Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
Je umeshawahi kusikia stori ya kuku aliyeishi miaka miwili bila kichwa ?
Karibu!!..
Mnamo tarehe 22 oktoba *mwaka 1945*, gazeti kongwe la huko marekani linalojulikana kama *'life magazine'* lilitoa habari inayomuhusu kuku aliyekatwa kichwa lakini aliendelea kuishi kwa muda wa miezi 18 zaidi.
Habari hiyo iliwastua sana watu na kufanya waanze kuifuatilia kwa kina, huku wengi wao wakiamini sio ya kweli.
Ilikuwa hivi[emoji1541].
Ilikuwa ni siku ya tarehe 10 September mwaka 1945, katika mji wa *Fruita* uliopo Colorado huko Marekani ambapo familia ya bwana *Lloyd Olsen* ilitembelewa na mgeni wao, na ndipo alipoamua kukamata kuku wake mmoja ili amchinje na kupata *kitoweo* kwa ajili ya chakula cha usiku.
Lakini kitu cha kushangaza kilitokea Baada ya kumaliza kumkata shingo kuku huyo, ambapo alionekana bado *yu Hai* na mwenye nguvu thabiti za kuweza kutembea.
Kuona vile, bwana Olsen aliingiwa na *mshangao mkubwa* ulioambatana na hofu kwani, kitu hiko hakuwahi kukiona wala kusikia.
Baada tukio hilo, habari zilianza kutapakaa katika mji wote wa fluita huku Watu wengi wakimiminika nyumbani kwa bwana *Olsen* kujionea maajabu hayo.
Kituo kimoja cha habari cha pale pale Fruita, kilimtuma mwandishi wake kwenda kuhakiki pamoja na kufanya mahojiano na bwana olsen.
Habari zikaendelea kusambaa zaidi na kusababisha Watu wengi kudhani ni 'hadithi tuu za kutungwa.'
Ndipo siku moja bwana Lloyd Olsen alimbeba kuku huyo na kwenda nae katika *chuo kikuu cha Utah* ili tu kuthibitisha kwamba hiyo stori ni ya ukweli, na wala si uzushi kama wengi wanavyodhani.
*
Naam hayo ndio maajabu ya kuku ambaye alipewa jina la *Mike*.
Bwana Lloyd Olsen anasema baada ya kuona kuku huyo hajafa, akamuonea huruma na kuanza kumpa chakula ili aone pengine angeendelea kuishi au lah!..Ndipo sasa akawa anampa mchanganyiko wa maziwa na unga unga wa mahindi kwa kumkamulia kupitia kwenye ule mrija wa chakula kwa kutumia *'dropper'.* (kama zile zinazotumika kunyunyizia dawa kwenye jicho, sikio).
Pia bwana Olsen, akawa anafanya nae ziara katika sehemu mbalimbali kwa ajili ya Watu kumuona 'kuku Mike' huku wakilipa.
Pia 'Mike' alikuwa anawekwa kwenye sehemu za maonesho ambapo Watu *hulipia kiingilio* kwa ajili ya kumuona. Unaambiwa kwamba bwana Olsen kwa wakati huo alikuwa anaingiza kiasi cha *dola $ 4,500* kwa mwezi. Ambayo ukiigeuza kwa thamani ya sasa ni sawa na dola $49,300.
Mnamo mwezi march 1947, Olsen akiwa anarudi kwenye 'tour' ya maonesho ya 'kuku Mike'. Mara ghafla kuku akaanza kuugua na hatimaye *Akafa*.
Hivyo, Baada ya kuishi kwa miezi 18 bila kichwa hapo ndio ukawa mwisho wa kuku huyo, maarufu kama *'MIKE' THE HEADLESS CHICKEN"* .
**
Olsen Alihuzunika sana, na hiyo kupelekea kuanzishwa kwa taasisi ya kumuenzi Mike huko mjini Fruita, ambapo Kulijengwa *Sanamu* ya kuku huyo kama ishara ya kumbukumbu.
Na pia inapofika mwezi mei ya kila mwaka mjini hapo, huwa kuna sherehe *festival* ya kumuenzi Mike, ambapo Watu wengi wanaenda kufurahi pamoja kwa michezo mbalimbali huku wakifanya 'barbeque' za *nyama choma za kuku*.
**
Mwisho.