Je! Umewahi kukutana na Gari zenye Namba Mpya lakini ni chakavu kuliko yako ulonayo?

Mwana Ilala

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
1,287
Reaction score
486
Hallo Wana-JF
Mimi huwa inanishangaza kitu kimoja barabarani, wakati unaendesha then ghafla unakutana na Gari kama yAko then unaitupia jicho, cha kustaajabisha unakuta namba ni Mpya hata mwezi haina,ila sasa,utadhania ni gari yenye namba series AA#.

Nina doubt kama zile Inspection institutes "JAAI/EAA"zilizopewa dhamana na Serikali yetu ya kukagua ubora wa magari yanayo agiziwa toka nje, kama zinafanya inavyotatikana. Haiwezekani gari inakuja hapa bongo ukiitazama sura haitazamiki. Eti naye kaagiza Gari Reconditioned.

Jaman....! tujali thAman ya hela yetu kwa kuhakikisha tunapata kile ambacho ni sawa na tulicholipia.hela yetu tunaipata kwa mazingira Magumu:wengine hudiriki hata kukopa ili mradi naye aweze kutatua tatizo la usafiri.

Sawa:unaweza usiwe na Uwezo wa kununua gari ya 2005/2006/08/09/10, basi tujitahidi tusichague Magar Makuu kuu kwenye Mtandao, Kisa gari inauzwa $600/350 nawe unAjisifia kuwa nimepata gari kwa bei rahisi kweli kweli. Kumbe kule kwao hiyo gari ilitakiwa kupelekwa Manispaa kuwa-recircled nawe unajisifia nimepata.

Ngoja nikomee hapa kwani kuna watu wana ushahid na hili jambo hasa wenzangu wa Clearing & Forwading.

Halafu kuna Makampuni huko Japan wao wakisha nunua Gari Mnadani hawanaga tena Muda wA kuikagua kama wafanyavyo "Autorec" hawa jamaa nawapa Big Up. Gari zao zinakuwa zimesimama hata ununue gari ya 1989 unaikuta kwenye Kiwango utadhani imetoka Kiwandani leo. Wenzao Beforward Ndio wanongoza kwa kuuza Gari Ngarangara/Mikaangafu.

Gari 4 hadi 6 kati ya 15 za Beforwrd ukizifanyia physical checkup lazima utazikuta na tatizo kama sio kasoro. Nmewahi kununua gari IST kwa hawa Beforward:gari ilikuja na Mlio/Mvumo wa Bearing zote kushney.Salaaleeeee.na ilikuwa na "EAA" Inspection Certificate.
 
Naunga mkono Autorec wanakagua gari zao vizuri na wanajali kuuza gari bora na siyo bora gari.
 
Na hata bei za autorec ni za juu kuliko wengine. lakini kama alivyosema jamaa gari inakuja vizuri mpaka unapenda
 
Yaani ziko nyingi tu, unaona gari maybe ni T 888 CKW, gari imechokaa, mie mwenyewe huwa najiuliza inakuwaje, kumbe linakuja limeshachoka eeh!
 
AUTOREC, CARJUNCTION nawakubali ile mbaya. Gar nilinunua 2011 ikiwa grade 4, kwakweli hadi leo hii miaka 3 injini haijaguswa na haina dalili.
 
Kampuni nyingi wanajitahidi lakini hao befoward ni kiboko wanajali faida kuliko huduma
 
Usilolijua ni sawa na usiku wa kiza!s Huyu jamaa huenda anafanya marketing au hajui anachoongea, naona anapondea tu kampuni za watu, hiyo kampuni unayosema mimi nilishaagiza magari hata sikumbuki ni mangapi, gari pekee ambayo ilikuwa na tatizo ni fuso moja tu, nayo representative alilinote kwenye email lakini mteja wangu akasema haina shida kwa bei hiyo value for money iko vizuri. WABONGO MKIUZIWA GARI CHA KWANZA MNAULIZA "NI NAMBA GANI?"...au "NI MILAAGE NGAPI?"..Badala ya kuuliza kama gari ina service history!!! NAMBA NA MILAGE ZINABADLISHWA NA WAJANJA, KISHA GARI INAPIGWA RANGI YA MKONO MMOJA NDIYO MTU ANAPIGWA NALO!
 

Cyberteq umenena vzr, watz utasikia km ngapi, namba gani, yani badala ya kuangalia uimara mtu anatoa macho kwenye namba
 
AUTOREC, CARJUNCTION nawakubali ile mbaya. Gar nilinunua 2011 ikiwa grade 4, kwakweli hadi leo hii miaka 3 injini haijaguswa na haina dalili.

very true autorec wako makini sana, nilinunua gari kwao ilipofika bandarini wakati wa ukaguzi watu wa tra wakasema tume-forge doc maana gari ilikuwa inaonekana kama vile mpya though ilikuwa 10 yrs old.
 
Hata SBT wako vizuri sana. Magari yao ni mapya na yana ubora. Mi nilinunua gari 2010 mpaka leo utafikiri imetoka juzi bandarini. Na kilomita hata laki hazijafika. Pata picha nilinunua gari ikiwa na km ngapi
 
Nashukuru kwa kutufumbua macho kaka
unataka kusema nini? Namba mpya hupewa gari au chombo chochote cha moto kinaposajiliawa kwa mara ya kwaza nchini. Au ukomo wa mawazo yako ndipo ulipoishia? kwa kiwango chako cha ufahamu unadhani huwezi kuingiza gari toka Kenya,Uganda ,Burundi wala Zambia? Usiwe mshamba wa mambo kaka. Jf ni ya wasomi.
 
umejibu vizuri kiongozi pia kuna gari zinanunuliwa ndani ya nchi kutoka kwa mashirikka kama UN so unaposajili ni lazima ipewe namba mpya
 
Hata SBT wako vizuri sana. Magari yao ni mapya na yana ubora. Mi nilinunua gari 2010 mpaka leo utafikiri imetoka juzi bandarini. Na kilomita hata laki hazijafika. Pata picha nilinunua gari ikiwa na km ngapi

Kilometa bongo?? Unajipa moyo mkuu, hizo maneno zinachenjiwa kalaga baho
 
Magari yanayoingia Tanzania lazima yafanyiwe inspection. Huenda hayo mabovu yalikuwa SU
 

ni matumizi tu....hata watu hivyo hivyo unaweza kukuta kijana kachakaa kuliko kibabu!!!!
 
Gari ilishaingia Zanzibar ikakaa miaka mi-4, ikavushwa Bongo ikapewa namba Mpya, itaacha kuonekana Mzee??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…