Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Katika jamii tunayoishi kuna aina mbalimbali za ukatili ambao watu hutendewa na watu wengine eidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya lakini athari ya ukatili huwa na matokeo mabaya kwa mtendewa.
Zipo aina nyingi za ukatili kama ukatili wa kijinsia, ukatili wa kimwili, au ukatili wa kihisia. Jamii na vyombo mbalimbali vimekuwa vikijitahidi kupigana kutokomeza ukatili wa aina yoyote katika jamii ili iwe sehemu salama ya kuishi kwa wanadamu wote.
Pamoja na jitihada hizo kuna ukatili wa kihisia ambao huendelea na haujapewa nguvu kubwa sana katika kupambana nao na ukatili huu umekuwa chanzo kikubwa cha watu kujidhuru wenyewe au kudhuru wengine kwa kuwa huacha athari ya kisaikolojia.
Ukatili wa kihisia hutokea kwa kushambulia hisia za mtu iwe kwa maneno au vitendo vinavyo ashiria kumshusha thamani ya mtu na kumfanya ajione hafai au aliye na kasoro.
Ukatili wa kihisia unaweza anzia kwenye ngazi ya familia, shuleni au sehemu za kazi nk. Ukatili huu ukifanyika huchukuliwa kawaida kwa kuwa aliyetendewa hajaonesha kuumia mwili hivyo hakuna anayejali kumponya muhusika.
Athari za ukatili wa kihisia humuumiza mwathirika kila anapokumbuka kitu alichofanyiwa au kuambiwa na asipopata msaada wa kisaikolojia kuweza kuponya jeraha lake huweza kuanza kufanya ukatili kwa wengine au kujifanyia ukatili mweyewe kwa kuwa haoni tena thamani yake au ya kuwa na watu wengine.
Tujitahidi kutokuwasemea vibaya watu wengine au kuwatendea vitu vitakavyowaumiza kihisia na ikitokea kwa bahati mbaya watu hao wapate msaada wa kisaikolojia ili kuwaweka sawa kurudisha thamani yao.