beneli
Member
- May 1, 2013
- 86
- 7
Baada ya heka heka , kukosa usingizi na wasiwasi wa muda mrefu, wanafunzi wenye vigezo vya ufaulu kidato cha sita na diploma wamepata matokeo ya vyuo pamoja na kozi walizozichagua, wote twajua kuwa kuna machaguo takribani matano wakati wa kufanya uchaguzi wa kozi, kuna zile kozi na vyuo ambavyo ni vya kujazia tu na zile ambazo ni kozi na vyuo ambazo ziko moyoni kabisa mara nyingi huwa chaguo la kwanza, swali langu kwa wanachuo watarajiwa ni Je ? Umependa kozi uliyochaguliwa na chuo husika ? Kama ikitokea umepata nafasi ya kubadilisha ,Je ? Utabadilisha kozi yako tu na kubaki katika chuo hiko hiko ? Ama utabadilisha chuo tu na kubaki kozi hiyo hiyo ? Au utahama chuo na kozi ? Kuwa huru kusema chuo na kozi ambayo ungependa uwe.Karibuni