Je umewahi kukumbwa na hali hili? Je kama ni wewe utaweza? Tupeane uzoefu

Je umewahi kukumbwa na hali hili? Je kama ni wewe utaweza? Tupeane uzoefu

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Nadhani wengi mmewahi kusoma somo la sayansi mada ya uzalishaji kwa shule za msingi au Reproduction kwa secondary

Wewe kama mwalimu wa somo husika wa darasa husika kuna mwanao yumo, Wewe mzazi ambaye pia ni mwalimu wa kiume una mtoto wako wa kike darasa husika aliyebalehe,je utaweza kufundisha mada ipasavyo?

Na kama wewe ni wa kike mwanao yumo darasa husika ni wa kiume utaweza kufundisha mada husika ipasavyo ?

Je kama wanao wawili wa kike na wa kiume wapo darasa moja ,vipi utaweza kufundisha mada husika ipasavyo?

Je mwanafunzi/wanafunzi ambao ni wanao wa kuzaa watafurahia somo na kulielewa,na je watakuwa huru kujifunza?

Fikiria ni wewe tu mwalimu wa somo husika shuleni kwako na walimu wengine hawawezi kufundisha somo hill

Kama umewahi kukutana na hali hiyo tupeane uzoefu ilivyokuwa
 
Unaweza ni kutokana na tofauti ambayo ulishawapa.. shuleni ni mwalimu kama walimu wengine nyumbani ni mzazi... Unafundisha tu haina shida
 
Unaweza ni kutokana na tofauti ambayo ulishawapa.. shuleni ni mwalimu kama walimu wengine nyumbani ni mzazi... Unafundisha tu haina shida
Unachora penis na vagina pale ubaoni na kuanza kuelezea::sipati picha hao wanangu watakuwa wananifikiriaje
 
Unachora penis na vagina pale ubaoni na kuanza kuelezea::sipati picha hao wanangu watakuwa wananifikiriaje
Hakuna jinsi upo kazini ikibidi na nyumbani unawaendelezea somo
 
Kama taaluma yako ni ualimu unafundisha bila wasiwasi.

Mzazi gani atakayeona aibu kumwelimisha mwanae? Labda chizi
 
Ndio nitaweza pasina shaka
Kuweza utaweza,je utakuwa huru kufundisha ipasavyo na ukumbuke mada hii ndo wanafunzi wanakuwa makini na maswali kibao ya wanafunzi,je utakuwa huru kabisa kutamka maneno kama yalivyo?
 
Kuweza utaweza,je utakuwa huru kufundisha ipasavyo na ukumbuke mada hii ndo wanafunzi wanakuwa makini na maswali kibao ya wanafunzi,je utakuwa huru kabisa kutamka maneno kama yalivyo?
nimekwambia ntawezaaaaa, na ntakua huru na ntafundisha kama kawaida kila kitu
 
Back
Top Bottom