye rais mmoja wa JMT. Zanzibar itakuwa ni mkoa.Ebu tuwekee hapa mfumo wa hiyo serikali moja utakavyokuwa ili Zanzibar nayo ipotee kiukweli kama Tanganyika ilivyopotea. Na yenyewe imezwe na hiyo katiba ya serikali moja ya jamuhuri kama Tanganyika ilivyo mezwa.
Wazanzibari hawatakubali hili katu....kabla ya 1964 Zanzibar ilikuwa nchi kamili kumbuka hilo, sio rahisi nchi kumezwa kirahisi hivyo.Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa mmefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye serikali moja?
Bora tuwe na muungano kama (China na Hongkong) au (China na Macau)....one country two systemsKwenye hizo sehemu mbili, sehemu ya iliyokuwa Tanganyika iko ndani ya Tanzania ila sehemu ya Zanzibar ilipewa mamlaka yake ya ndani kwa mambo yasiyo ya muungano, ndio maana ina katiba yake, wimbo wake wa taifa, na serikali yake, rais wake, eneo lake etc.
Umekaa ukashauriana na halmashauri ya ubongo wako na ukakubali kuandika pumba hizi!! Nauhurumia mwili wako tu kuwa mkokoteni wa kubeba kichwa cha kufugia nywele.Masikini.
NCHI zetu karibu zote Africa ziliwahi mno sana kupata uhuru wake Mapema.
NASIKITIKA KOSA kubwa waliloolifanya wakoloni ni kuziacha NCHI hizi zijitawale mapema.
AFRIKA TULIPASWA kupata uhuru kuanzia Mwaka 2000.
AFRIKA Kuna LAANA.
AFRIKA Kuna VIONGOZI WAPUMBAVU
AFRIKA KUNA MAJUHA.
AFRIKA KUNA MIUAJI.
MIFISADI.
MAJIZI
WAZUNGU hamkupaswa kutupa uhuru Mapema mngetusaidia kama south Africa
Hapa umesema kweliHili ni eneo ambalo Watanzania wanapaswa kuelimishwa, watu wanachanganya nchi na eneo, kwenye Bible neno Mungu na nchi, neno nchi ni eneo. Hivyo neno nchi kwenye katiba ya Zanzibar inamaanisha eneo, lakini nchi kwa maana ya nchi, Zanzibar sio nchi bali ni eneo la Zanzibar ambalo ni sehemu ya JMT. Nchi ni moja tuu, Tanzania.