Chozilaurithi
Senior Member
- Apr 13, 2018
- 120
- 55
Uchawi ni ushirikina
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Je Unadhibitishaje Huo ni Uchawi.... Kwanini Asiwe malaika?Habari za muda huu tulivu wapendwa wangu wa Jf,
Niende moja kwa moja kwenye mada husika, ilikuwa siku moja nilikuwa natoka kuwatafuta rafiki zangu mitaani maana wao waliwahi kurudi nyumbani mimi waliniacha shule nikiwa nawasaidia walimu kusahihisha mitihani ya kidato cha pili,sasa niliporudi nyumbani sikuwakuta kwani tulipanga ktk nyumba moja.
Baada ya kuona hawapo nikaamua kipita mitaani kuwatafuta kwa bahati mbaya niliwatafuta kwa muda mrefu sana bila mafanikio, ilipofika saa tatu ya usiku nikaamua kuanza kurudi nyumbani tu maana wao sikuwaona
Sasa nikiwa njiani kuelekea nyumbani nilipofika karibu na kanisa nikashangaa nimemulikwa na mwanga mkali sana toka juu ya mti nilioupitia jirani yaani huo mwanga sijawahi kuuona tangu nizaliwe mpaka leo hii na huo mwanga baada ya kunimulika ulipotea juu kwa juu na kutoweka ghafla.
Kwa kuwa nilikuwa peke yangu ikabidi nianze kukimbia kwenda nyumbani aisee niliona nyumbani ni mbali kama naenda urusi hivi sijui wenzangu kama mmeshawahi kukutana na matukio ya ajabu ajabu kama yalivyonikuta mimi.