Je, Umempata unayemtafuta huku Love Connect?

ShyaRuwa

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
7,895
Reaction score
13,643
Habari zenu wanajamvi wenzangu?

Nimeanzisha huu uzi ili kuja mafanikio ya hili jukwaa kwa watu wanaolitumia kutafuta wenzi wao, yaani wachumba, wanandoa hata rafiki wa karibu kutoka humu ndani. Kama umewahi kumpata uliyemtafuta kutoka humu JF tafadhali tujulishe ili kuwatia moyo wale wanaondelea kutafuta.

Nawatakia wakati mwema.
 
humu kumejaa micharuko, kiukweli sijawahi kukutana na mtu serious ujoti tupu
Jipe moyo mkuu anayetafuta ndiye atakayepata ila usisahau kuangalia hapo mtaani pia.
 
Humu hakuna tofauti sana na mitaani,kuna watu wa kila aina kikubwa ni kuwa makini na watu unaokutana nao pia usisahau kumshirikisha Mungu kwani waliopo humu ni watu sawa na waliopo mitaani kuna matapeli wa mapenzi,kuna magolddigger,kuna wa kuchezeana tu,kuna waongo ,kuna kuna wenye mapenzi ya kweli na nia thabiti,n.k.
Kikubwa ni mtafutaji kuwa makini kuwabaini watu anaokutana nao ni wenye tabia zipi kama ilivyo tu huko mitaani,makazini,vyuoni,makanisani na misikitini. Hii ni kulingana na uzoefu wangu hapa jukwaani!
 
Kwa uzoefu wangu ni kuwa makini sana na uwe mtu wa kumchimba mtu mpaka umfahamu sana. Usiogope kuuliza maswali tena yale ya mtego na wakati mwingine unatumia mbinu ya kujifanyisha jambo fulani ili kupata reaction ya upande wa pili na itakufunza kama mtu anakupenda au amekuja kwako kimaslahi. Ukifanya haraka utaumizwa sana kwa kuwa kuna watu wako humu wanategeshea tu utangaze ndipo wapate upenyo wa kukutaka kimapenzi na kutokomea. Wengine watakuuliza maswali ya kipato ili waweze kukutapeli au kukutumia kama mtaji. Wengine watauliza vitu kadha wa kadha. Ukweli ni kuwa na msimamo na usiende kwa pupa kujieleza sana hasa hali yako ya kifedha, mali na kazi yako ikiwemo cheo kama unacho. Ukiwa firm baada ya muda utaona wenyewe wanajiondoa taratibu bila kufukuzwa.
 
Minaoga tu watu huku wanatafuta kujua kazi za watu na sio kutafuta mpenzi/mume/mke nk
 
Duhh...kwani hata kwenye basi la mwendokasi huko umekosa jamani...?? Hahah
 
Kwa uzoefu wangu ni kuwa makini sana na uwe mtu wa kumchimba mtu mpaka umfahamu sana. Usiogope kuuliza maswali tena yale ya mtego na wakati mwingine unatumia mbinu ya kujifanyisha jambo fulani ili kupata reaction ya upande wa pili na itakufunza kama mtu anakupenda au amekuja kwako kimaslahi. Ukifanya haraka utaumizwa sana kwa kuwa kuna watu wako humu wanategeshea tu utangaze ndipo wapate upenyo wa kukutaka kimapenzi na kutokomea. Wengine watakuuliza maswali ya kipato ili waweze kukutapeli au kukutumia kama mtaji. Wengine watauliza vitu kadha wa kadha. Ukweli ni kuwa na msimamo na usiende kwa pupa kujieleza sana hasa hali yako ya kifedha, mali na kazi yako ikiwemo cheo kama unacho. Ukiwa firm baada ya muda utaona wenyewe wanajiondoa taratibu bila kufukuzwa.
Mim nimechoka maisha ya upweke nataka nipate mke,tukapime nikajitambulishe kwao na kutoa posa
 
Habari zenu wanajamvi wenzangu?

Nimeanzisha huu uzi ili kuja mafanikio ya hili jukwaa kwa watu wanaolitumia kutafuta wenzi wao, yaani wachumba, wanandoa hata rafiki wa karibu kutoka humu ndani. Kama umewahi kumpata uliyemtafuta kutoka humu JF tafadhali tujulishe ili kuwatia moyo wale wanaondelea kutafuta.

Nawatakia wakati mwema.
Upweke unachosha,acha tupate wake tukajitambulishe kwao tuanze maisha
 
kama kuna manzi bado anataka mume naomba anistue .
 
Mim nimechoka maisha ya upweke nataka nipate mke,tukapime nikajitambulishe kwao na kutoa posa
Utakuwaje mpweke wakati wanawake kwa idadi ni wengi kuliko wanaume? Kama uko serious hakuna utapeli utanpata mke mwema tu. Ninaamini wapo kama na wewe umetulia kweli na unamaanisha.
 
Kuna kupata kweli humu? Kuna mtu anajiita Natafuta huu kama mwaka wa tisa hivi akianza kujiita nimepata basi hapo tutajua kua kupata kumo
 
Kwa dharau tu eti Manzi basi jua utampata yule ambaye naye si mke bali ni wa maslahi. Hata kama pengine ningekuwa nahitaji mtu siwezi kuwa namtu wa lugha ya dharau kama hii. Our actions symbolize who we real are.
yaani umemjibu vema mpaka nimekuona ....
 
Kwa dharau tu eti Manzi basi jua utampata yule ambaye naye si mke bali ni wa maslahi. Hata kama pengine ningekuwa nahitaji mtu siwezi kuwa namtu wa lugha ya dharau kama hii. Our actions symbolize who we real are.
Kila la kheri. .
 
Back
Top Bottom