Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lakini dini inafahamika na ndio maana nikikashfu dini ya mwenzangu nitachukiliwa hatua za kisheria, lakini kama nikutishia kukuroga sichukuliwi hatua yoyete.
dah!mkuu mbonaa na sikiaa huwezi kumuona kwa macho ya kibinadamu mchawii..au na wewee umeangaa kwenu banaaaUchawi hakuna,bali kuna imani za uchawi. Na ukizi puuza na kumuamini Mungu,hakuna cha kukutisha wala kukudhuru.
Asante Mkuu, maoni yamepokelewa na kufanyiwa kazi. Nilifundishwa kusikiliza ushauri na kuufanyia kazia.
Uchawi hakuna,bali kuna imani za uchawi. Na ukizi puuza na kumuamini Mungu,hakuna cha kukutisha wala kukudhuru.
kwani serikali ni nini? Inakuwaje serikali haiamini katika dini lakini viongozi wana dini? Haya yakipata majibu, hata la uchawi majibu yatapatikana
Siku nyingi nimekuwa siamini kama kweli kuna uchawi katika Tanzania hii, achilia mbali huko kwa wengine. Nimekuwa siamini kwa sababu makosa yote hapa nchini yana adhabu zake isipokuwa la uchawi hii ikimaanisha kuwa Serikali inaamini kuwa hakuna uchawi. Hatahivyo, siku za hivi karibuni imani yangu imeanza kupungua baada ya Kiongozi mmoja katika Serikali hiyo hiyo inayoamini kuwa hakuna uchawi kudai kuwa amegundaua mbinu kuwa anarogwa ili awe zoba auwawe kirahisi. Sasa nikajiuliza, huyu mtu yumo ndani ya Serikalini inayoamini kuwa hakuna uchawi, akiwa pekee yake kuna uchawi, inakuwaje hapa?
Aidha, jana tarehe 28/03/2011 nilikuwa nasikiliza Redio Wapo FM kuanzia saa 1.30 jioni kipindi cha yaliyotufikia nikasika kuwa kuna fisi ameshambulia watu huko Mto wa Mbu, akauawa na askari wa wanyama pori, baada ya kuuawa, wakakuta ametobolewa masikio kama alikuwa anawekewa hereni.
Je, huyu fisi alikuwa anashiriki mashindano ya Miss Mto wa Mbu au ni fisi wa wachawi?
Sasa wana JF wenzangu ni kweli kuna uchawi? Au ni njama za wajanja kutishia wenzao.
uchawi pamoja na imani nyingine zote supernatural ni fix tupu.
Hiyo ni sehemu ya mazingaombwe na mauza uza ya kukufanya uamini kuwa kweli uchawi upo. Lakini mwenye akili ya ukweli ulivyo hawezi kutishika eti kwa sababu mtu kachukua viungo vya uzazi vya mnyama. Unaweza kweli kulitumia hili kama kithibitisho cha kuwepo kwa uchawi? Samahani, naona tuko kwenye viwango tofauti mno vya uelewa wa mambo na itakuwa vigumu kueleweshana ikiwa haya ndo madai ya kuthibitisha kuwepo kwa uchawi.
Uchawi ni dhana. Ni dhana inayoishi na watu. Ziko dhana nyingi sana zinazoishi na watu hadi leo. Hata mira nyingi na desturi ni dhana tu ambazo zimejijenga kwa muda mrefu. Nyingine zina sababu za msingi, nyingine hazina sababu yoyote..
Agalia wakati mwingine spelling zaweza kuaribu maana ya kile ulichokusudia. Hebu hii " akawauwa na askari wa wanyama pori, baada ya kuauwa, wakakuta ametobolewa masikio kama alikuwa anawekewa hereini" Hii haijatulia.