Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?

Wewe nawe, hiyo mi laana uliyoandika hapo yote ya nini? changamoto hiyo ya Zanzibar nchi ama si nchi ni changamoto ambayo haimpunguzii mtanzania wa kawaida chochote, inajadiliwa twitter na jamii forums
Kuna nchi zina changamoto kubwa, ma vita, ukabila, etc huko kwengine wanapinduana, kwetu huku changamoto zetu ni za watu wakae wabishaane we, ila usiku tunalala na kesho kukikucha tunaamka

Kwahiyo hayo malaana uliyoandika hayana maana.
 
Nyerere hakuwa na msimamo wa kutaka Muungano, hata huu uliopo haukuwa ni wazo lake au kuwa waliupenda sana yeye au karume.

Nyerere alikuwa ni "secessionist", ushahidi kamili ni Biafra huko Nigeria. Nyerere alikuwa tayari waingie vitani huko lakini watengane.
 
Nyerere hakuwa na msimamo wa kutaka Muungano, hata huu uliopo haukuwa ni wazo lake au kuwa waliupenda sana yeye au karume.
With due respect, naomba kukumbia wewe dada yangu FaizaFoxy , Nyerere utakuwa humjui!. Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere was a true patriotic Pan Africanist who practiced Pan Africanism. Alikuwa yuko tayari kuuchelewesha uhuru wa Tanganyika kuwasubiria Kenya na Uganda!.
Nyerere alikuwa ni "secessionist",
Naomba msaada wa ufafanuzi wa secessionist
ushahidi kamili ni Biafra huko Nigeria. Nyerere alikuwa tayari waingie vitani huko lakini watengane.
Biafra was a special case!, Nyerere ni mpenda haki, alikuwa anatetea haki ya jimbo la Biafra.
P
 
Wewe umeongea kwa kupendelea sehem moja.
Je, huon tukiweka serikali moja ndo mattizo yatazidi, jumlisha ubaguzi uliopo saizi utazidi mradufu.
Ziwepo serikali mbili ili kila nchi ipambane na hali yake. Hakuna atakaemlaumu mwenzake.
 
Wewe umeongea kwa kupendelea sehem moja.
Je, huon tukiweka serikali moja ndo mattizo yatazidi, jumlisha ubaguzi uliopo saizi utazidi mradufu.
Ziwepo serikali mbili ili kila nchi ipambane na hali yake. Hakuna atakaemlaumu mwenzake.
Serikali moja ndio dawa na suluhisho la kudumu la kero zote za muungano.
P
 
Serikali Moja ndiyo "muarobaini wa kero zote za Muungano kwa pande zote mbili". Tusidhubutu kwenda kwenye mfumo wa serikali Tatu tutakwama kabla hatujaanza!!!
 
Serikali moja ni swala la muda tu, liko njiani. Maono ya Nyerere ilikuwa ni serikali moja. Wazanzibar wanaofahamu na kufaidi matunda ya muungano wanazidi kuongezeka siku hadi siku, idadi ya wazanzibar wanaoufahamu ubora na utajiri na umuhimu wa Tanganyika kwao inazidi kuongezeka, idadi ya watanzania wenye mzazi mmoja mbara na mzazi mwingine mzanzibar inazidi kuongezeka pia, idadi ya watanganyika wanaoishi zanzibar na kuishi bila bughuza inazidi kuongezeka siku hadi siku. Hata mama Samia kwa kukaa pale Ikulu ya Tanzania atakuwa mtu wa mwisho kukubali Zanzibar ijitenge, Tanginyika ina utajiri mkubwa wa kutisha ambao kama utatumika vizuri unatosha kuzilisha tanganyika na Zanzibar bila shida yoyote. Utajiri wa bandari tu za Tanganyika unatosha kuendesha uchumi wa tanzania yote. Wazanzibar wenyewe wanajiona salama sana kama wakiwa Tanganyika kuliko kuwa Zanzibar.
 
Leo tunapo adhimisha miaka 60 ya huu muungano wetu adhimu, nafanya tafakuri, niliwahi kuandika nini humu kuhusu muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya muungano wetu adhimu.
Ujumbe wangu ni muungano wetu adhimu udumu milele, na sasa ni muda muafaka tuachane na huu muungano wa kimaghumashi, wa union na federation, sasa twende kwenye muungano wa kweli wa union wa nchi moja, serikali moja, na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Tusaidie
P
 

Naunga mkono serikali moja maana huu utaratibu wa sasa una mapungufu makubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…