Mkuu kama hujatembea huwezi elewa hayaKwani kuna binadamu as in watu (homo-sapiens) wanakula hivi vitu!!!
Tembo wataadimika mkuu. Nakuambia Tanapa watakuwa na kazi nzito na kubwa mno kuliko kulinda majangili wa pembe pekeeTembo ana supu nzuri na nzito nyama yake ipo na nyuzi nyuzi nyingi, ukinywa supu yake abdala kichwa wazi lazima asimame nyuzi 90 kwa masaa 24
Ulikula huyo mbuzi?1 nungu nungu
2 mzoga wa mbuzi iliokufa days 3 ago nikapewa na wamasai cha kushangaza nyama inachefu nichunguze mzoga ni wa mtoto wa mbuzi
Umenikumbusha nimwambie wifi yako aniandalie bakuli la senene. Kesho nikiingia tu maskani sitaki kula chakula kingine chochote kabla ya kula seneneKuishi kwingi kuona mengi wakuu.
Habari za Leo ninyi nyote wakuu!
Ninaudhoefu kadhaa wa kuishi porini kulingana na kupenda Nature ama kuwa na Hobby ya kilimo na kufuga.
Nimeishi maporini Kwa nyakati tofauti tofauti na kukuta jamii zikila wanyama ambao kikwetu ni mwiko na hawaliwi ila jamii hiyo ndo unakuta chakula chao au ni mboga Yao pendwa!
Kanda ya ziwa ni ngumu kukuta watu wanakula.
Panya
Bundi
Mwewe
Kipanga
Fisi
Chui
Nyani
Ndezi
Funza wa kwenye magogo ya miti nk.
Hao ni ngumu na sikuwahi kuona tangu kukua kwangu.
Lakini Kwa mara ya kwanza nikiwa pwani nilishuhudia Nyani analika vizuri TU na watu jamii ya malila kutoka mbeya huko na waluguru kama sio wapogoro
Ni nusura TU nile nyani Kwa mpogoro kama sio mluguru bahati yangu nilikuwa na msukuma akanikataza Kwa kisuma Kisha nikaona kiganja Cha nyani wao walikuwa wanamuita abdalah kapotea.
Hapo alikuwa amebanikwa vizuri kwenye moto wa nje uroho ukaniingia na vile Kwa mtani wetu nikataka kujipimia kumbe nyani bana.
Nikiwa huko nilishuhudia panya wakubwa wanaliwa vyema TU wengine waliitwa ndezi hii ni mto Ruvu kulikuwa na makabila tofauti wakiwamo na wazaramo wenyeji wetu.
Pamoja na yote hayo sikula hao wanyama.
Sasa nimeenda mahali pengine tena nikakutana na wafipa na wabende nk asee wanafukia vitu vya ajabu sana na ikanifanya sasa nami nitest mitambo wanyama niliokula na kuona ni watamu TU na hawana shida labda shida uwe nayo wewe mwenyewe ni
Ndezi
Mwewe wakubwa kabisa wale wenye uwezo wa kubeba hata mtoto wa mbuzi
Chui
Mbawala
Nungunungu
Kasogo yeye
Nguruwe pori
Kuna mnyama fln jina limenitoka wale huchimba mashimo Kwa Kasi sana .
Hawa wanyama watamu sana.
Ajabu ni bawala hana mafuta hata Tone Moja yaani ni mnyama asiyechosha kumla lakini ndo hivyo hana mafuta kabisa kabisa pamoja na kuwa amenawili vyema!
Naangalia namna nipate mtu wa kumuandaa chatu vizuri naye ni mle TU kesi iishe.
Hao ni baadhi TU ya wanyama niliokula ambao kwetu hawaliwi
Labda Hawa ndo Kwa uchache huliwa huko kwetu
Nguruwe pori(kwanza hawako)
Ngiri hawapo pia
Nungunungu wapi wakubahatisha walaji ni wachache mno
Mbawala wapi ila SI Kwa wingi ..hasa shida kubwa ni koo mfano ukoo wetu ni mwiko kumla pasina sababu yoyote ya maana Mimi nimemla na Niko vizuri TU.
Wewe umewahi kula nini ambachi kwenu ama jamii yenu haili kabisa?View attachment 3631650
Hapo sijala Njusi TU labda vile simjuipanya buku
nguruwe pori
kumbikumbi
panzi
muhanga
nungunungu
njusi(anafanana na mbuzi)
Wadudu hao kwakweli ni watamu sana na wingi proteinUmenikumbusha nimwambie wifi yako aniandalie bakuli la senene. Kesho nikiingia tu maskani sitaki kula chakula kingine chochote kabla ya kula senene
Nilimla baadaee ndo nikagundua ila wakati nakula sikujuaUlikula huyo mbuzi?
Niliwahi kuchuna na kumkaanga Kwa ajiri ya kupata mafuta yake aloo ana mafuta ila ananuka mbaya siku nipate wa kumuandaa ataliwa TUAisee maeneo fulani Wazungu kutoka Paraguay walikuwa wanataka nyama ya Kenge na walikuwa na arosto Ile mbaya walikuwa tayari kutoa 100$
HahahaahNilimla baadaee ndo nikagundua ila wakati nakula sikujua
Mbona mpaka leo hii kuna jamii zinakula binadamu.Zamani mpaka watu walikuwa wanaliwa. Ni bahati tuu dunia imekataza hilo. Vinginevyo sijui hata
Naam umenikumbusha na komba alikuwa analiwa sana hukoHuku pwani nimekula komba ni mtamu sana
Wengine wapo wanafanana na na nyingu sema wao ni wanene na wantoka kwenye vichuguu vilevile asee wanalika vizuri TU. Sijui ndo hao?Kuna wadudu flani wanatoka kwenye vichuguu wanaitwa SWAA jamii ya kumbikumbi ila wao wakubwa kidogo lol watamu sana
Porini Kuna mambo mazuri sana hasa ikiwa mtundu wa mitengo nyama za ng'ombe hutakuwa nazi timeKatika kuishi kwangu porini muda mrefu, nilijikuta nafakamia wadudu na wanyama wa kila aina.
Nimekula kobe, kenge, nguchiro, kima, mbega, ndezi, kuhe, nungunungu etc.
Kuna sehemu niliishi nikaamua kufuga kuku. Kuna hawa wanyama waharibifu wakaanzisha bifu na mimi kwa kunichukulia kuku wangu; kicheche, suzi na pakapori. Ilibidi nianze kusuka mipango ya kuwawinda kwa mitego na wote niliishia kuwanasa na sikuwa na ajizi zaidi ya kuwatengeneza ndafu na kaugali kwa mbaaali!
Katika nyama zote niliinjoi sana siku nilipokuwa nyama ya kiboko! Ni tamu balaa huyo kasongo na noa wakasome!
Hii mbaya aseeZamani mpaka watu walikuwa wanaliwa. Ni bahati tuu dunia imekataza hilo. Vinginevyo sijui hata
Umetisha asee Mimi nyani siwezi kula na jamii zakeMi hakuna mnyana sijala kutoa fisi simba na chui..
Na upande wa ndege ni mbayuwayu tuu ndo sijaonja
Umekula vingi aseeNyama ya mbuni ni laini mno na tamu ila supu yake ni mbaya kama ya nguruwe
Hao wanaofanana na nyigu nawajua ila sijawahi kula bibi alikuwaga anawa HAO NINAOWAZUNGUMZIA WAKO KAMA KUMBIKUMBI WALE WANAOTOKA SANA MVUA IKINYESHA inasemekana kumbikumbi ukiwala unakua kiziwWengine wapo wanafanana na na nyingu sema wao ni wanene na wantoka kwenye vichuguu vilevile asee wanalika vizuri TU. Sijui ndo hao?