TUSHIRIKISHANE Je una maoni, ushauri au maswali kwa Mbunge Nape Nnauye kuhusu maendeleo ya Mtama?

Joined
Aug 9, 2016
Posts
13
Reaction score
67
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye Nape Nnauye amekuwa akishirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wananchi na Viongozi wa Manispaa katika kuleta maendeleo jimboni kwake kupitia mradi wa Tushirikishane.


Washiriki wa Warsha ya Tushirikishane Mtama katika picha ya pamoja na timu ya Jamii Media baada ya kumalizika kwa warsha ya siku tatu ya mradi huo.

Kufanikiwa kwa maazimio haya ya maendeleo kunategemea pia mchango wa wadau mbalimbali wa maendeleo ndani na nje ya Jimbo la Mtama.

Je una maoni yeyote kwa Mbunge kuhusu utekelezaji wa maendeleo jimboni mwake?

Una swali lolote kwa Mbunge? Unapendezewa na namna mbunge wako anafanya kazi?

Kwa mjadala wa Mradi wa Tushirikishane Jimboni Mtama, tembelea => TUSHIRIKISHANE - Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Mtama
 
maendeleo ya mtama? ameanzisha kilimo cha mtama au una maana gani? au mnataka muanzishe kiwanda cha kutengeneza unga wa lishe/uji wa mtama badala ya ulezi?
 
Nawatakia watu wa mtana kila la kheri kwenye uwakilishaji wa changamoto zao, nina imani na Nape kuliko mwana ccm mwingine yeyote.
 
Nape karibu CDM polepole akizingua

Don't put all egg on one Basket
 
Kipindi cha ziara ya raisi jimboni mtama tuliona kupitia runinga miradi mingi ya maendeleo jimboni kwake mtama imelala, mfano ujenzi wa zahanati, ambayo mh raisi aliahidi kutoa pesa

Swali kipi kinapelekea miradi ya maendeleo muhimu kama ile inalala ikiwa yeye mbunge yupo
 
Kiwanda cha mbolea kinajengwa link mkoani mtwara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…