Uchawi ni imani muflis kuwa watu fulani wana nguvu fulani yenye uwezo wa kudhuru wengine. Hili jambo ni imani tu na imani hizo zimejikita katika jamii kweli kweli. Hao waliokuwa wakiitwa au wanaoitwa wachawi katika jamii huwa ni watu dhaifu sana, maskini na waoga wanaodharauliwa sana na jamii. Mara nyingi watu hao wakiitwa wachawi, hawakatai wala kukubali, kwani wengine hufikiria kuwa watu wakimuona ana nguvu hiyo ya ajabu (yaani uchawi) itakuwa ni sababu ya kuheshimiwa na kuogopwa.
Wengi wao hujiingiza katika matendo ya kufanya viinimacho au mazingaombwe ya kuwasadikisha watu kuwa wao kweli wanazo hizo nguvu na wana uwezo wa kudhuru. Kutokana na hilo, wakazaliwa watu wanaoitwa wachawi au walozi. Hawa watu wameanzisha utamaduni wao, kama zilivyo dini. Tofauti yao ni kuwa wao mambo yao hufanyika kwa siri, kwani lengo ni kuwadanganya watu waamini kuwa kweli wanazo nguvu za ajabu.
Hizi jamii za kichawi, kama secrete societies zingine hutoa sadaka na kufanya vitimbi vya hapa na pale vyenye lengo la kuwaaminisha watu kuwa wao wana nguvu zisizoonekana.
Lakini ukweli ni kuwa kama zilivyo jamii zote za siri, mambo haya yanagundulika na walio wengi kuwa si kweli. Wale wanaodanganyika wanabaki kuishi kwa hofu na wakati mwingine enzi hizo watu walilazimika kutoa kitu kidogo kwa wachawi ili wasirogwe. Huo ndo uchawi.
Ukiogopa vitimbi vyao, utajisalimisha kwao na kuwapa kitu kidogo ili wakulinde na uchawi.
Jamii ya wachawi ina umri mrefu kuliko hata dini zetu nyingi, ambazo nazo zimetumia mbinu kama zile zile wanazotumia wachawi kupambana nao. Mbinu wanayotumia wachawi ni kutangaza uwezo wa kudhuru watu kwa kutumia "magic". Dini zinatumia "nguvu za kimungu" kupambana na wachawi. Nguvu zote hizo ni 'supernatural'.
Kwa mtu mwenye scientific knowledge ya mwili wa binadamu na mazingira yake, uchawi ni kama hadithi za riwaya kwake na hauna madhara yoyote!
Huo ndo uchawi!