Je umewahi kunywa Juice ya karoti + machungwa cheki hapa

Je umewahi kunywa Juice ya karoti + machungwa cheki hapa

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,753
Reaction score
9,575
Habarini marafiki

Ifuaatayo ndo menyu ya kuandaa Juice ya Karoti na Machungwa

Mahitaji:

- Machungwa 20 au zaidi kutegemeana na jinsi upendavyo.
- Karoti 10 -17 hivi inategemeana anavyopenda
- maji safi yaliyochemshwa pamoja na sukari
- tangawizi, au vitunguu saumu ukipenda

Matayarisho yake:

Andaa machungwa na uyasafishe kwa usafi maji moto,
yamenye kati bila kutoa maganda yake huku ukiangalia yasivuijie kwenye kisagio
kisha yasage kwenye kisago chake moja baada la lingine. Ondoa mbegu zake na
weka kwenye bakuli kubwa.

Chukua Karoti zako zimenye na kuziosha kisha zisage kwa kisagio au brenda yake
changanya changanya kwenye yale machungwa kisha weka maji kidogo halafu
chukua tangawizi kidogo sana iliyosagwa changanya humo
Mwisho chukua sukari ambayo ulichanganya na maji ii ilainike nyunyiza kwenye
hayo machungwa na karoti weka maji upendayo ya kutosha halafu angali kama
juisi ni nzito au nyepesi, baada ya hapo ongeza tena kipunje cha kitunguu saumu
kisha weka korogo koroga vichanganyikane
Mwisho weka kwenye friji na tayari kunywa kwa kitu chochote kile
iwe keki, chakula cha kawaida, au maandazi

CC: Paloma, charminglady, Passion Lady, sweetylady, amu, Smile, Mamndenyi, lara 1, AshaDii, Madame B, Kaunga, Heaven on earth, The secretary, everlnsalt, gfsonwin, Bujibuji, watu8, Mtambuzi, kaka Bishanga (acha juisi za azam kunywa flesh) na marafiki zangu
wote wa hapa karibuni mjitayarishie na muone ilivyo tamu na radha nzuri kwa yeyote anayetaka
kutayarishiwa asisite kuniita nijek kwake nitamuandalie atabrooo maandalizi yangu!!! weeeee si mchezo!!
 
Last edited by a moderator:
Chungwa huwa linamenywa vipi pasipo kutoa yake maganda?
Nafikiri alimaanisha unalikata kati bila kumenya.
Ahsante mamy,hilo la kutupia kitunguu saumu ndio jipya ngoja nijaribu.
 
Mimi naomba kufahamishwa walipo wafanyabiashara fulani wa mashine za nyumbani kama za kumenyea matunda,kukata mboga e.tc.
One time niliwasikia kipindi cha sabasaba wakijitangaza kuwa wana vifaa mbalimbali vya nyumbani ambavyo unaweza kukata na kumenya kwa shape unayotaka na pia kuna combination ya machine inayofanya kazi zote kwa pamoja.
yaani kuanzia kumenya mpaka kutoa juice.
Tafadhali anayeweza kunielekeza ninapoweza kupata hizi machine rahisi za nyumbani anifahamishe.
 
Inavutia, Sjawahi jaribu hiyo, nashkuru, ngoja nitengeneze namie ntakupa feedback
 
nadhani ulitaka kusema tangawizi na iliki....lakini kitunguu saumu - naona ngumu kumesa!!!

asante lady furahia
 
Last edited by a moderator:
haulimenyi baba ila unalioshakwa maji moto na kukata
katikati kisha unablenda kwenye mashine yake
ukumbuki nilivyokuja mwaka jana nikawatengenezea au umesahau
Chungwa huwa linamenywa vipi pasipo kutoa yake maganda?
 
besti unaweka kama unapenda hata iliki nayo
ni njema ni mtazamo tu wa mtu na vile apendavyo
je ushajaribu kuitengeneza uone radha yake?[
QUOTE=Paloma;7274916]nadhani ulitaka kusema tangawizi na iliki....lakini kitunguu saumu - naona ngumu kumesa!!!

asante lady furahia[/QUOTE]
 
hata ukinikaribisha sio mbaya nije kukuonjea nione kama
nimeweza fundisha mtu ameelewa somo hapo juu
Inavutia, Sjawahi jaribu hiyo, nashkuru, ngoja nitengeneze namie ntakupa feedback
 
ondoa shaka kama uko dar au mwanza
tembelea soko kubwa la hapo uliopo kisha
nenda maduka ya vyombo watakupa vifaa
hivyo unavyohitaji na wala havina sio ghali sana
Mimi naomba kufahamishwa walipo wafanyabiashara fulani wa mashine za nyumbani kama za kumenyea matunda,kukata mboga e.tc.
One time niliwasikia kipindi cha sabasaba wakijitangaza kuwa wana vifaa mbalimbali vya nyumbani ambavyo unaweza kukata na kumenya kwa shape unayotaka na pia kuna combination ya machine inayofanya kazi zote kwa pamoja.
yaani kuanzia kumenya mpaka kutoa juice.
Tafadhali anayeweza kunielekeza ninapoweza kupata hizi machine rahisi za nyumbani anifahamishe.
 
haulimenyi baba ila unalioshakwa maji moto na kukata
katikati kisha unablenda kwenye mashine yake
ukumbuki nilivyokuja mwaka jana nikawatengenezea au umesahau

Loh..sasa yale maganda yawashavyo hiyo juice sio kuwa itakuwa inakereketa
 
hapana kuna style yake ya kulimenya wala haitaleta muwasho wowote dady!
ngoja nitakuja home tena niwatengenezee naona dady umeshasahau ulivyokuwa unajilamba
Loh..sasa yale maganda yawashavyo hiyo juice sio kuwa itakuwa inakereketa
 
Juice na thom? Sijawah test, ngoja nijaribu hii.
Ila hapo kwenye carrots ni vizuri ukizichemshe kdg sana, huwa zinasaidia kuepusha yale machenga yanotuwama na inakua haina haja ya kuchuja tena huwa na rangi nzuri. Tangawawizi ni kiungo kizuri sana kwa juice nyingi. Thanx
 
Thanx ladyfurahia really tumeifurahia hii juice. Nliitengeneza, watoto na babayao waliinywa pamoja na keki. Asante sana kwa maujuzi
 
Back
Top Bottom