Je, umewahi kutapeliwa ukinunua gari mtandaoni, hasa Japan?

Je, umewahi kutapeliwa ukinunua gari mtandaoni, hasa Japan?

kintu

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
541
Reaction score
133
Mimi nimekuwa nikinunua magari mtandaoni kutoka Japan,lakini mara nyingi nimekuwa nikikutana na changamoto za hapa na pale na pia nina jamaa zangu na marafiki zangu wametapeliwa kwa njia tofauti tofauti au

- Kubadilishiwa gari na kutumiwa gari hisiyo uliyochagua.

- Kutuma hela baadae husitumiwe gari n.k

Hivyo basi ningependa tuelimishane kuhusu yaguatayo:-

1. Watu tupeane njia wanazofanya au ikibidi kuweka na kampuni ambazo zimekuwa zikitapeli watu .

2. Je, kuna njia gani mbadala ya kuweza kurudisha pesa iliyokwisha tumwa kwa muuzaji?

3. Je, kupitia barozi zetu au za Japan unaweza kupata msaasada wowote?

4. Ni njia zipi wamekuwa wakitumia kutapeli wakati wa kununua?

5. Je, ni njia zipi unazitumia kuakikisha unatuma/kununua kwa mtu/ kampuni sahihi?

Naomba kuwakilisha !
 
Ni kazi sana kutapeliwa hasa kwa biashara kubwa kama magari na mizigo mikubwa.
 
Bank hawausiki na transactions au manunuzi unayoyfanya zaidi ya kutuma TT.

Nikweli nimekumbana na changamoto za online transactions japo sijatapeliwa kwa asilimia 100. Nimekuwa nanunua magari kutoka japan tangu 2009,mara nyingi nimekuea nakutana na changamoto za hapa ja pale lakini pia kama nilivyosema kuna watu wengi wametapeliwa au kukutana na changamoyo na lengo langu ilikuwa kupeana uzoefu ,na njia mbadala za kuweza ku recover pesa yako kama umetapeliwa.
We unaonekana umetapeliwa unatafta justification kwa maboya wenzio tu! Hamna wizi wa kijinga namna hio ukizingatia bank zetu zinahusika kwa ukaribu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli inawezekana fake lakini nimekuwa mara nyingi natumia Tradecarview,sbt japan.beforwarding na mara chache hizo site za kampuni binafsi kama picknbuy24.com,everycar.jp etc.

Mfano nilinuninua gari tradecarview kwenye kampuni moja tukaelewana nikalipa tena kupitia huduma yao ya paytrade na wana huduma ya car check yaani wanafanya kulinganisha kile ulichangua kwenye gari na physical inspection kama kila kitu kipo sawa.

Lakini ujanja wanaofanya anakwambia gari haikupita kwenye inspection kwahiyo anakupa offer ya gari nyingine ambayo haipo wlkwenye record za tradecarview ,sasa ukikubali na tradecarview wakiona umekubali wanakuwa hawana kipingamizi.
Jamaa anatafuta gari yoyote ya bei ya chini anakutumia.
Pengine mdau aliingia kwenye acc fake za magari...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom