Mimesikia mara nyingi tu watu wakisema hawawezi kutunza pesa zao au hawajui hata inaishaje. Wengine wanaweza kusema kuwa pesa ina majini ndiyo maana hawaelewi hata inavyoisha.
Njia moja nzuri ya kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima na kujuwa vizuri namna unavyotumia pesa zako ni KUANDIKA KILA SENTI INAYOTOKA MFUKONI MWAKO. Unapofanya manunuzi yoyote, andika. Unapotoa sadaka, andika. Unaposaidia mtu, andika.
Nakuhakikishia siku ukianza kuandika matumizi tu, utaanza pia kujifunza namna ya kudhibiti pesa yako. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, ukijua tu namna unavyotumia pesa yako, utaanza kujiona wewe ni mtumiaji wa pesa wa namna gani.
Nakutakieni siku njema.