Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Si muumini sana wa hii imani ila kuna kipindi fulani ilinibidi kuamini kuwa uchawi upo baada ya kila siku asubuhi kukuta damu mbichi chumbani kwangu.....yaani leo nitaikuta kwenye shuka nililotandika, kesho shuka nililojifunika, keshokutwa nitaikuta ukutani, siku nyingine sakafuni..... It was one of worse experience I ever had in my life!
 
Okoka upate kinga na ulinzi wa Yesu Kristo ndugu shetani ni mbaya sana na kwa bahati mbaya ana deal na wasio na imani imara.
MUNGU ndio kimbilio lako/letu.
Mtafute yeye anapatikana bure hahitaji tozo.
 
Zipo nguvu za aina mbili duniani.
1/Ya MUNGU
2/Shetani.

Shetani ndio hao wachawi, waganga, freemason, illuminant na mawakala kibao...
Unapaswa utambue hivyo kama ulikua hujui.
Mtafute MUNGU awe mlinzi na mkombozi wa maisha yako.
 
Zipo nguvu za aina mbili duniani.
1/Ya MUNGU
2/Shetani.

Shetani ndio hao wachawi, waganga, freemason, illuminant na mawakala kibao...
Unapaswa utambue hivyo kama ulikua hujui.
Mtafute MUNGU awe mlinzi na mkombozi wa maisha yako.
Hakika niliiona nguvu ya Mungu katika hilo!
 
Eti kama naenda Urusi, teh teh, tafuta namna nyingine ya kudanganya
 
Hapo,hiyo alikuwa ni kibaka anakumulika na tochi hizo za wachina,huwa zina mwanga sana
 
Kwanini uliamua kuamini ni uchawi na si jambo jingine lolote? Ukijibu hili swali utakuwa umetegua kitendawili! NB kiimani kuna nguvu nyingi ambazo binadamu huwa tunaamini. eg Kwanini hukuamini ni nguvu takatifu na ukaamini ni uchawi? Kwa nini hukuamini kuwa ni wale viumbe kutoka anga za mbali na ukaamini ni uchawi?
 
Tafsiri rahisi ya kitu cha ajabu ni uchawi. Hicho ndicho kilichomo kichwani mwa mtoa hoja. Hukufikiria kingine zaidi ya uchawi??
 
Sasa hapo uchawi uliokutana nao ni upi? Ni huo mwanga au kupotelewa na rafiki zako? Kama ni mwanga! Chaajabu ni kipi? Nini kilitokea baada ya huo mwanga?
NB: ACHA UOGA.
 
Mkuu uchawi upo ila hili lakwako nahic itakuwa ni kimondo tuu
 
Kitambo sana sijamroga mtu,ngoja nirudi tena kwenye kazi yangu ya uchawi
Nalog off
 
[QU niOTE="Chozilaurithi, post: 27738176, member: 484614"]Habari za muda huu tulivu wapendwa wangu wa Jf,

Niende moja kwa moja kwenye mada husika, ilikuwa siku moja nilikuwa natoka kuwatafuta rafiki zangu mitaani maana wao waliwahi kurudi nyumbani mimi waliniacha shule nikiwa nawasaidia walimu kusahihisha mitihani ya kidato cha pili,sasa niliporudi nyumbani sikuwakuta kwani tulipanga ktk nyumba moja.

Baada ya kuona hawapo nikaamua kipita mitaani kuwatafuta kwa bahati mbaya niliwatafuta kwa muda mrefu sana bila mafanikio, ilipofika saa tatu ya usiku nikaamua kuanza kurudi nyumbani tu maana wao sikuwaona

Sasa nikiwa njiani kuelekea nyumbani nilipofika karibu na kanisa nikashangaa nimemulikwa na mwanga mkali sana toka juu ya mti nilioupitia jirani yaani huo mwanga sijawahi kuuona tangu nizaliwe mpaka leo hii na huo mwanga baada ya kunimulika ulipotea juu kwa juu na kutoweka ghafla.

Kwa kuwa nilikuwa peke yangu ikabidi nianze kukimbia kwenda nyumbani aisee niliona nyumbani ni mbali kama naenda urusi hivi sijui wenzangu kama mmeshawahi kukutana na matukio ya ajabu ajabu kama yalivyonikuta mimi.[/QUOTE]
Huo sio mwanga ni moto wa kichawi unaitwa " Chenge" .Nadhani hata Yule Andrew Chenge jina chenge linatokana na uchawi huo.

Huo ni uchawi mkubwa sana na una siri nzito sana nyuma yake..Asili ya uchawi huo ni katika mkoa wa simiyu hususani wilaya za Maswa na Bariadi vijijini ( Gamboshi ).
Ni uchawi hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…