Je, Umewahi Kusikia Deed Poll?

Je, Umewahi Kusikia Deed Poll?

Marichris

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2020
Posts
571
Reaction score
509
Hii ni nyaraka (document) maalumu inayotumika kubadili au kurekebisha majina katika nyaraka mbalimbali. Nyaraka hii ni kiapo cha kubadili jina, ambapo mwombaji katika nyaraka hii husema wazi majina ambayo alikuwa akiyatumia awali pamoja na majina mapya anayoyataka. Nyaraka hii hutengenezwa na mwanasheria na baadae husajiliwa kwa msajili wa nyaraka...

Karibuni kwa maswali.
 
mwanasheria
Naomba nisisitize jambo moja kwamba nyaraka hizi kama deed poll, affidavit nk, huandaliwa/ kutengenezwa na wanasheria ambae ni wakili anaetambulika na Mahakama Kuu, Sio kila Mwanasheria ni Wakili ila kila Wakili ni Mwanasheria. 🙏 🙏
 
Hii ni nyaraka (document) maalumu inayotumika kubadili au kurekebisha majina katika nyaraka mbalimbali. Nyaraka hii ni kiapo cha kubadili jina, ambapo mwombaji katika nyaraka hii husema wazi majina ambayo alikuwa akiyatumia awali pamoja na majina mapya anayoyataka. Nyaraka hii hutengenezwa na mwanasheria na baadae husajiliwa kwa msajili wa nyaraka...

Karibuni kwa maswali.
Vipi kama unataka kubadilisha mwaka wa kuzaliwa, unatumia njia gani kisheria?
 
Hii ni nyaraka (document) maalumu inayotumika kubadili au kurekebisha majina katika nyaraka mbalimbali. Nyaraka hii ni kiapo cha kubadili jina, ambapo mwombaji katika nyaraka hii husema wazi majina ambayo alikuwa akiyatumia awali pamoja na majina mapya anayoyataka. Nyaraka hii hutengenezwa na mwanasheria na baadae husajiliwa kwa msajili wa nyaraka...

Karibuni kwa maswali.
Shukrani sana kwa hii elimu ila natamani kujua yafuatayo:

a) Utaratibu upi natakiwa kufuata kama katika academic certificates zangu nilitumia majina 2 lakini kwa sasa niko kazini nataka kutumia majina 3 kama ilivyo kwenye national I'd?

b) Gharama za kwenda kusajili kwa msajili wa nyaraka zipoje au itategemea na sehemu?
 
Shukrani sana kwa hii elimu ila natamani kujua yafuatayo
a) Utaratibu upi natakiwa kufuata kama katika academic certificates zangu nilitumia majina 2 lakini kwa sasa niko kazini nataka kutumia majina 3 kama ilivyo kwenye national I'd?...
Njoo nikuandalie Deed Poll. Pia andaa Tshs 32000/= kwa ajili ya kusajili hilo jina. Nowadays inachukua siku 3 au 4 kusajiliwa.
 
Ni vizuri uwe unaeleza vitu kwa ukamilifu wake ukizingatia kuna watu wanajifunza hapa. Deed Pool ni document yoyote ambayo inakuwa executed na one party, na mfano wake ni hiyo nyaraka ya kubadili majina. Hivyo deed pool ni zaidi ya kubadili majina.
 
Back
Top Bottom